ⓘ Free online encyclopedia. Did you know? page 18

Sukarno

Sukarno alikuwa mwanasiasa wa Indonesia ambaye alikuwa rais wa kwanza wa Indonesia, akihudumu kutoka mwaka 1945 hadi 1967.

Sun Yat-sen

Sun Yat-sen alikuwa kiongozi wa kisiasa nchini China aliyeshiriki katika mapinduzi ya China ya 1911 yaliyoondoa utawala wa kifalme nchini akawa rais wa kwanza wa Jamhuri ya China na mwanzilishi wa chama cha Kuomintang.

Sylvanus Olympio

Sylvanus Olympio Epiphanio alikuwa mwanasiasa wa Togo ambaye aliwahi kuwa Waziri Mkuu, na kisha Rais wa nchi na 1958 hadi alipouawa mwaka 1963. Yeye alitoka Familia muhimu ya Olympio, ambayo ilimjumuisha mjomba wake Octaviano Olympio, mmoja wa wa ...

Margaret Thatcher

Margaret Hilda Thatcher alikuwa waziri mkuu wa Uingereza kuanzia 1979 hadi 1990 na mwanamke wa kwanza aliyeshika cheo hiki. Alichaguliwa kama mgombea na kiongozi wa chama cha Conservative Party. Aliendesha mabadiliko mengi ya kiuchumi na kisiasa. ...

Thomas Seymour

Thomas Seymour alikuwa ndugu wa malkia wa Uingereza, Jane Seymour ambaye alikuwa mke wa tatu wa Mfalme Henry VIII na mama wa Edward VI. Pia alikuwa mume wa nne wa Catherine Parr ambaye alikuwa mke wa sita na wa mwisho wa Henry VIII. Hata hivyo, l ...

Timur

Timur alikuwa kiongozi Mwislamu wa Waturuki na Wamongolia wa Asia ya Kati wakati wa karne ya 14 aliyeanzisha milki ya Watimuri. Jina lake kamili Lilikuwa Timur bin Taraghay Barlas kutokana na neno la Kichagatai تیمور "chuma". Alijulikana pia kama ...

Tito Okello

Tito Lutwa Okello alikuwa afisa wa jeshi la Uganda na mwanasiasa pia; alipata kuwa Rais wa Uganda kuanzia tarehe 29 Julai 1985 hadi tarehe 26 Januari 1986.

Toussaint Louverture

Toussaint Louverture alikuwa askari na mwanasiasa nchini Haiti. Alikuwa kiongozi wa Mapinduzi ya Haiti na mkombozi nchini Haiti. Ni shujaa wake mkuu hadi sasa. Aliongoza Haiti kupata Uhuru mwaka 1804 ijapo Wafaransa walimwua kabla ya Uhuru.

Volodymyr Zelensky

Volodymyr Oleksandrovych Zelensky ni mwanasiasa, mwandishi wa filamu, mwigizaji wa filamu, mchekeshaji na rais wa sasa wa Ukraine toka 20 Mei 2019. Kabla ya kujihusisha na siasa, alipata shahada ya sheria na baadaye akaanzisha kampuni ya filamu, ...

Boris Yeltsin

Boris Nikolayevich Yeltsin alikuwa rais wa kwanza wa Urusi baada ya mwisho wa ukomunisti. Alitumikia taifa la Urusi kuanzia mwaka 1991 hadi 1999. Mikhail Gorbachev, alimtangulia Boris, wakati huo Urusi iliitwa Umoja wa Kisovyeti. Vladimir Putin a ...

Yun Chi-ho

Yun Chi-ho alikuwa mwanasiasa na mwanaharakati wa Korea. Mjomba wa Yun Bo-seon, rais wa nne wa Korea Kusini, alikuwa kiongozi wa klabu 독립협회 獨立協會 ya kujitegemea Habari 독립신문 獨立新聞 na mwandishi wa nyimbo za Aegukga대한민국애국가 大韓 ...

Yun Hyon-seok

Yun Hyon-seok alikuwa mwanaharakati wa haki za binadamu, mshairi na mwandishi wa nchi ya Korea Kusini. Alikuwa na jina la utani Yukwudang 육우당 六友堂, Marafiki sita nyumbani, Sulheon 설헌 雪軒, Midong 미동 美童, uzuri kijana. Alizaliwa mjini By ...

