ⓘ Free online encyclopedia. Did you know? page 140

Tarantula

Tarantula ni spishi za buibui katika familia Theraphosidae wa nusuoda Opisthothelae. Spishi za nusufamilia Harpactirinae huitwa bui-nyani. Spishi nyingi ni kubwa hadi kubwa sana na zote zina manyoya marefu mengi. Kwa kawaida huwinda kwa kuvamia m ...

Chande

Chande ni arithropodi wa oda Opiliones katika ngeli Arachnida wafananao na buibui. Kama hao chande wana miguu minane, lakini miguu yao ni mirefu sana katika spishi nyingi. Jozi ya pili ni mirefu kuliko mingine na hutumika kama vipapasio. Sehemu z ...

Funduku

Funduku ni utitiri mdogo sana wa familia Sarcoptidae katika oda Sarcoptiformes anayesababisha ugonjwa au hali ya ngozi iitwayo upele wa funduku. Utitiri huyu huishi katika ngozi ya watu na wanyama mbalimbali.

Utitiri (Arithropodi)

Kwa asili jina utitiri hutumika kwa ugonjwa wa kuku ambao unasababishwa na wadudu wadogo walio na mnasaba na kupe na papasi. Lakini kwa sababu hakuna jina la jumla la Kiswahili kwa kundi la Acari" utitiri” hutumika zaidi na zaidi kwa spishi nying ...

Utitiri-mahameli mkubwa

Utitiri-mahameli mkubwa ni utitiri mkubwa wa familia Trombidiidae katika oda Trombidiformes ambaye ni baini ya spishi kubwa kabisa za matitiri.

Utitiri-utando madoa-mawili

Utitiri-utando madoa-mawili ni utitiri wa familia Tetranychidae katika oda Trombidiformes aliye msumbufu mbaya katika mashamba na vibanda vya kukuzia mazao. Anashambulia spishi zaidi ya 1000 za mimea na kwa hivyo ni moja baini ya spishi zinazojil ...

Utitiri-utando mwekundu

Utitiri-utando mwekundu ni utitiri wa familia Tetranychidae katika oda Trombidiformes aliye msumbufu mbaya katika mashamba ya mboga. Inashambulia spishi za mimea za familia Solanaceae hasa na nyingi nyingine pia. Kwa asili spishi hii ilitokea Ame ...

Nge

Kwa matumizi tofauti ya jina hili angalia Akarabu Nge au akrabu kutoka Kiarabu عقرب ni arithropodi wa oda Scorpiones katika ngeli Arachnida. Spishi ndogo huitwa visusuli pia. Kama arakinida wote wana miguu minane. Pedipalpi zao ni kubwa na zina g ...

Nge-bila-mkia

Nge-bila-mkia ni arithropodi wa oda Pseudoscorpiones katika ngeli Arachnida. Kinyume na nge wa kawaida wadudu hawa hawana mkia, kwa hivyo jina lao. Ukubwa wao ni mdogo sana: mm 2-8; spishi kubwa kabisa ina mm 12 tu. Wanatokea mahali popote ambapo ...

Nyungunyungu

Nyungunyungu ni wanyama wadogo wenye umbo la neli wa oda Megadrilacea katika faila Annelida. Kwa kawaida huishi katika udongo akijilisha kwa viumbehai na waliokufa. Mfumo wa mmengenyo wa chakula wa nyungunyungu unanyumbua kupitia urefu wa mwili w ...

Fuko (mnyama)

Mafuko ni wanyama ambao wanachimba katika ardhi na kushinda takriban maisha yao yote chini ya uso wake. Wanyama hawa wamo katika oda na familia mbalimbali. Spishi za Afrika zimo katika oda za Afrosoricida na Rodentia. Oda Soricomorpha ina spishi ...

Vertebrata

Vertebrata ni jina la kitaalamu la kutaja wanyama wote wenye uti wa mgongo. Mifano ni mamalia, ndege, reptilia na samaki. Mwanadamu pia huhesabiwa humo kibiolojia. Vertebrata wana kiunzi cha ndani, neva kuu zinapitishwa ndani ya uti wa mgongo zin ...

Rusu (mnyoo)

Rusu ni spishi ya mnyoo kidusia wa familia Oxyuridae katika faila Nematoda anayeishi katika utumbo mpana wa watu. Husababisha mwasho katika eneo la mkundu. Ambukizo la rusu linaitwa enterobiasisi.

Trichuris trichiura

Mnyoo-mjeledi ni spishi ya mnyoo kidusia wa familia Trichuridae katika faila Nematoda anayeishi katika sikamu ya watu. Anaweza kusababisha kuhara na damu, na anemia, katika watoto hasa.

Mnyoo-bapa

Minyoo-bapa ni wanyama wanaofanana na minyoo, lakini wao hawana uwazi wa mwili. Kwa hivyo hawana ogani za mfumo wa mzunguko wa damu au za mfumo wa upumuaji na lazima mwili uwe bapa ili oksijeni iweze kuingia kwa mtawanyiko. Mwili wao una uwazi um ...

Kaa (mnyama)

Kaa ni wanyama wa faila Arithropodi, oda Decapoda na oda ya chini Brachyura ambao kwa kawaida wana mkia mfupi mno au fumbatio lao limejificha ndani ya kifua. Wanyama wengine wafananao na kaa, kama wanamezi, kaa-mfalme na kaangao, sio kaa wa kweli ...

Kamba (gegereka)

Kamba ni wanyama wa faila Arthropoda na oda Decapoda, lakini spishi za oda ya chini Brachyura huitwa kaa. Spishi ndogo huwa na majina kama uduvi, duvi, kijino na ushimbu. Mwili wa kamba una sehemu mbili: kefalotoraksi kichwa na kidari vilivyounga ...

Bundi (Tytonidae)

Bundi ni ndege mbuai wa familia Tytonidae na jenasi mbalimbali ya familia Strigidae. Ukurasa huu unahusu familia Tytonidae. Spishi hizi zina rangi ya kahawa nyuma na nyeupe mbele pamoja na madoa madogo meusi. Kichwa chao kina umbo la mviringo na ...

Bundi-panga

Bundi-panga ni ndege mbuai wa jenasi mbalimbali za nusufamilia Surniinae katika familia Strigidae. Wengi baina ya ndege hawa wana ukubwa wa bundi, lakini wengine ni wadogo zaidi na wengine wakubwa zaidi. Wana rangi ya kahawia au kijivu na wengi w ...

Kitaumande

Vitaumande ni ndege mbuai wa jenasi mbalimbali wa nusufamilia Surniinae katika familia Strigidae. Ndege hawa ni wadogo kuliko bundi na wana rangi ya kahawa au kijivu pamoja na miraba au madoa. Vitaumande hula panya na wanyama na ndege wadogo weng ...

Kokoko-mlasamaki

Kokoko-walasamaki ni ndege mbuai wa jenasi Ketupa na Scotopelia katika familia Strigidae. Siku hizi wataalamu wengi wanawaainisha katika jenasi Bubo. Ndege hawa ni wakubwa kuliko bundi na wana mnasaba na kungwi. Ndege hawa wana mgongo kwa rangi y ...

Kokoko

Kungwi ni ndege mbuai wa jenasi mbalimbali za nusufamilia Striginae katika familia Strigidae. Spishi fulani zinaitwa kokoko. Ndege hawa ni wakubwa kuliko bundi na spishi za jenasi Bubo ni miongoni mwa spishi kubwa kabisa za Strigidae. Kungwi wana ...

Kilio

Mititi au vilio ni ndege mbuai wa jenasi mbalimbali katika familia Strigidae. Kwa kawaida ndege hawa ni wadogo kuliko bundi na wana rangi ya kahawa au kijivu pamoja na madoadoa ambayo yanafanana na gome la miti. Kwa kawaida jike ni mkubwa kuliko ...

Firigogo

Firigogo ni ndege wa nyika wa jenasi Pterocles na Syrrhaptes katika familia Pteroclidae. Wataalamu wengine wanawaainisha katika jenasi moja Pterocles. Wanafanana kidogo na njiwa lakini ni wanono kuliko hao.

Hinabuluu

Hinabuluu ni ndege wa ardhi wa familia Pittidae. Ndege hawa ni wakubwa na wanene kiasi wenye miguu mirefu, mkia mfupi sana na domo lenye nguvu. Spishi nyingi zina rangi kali. Wanatokea ardhini kwa misitu minyevu ya tropiki ya Afrika, Asia na Aust ...

Domomundu

Domomundu, kwembemundu au hanjari ni ndege wa jenasi Rhinopomastus katika familia Phoeniculidae. Wanafanana na goregore lakini domo lao limepindika zaidi. Mwangani kwa jua manyoya yao yana mngao buluu wa metali. Hula wadudu ambao wanawatafuta kat ...

Kwembekwembe

Fimbi ni jina linalotumika kwa spishi ndogo za familia ya ndege Bucerotidae; spishi moja inaitwa kwembe au kwembekwembe pia. Spishi kubwa za familia hii zinaitwa hondohondo. Fimbi wana domo kubwa lakini lile halina aina ya pembe juu lake kama dom ...

Golegole

Goregore, gegemela au vinuka ni ndege wa jenasi Phoeniculus katika familia Phoeniculidae. Hawa ni ndege weusi wenye mkia mrefu na domo refu jekundu au jeusi lililopindika. Mwangani kwa jua manyoya yao yana mngao kijani au zambarau wa metali. Kuna ...

Hondo

Hondohondo ni ndege wakubwa wa familia Bucerotidae. Spishi ndogo zinaitwa fimbi kwa kawaida. Wana domo kubwa na lile la spishi nyingi lina aina ya pembe juu lake. Domo linaweza kuwa jeusi, jeupe, jekundu au njano. Ndege hawa hula matunda, wadudu ...

Mbizi wa nyika

Mumbi, hondo-ardhi au mbizi wa nyika ni ndege wa jenasi Bucorvus, jenasi pekee ya familia Bucorvidae. Wana mnasaba na hondohondo na hadi juzi waliainishwa katika familia Bucerotidae, lakini ndege hawa ni wakubwa sana na hukaa ardhini takriban saa ...

Dudumizi

Dudumizi ni ndege wakubwa kadiri wa jenasi Centropus, jenasi pekee ya nusufamilia Centropodinae katika familia Cuculidae. Wana macho mekundu na mkia mrefu, na ukucha wa kidole kikabilicho nyuma ni mrefu sana. Jina" Centropus” linatoka maneno ya K ...

Kekeo

Kekeo ni ndege wadogo hadi wakubwa kiasi wa nusufamilia Cuculinae katika familia Cuculidae. Wana mkia mrefu na mabawa marefu na membamba. Miguu yao ina vidole viwili vikabilivyo mbele na viwili vikabilivyo nyuma. Rangi zao kuu ni nyeusi, nyeupe n ...

Kua

Kua ni ndege wakubwa kiasi wa jenasi Coua katika nusufamilia Phaenicophaeinae ya familia Cuculidae. Pengine wanaainishwa katika nusufamilia yao Couinae pamoja na kekeo-ardhi wa Asia. Jenasi pekee ya Bara la Afrika inayoainishwa katika Phaenicopha ...

Malkoha

Malkoha ni ndege wakubwa kiasi wa nusufamilia Phaenicophaeinae katika familia Cuculidae. Spishi za malkoha zinazotokea Afrika zinaitwa ukiki na kua kwa Kiswahili. Lakini hivi karibuni wataalamu wengine wameainisha kua katika nusufamilia yao, Coui ...

Pundamakaa

Ukiki au pundamakaa ni ndege wakubwa kiasi wa jenasi Ceuthmochares katika nusufamilia Phaenicophaeinae ya familia Cuculidae wanaofanana na kekeo. Wana mnasaba na malkoha wa Asia. Wanatokea misitu wa Afrika kusini kwa Sahara. Rangi yao ni buluu au ...

Bandabanda

Vijogoo-shamba au bandabanda ni ndege wa familia Calyptomenidae. Zamani ndege hawa waliainishwa katika familia Eurylaimidae lakini siku hizi inabaki spishi moja tu ndani yake, kijogoo-shamba kijani. Wana domo pana na spishi za Asia pamoja na kijo ...

Fuluwili

Fuluwili ni ndege wa jenasi Canirallus na Sarothrura, jenasi pekee za familia Sarothruridae. Ndege hawa wanafanana na viluwiri lakini wana rangi kali zaidi. Wanafanana nao kwa mwenendo pia. Spishi zote zinatokea Afrika na Madagaska.

Kiguudau

Viguudau ni ndege wa maji wa familia Heliornithidae. Familia hii ina spishi tatu tu, kila moja katika jenasi yake. Ndege hawa wana mwili mwembamba, shingo ndefu, mkia mpana na domo lenye ncha kali. Wana tando za ngozi kati ya vidole vyao zinazowa ...

Bwenzi

Korongo hawa ni ndege wa familia ya Gruidae wenye domo fupi na jembamba kuliko lile la korongo wa familia ya Ciconiidae. Spishi nyingi hufanya mikogo ya kubembeleza jike wakitoa sauti kubwa. Huugana kwa maishi yao yote. Spishi za nchi za halijoto ...

Kukuziwa

Kukuziwa ni ndege wa jenasi mbalimbali katika familia Rallidae. Wana mnasaba na viluwiri lakini ni ndege wa maji wa kweli. Wanaachana na viluwiri kwa kuwa na kigao kidogo juu ya domo. Rangi yao ni nyeusi au kijivu nzitu na mabawa ya spishi nyingi ...

Kukutanda

Shaunge ni ndege wa jenasi Porphyrio katika familia ya Rallidae. Huitwa kukutanda pia. Wanafanana sana na kukuziwa lakini rangi yao ni buluu au zambarau. Wana kigao chekundu isipokuwa Porphyrio flavirostris, ambaye ana kigao njano, na P. martinic ...

Chechele (Stenostiridae)

Chechele ni ndege wa familia Monarchidae na Stenostiridae. Zamani wale wa Stenostiridae waliainishwa katika familia Muscicapidae, Monarchidae, Sylviidae na Rhipiduridae, lakini uchunguzi wa ADN umeonyesha kwamba wana mnasaba na kwa hivyo wamepewa ...

Domofupi

Domofupi ni ndege wa familia Paridae. Hawa ni ndege wadogo wenye domo fupi na mkia mfupi; spishi kadhaa zina kishungi. Rangi zao si kali sana: kwa kawaida nyeusi, nyeupe, kijivu na/au kahawia, pengine buluu, njano na nyekundu. Wanatokea Afrika, A ...

Domosharubu

Domosharubu ni ndege wadogo wa jenasi Bleda katika familia Pycnonotidae. Wanafanana na korogoto na wana rangi ya kahawa au zaituni juu na njano chini. Wanaitwa domosharubu kwa sababu wana nywele ndefu msingini kwa domo. Ndege hawa wanatokea misit ...

Jeri

Jeri ni ndege wadogo wa jenasi Neomixis katika familia Cisticolidae. Wanafanana na videnenda lakini hawana michirizi mizito. Ndege hawa wana rangi ya kahawa au zaituni mgongoni na nyeupe au kijivu chini na pengine njano pia. Wanatokea misitu ya M ...

Kabumbu

Kabumbu ni ndege wadogo wa familia Remizidae. Wanafanana na domofupi lakini domo lao ni jembamba zaidi lenye ncha kali zaidi. Mabawa yao ni mafupi na yameviringa, na mkia una mkato wa V mwishoni. Wana rangi ya kijivu pamoja na njano na nyeupe na ...

Damisi

Kanghagha au zogoyogo ni ndege wa familia Leiotrichidae. Wanafanana na mikesha wa familia Turdidae. Wanatokea misitu na maeneo mengine yenye miti katika Afrika na Asia. Spishi za Afrika zina rangi za kahawa, nyeusi, kijivu na nyeupe, lakini spish ...

Kibwirosagi

Vibwirosagi ni ndege wadogo wa jenasi mbalimbali katika familia Cisticolidae. Wanafanana na videnenda lakini mkia wao ni mrefu zaidi na wana rangi kali zaidi: nyekundu, kijani, kahawia na/au kijivu mgongoni na njano, nyekundu, marungi, hudhurungi ...

Kidenenda

Videnenda ni ndege wadogo wa jenasi Cisticola na Incana katika familia Cisticolidae. Chimbuko la jenasi lipo Afrika lakini spishi kadhaa zinatokea Ulaya na Asia pia, spishi moja hata mpaka Australia. Ndege hawa hupatikana kwa maeneo wazi, k.m. sa ...

Kibubutu

Vikucha au vibubutu ni ndege wadogo ambao zamani waliainishwa katika Sylviidae, familia ya kucha wengine. Sasa wataalamu wanakubaliana kwamba labda ndege hawa ni kundi lao lenyewe pamoja na kolojojo na spishi nyingine za kucha wa Afrika. Kwa sasa ...