Yuri Andropov

Yuri Vladimirovich Andropov alikuwa kiongozi wa sita wa Umoja wa Sovyeti na Katibu Mkuu wa nne wa Chama cha Kikomunisti cha Umoja wa Kisovyeti. Kufuatia utawala wa miaka 18 ya Leonid Brezhnev, Andropov alihudumu katika wadhifa huo kutoka Novemba ...

Kurt Georg Kiesinger

Kurt Georg Kiesinger alikuwa mwanasiasa kutoka nchini Ujerumani. Kiesinger alizaliwa Ujerumani ya Kusini. Alisomea masuala ya historia mjini Tübingen na baadaye sheria mjini Berlin. Alijiunga na Chama cha Nazi mnamo mwaka 1933, na kufanyakazi kat ...

Petro Claver

Petro Claver, S.J. alikuwa padri Mjesuiti mmisionari huko Amerika Kusini. Kutokana na maisha yake aliyoyatoa kwa nadhiri ya kujifanya mtumwa wa watumwa, anaheshimiwa kama mtakatifu msimamizi wa misheni zote za Kanisa Katoliki kwa watu wenye asili ...

Gorée

Gorée ni kisiwa cha Atlantiki mbele ya pwani ya Senegal na sehemu ya manisipaa ya Dakar. Ilijulikana kama kituo cha biashara ya watumwa. Hadi kukomeshwa kwa biashara hiyo mwaka 1848 watumwa walipelekwa kisiwani kutoka bara, kufungwa katika jela, ...

Kanisa la Kristo, Zanzibar

Kanisa la Kristo ni kanisa kuu la Anglikana mjini Zanzibar lililo kati ya vivutio vya kihistoria vya mji huo. Liko Mkunazini Road, katikati ya Mji Mkongwe. Usanifu majengo uliotumika ni kati ya vielelezo vya kwanza vya Usanifu majengo wa Kikristo ...

Suema Akumboke

Suema alizaliwa sehemu za ziwa Nyasa. Huko alikamatwa na Waarabu, lakini mama yake hakutaka kuachana naye. Hivyo wote wawili waliingizwa katika msafara wa kupelekwa Unguja na kuuzwa sokoni. Kutokana na urefu na ugumu wa safari mama yake alidhoofi ...

Wabusinenge

Wabusinenge, Maroon) ni neno katika kikreoli cha Surinam kwa ajili ya wakazi wenye asili ya Kiafrika ambao mababu yao walipelekwa Surinam kama watumwa lakini walikimbia na kuanza maisha huru porini mbali na mashamba ya mabawana wa zamani. Kuanzia ...

Zanj

Zanj ni neno lililotumiwa na waandishi Waislamu wa zamani kutaja watu weusi kutoka Afrika ya Mashariki na pia kwa maana ya kijiografia kutaja eneo la Afrika ya Mashariki.

Uchaguzi Mkuu wa Kenya, 1997

Kulikuwa na wagombezi watano muhimu wa urais katika uchaguzi huu, huklu mmoja akiwa mwanamke wa kwanza kugomba urais nchini Kenya: Charity Ngilu Miongoni mwa wengine Mwai Kibaki Michael Wamalwa Kijana Raila Amollo Odinga Daniel Arap Moi

Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, 2005

Nchi ya Tanzania ilifanya uchaguzi wa urais na ubunge mnamo 4 Desemba 2005. Mapema ulikuwa ulipangiwa kufanyika mnamo 30 Oktoba lakini ukahairishwa kutokana na kifo cha mgombea kiti cha Makamu wa Rais. Uchaguzi huu ulikuwa wa tatu tangu nchi hiyo ...

Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, 2015

Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, 2015 ulifanyika tarehe 25 Oktoba. Wapiga kura walimchagua Rais, wabunge na Madiwani. Tarehe 29 Oktoba mgombea wa CCM, John Pombe Magufuli alitangazwa na Tume ya Uchaguzi kuwa mshindi wa kura ya rais, akifuatwa na Lowass ...

Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, 2020

Kufuatana na tangazo la Tume la Uchaguzi la 30 Oktoba matokeo yalikuwa kama yafuatayo: Wapiga kura walioandikishwa walikuwa 29.754.699. Waliopiga kura walikuwa 15.091.950 % 50.72, wasiopiga kura walikuwa 14.662.749 % 49.28. Jumla ya kura zilizopi ...

Mkataba wa Helgoland-Zanzibar

Mapatano baina Uingereza na Ujerumani kuhusu Afrika na Helgoland yalifanywa kati ya Ujerumani na Uingereza tarehe 1 Julai 1890. Pande zote mbili zilielewana juu ya mipaka ya makoloni yao au maeneo walimotaka kuwa na athira kuu katika Afrika. Mkat ...

Koloni ya Rasi

Koloni ya Rasi ilikuwa koloni ya Uholanzi hadi 1806 na baadaye ya Uingereza katika Afrika Kusini ya leo. Jina limetokana na Rasi ya Tumaini Jema iliyoko karibu na mji wa Cape Town.

Rhodesia ya Kusini

Koloni liliundwa na Cecil Rhodes aliyetwaa eneo hili pamoja na "Rhodesia ya Kaskazini" au Zambia na kuliweka chini ya Kampuni ya Kiingereza ya Afrika Kusini British South Africa Company. Rhodes aliwahi kujaribu kupata mapatano na mfalme Lobengula ...

Afrika ya Kusini-Magharibi ya Kijerumani

Afrika ya Kusini-Magharibi ya Kijerumani ilikuwa koloni la Ujerumani katika Afrika kuanzia mwaka 1884 hadi 1915. Leo hii ni nchi ya Namibia. Tangu mwaka 1891 Windhuk ilikuwa mji mkuu wa koloni. Sawa na Namibia ya leo, koloni lilikuwa na eneo la k ...

Helgoland

Helgoland ni fungukisiwa ndogo cha Kijerumani katika Bahari ya Kaskazini takriban 70 km mbele ya Ujerumani bara. Ina visiwa viwili: Helgoland yenyewe ni kisiwa kinachokaliwa na watu halafu kisiwa kisicho na watu cha "Düne". Kisiwa kikuu kina uref ...

Kamusi ya Koloni za Kijerumani (1920)

Deutsches Kolonial-Lexikon ni jina la Kijerumani la "Kamusi ya Kikoloni ya Kijerumani" iliyotolewa mwaka 1920. Kamusi hiyo ilikusanya habari juu ya koloni zote za Ujerumani kabla ya 1914. Kamusi imepita kipindi cha hakimiliki ikawekwa mtandaoni k ...

Kishoroba cha Caprivi

Kishoroba cha Caprivi ni kanda nyembamba ya eneo la Namibia inayoelekea mashariki kwenye pembe la kaskazini-mashariki kabisa ya nchi Namibia kati ya Botswana upande wa kusini na Angola pamoja na Zambia upande wa kaskazini. Kishoroba kina urefu ta ...

Togo ya Kiingereza

Togo ya Kiingereza ilikuwa eneo lililokabidhiwa mkononi wa Uingereza baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Mwaka 1914 Uingereza na Ufaransa walipatana kuvamia Togo ya Kijerumani na kugawana eneo lake. Theluthi ya magharibi ya koloni ya Kijerumani ...

Togo ya Kijerumani

Wafanyabiashara Wajerumani kutoka Hamburg na Bremen waliwahi kuwa na ofisi zao hasa huko Aneho kuanzia miaka ya 1870 BK. 1882 kampuni ya Woermann ilianzisha usafiri kwa meli kati ya Hamburg na Afrika na kufanya Togo kituo kimoja. Wakati ule pwani ...

Witu

Witu ni mji mdogo na tarafa katika kaunti ya Lamu nchini Kenya. Iko barabarani kutoka Malindi kwenda Lamu, takriban katikati ya mto Tana na Lamu. Katika karne ya 19 ilikuwa mji mkuu wa Usultani wa Witu. Kwa muda mfupi, kati ya mwaka 1885 hadi 189 ...

Julian Huxley

Sir Julian Sorell Huxley alikuwa mwanabiolojia na mwandishi kutoka nchi ya Uingereza. Anajulikana hasa kwa maandishi yake ya kisayansi aliyojaribu kuyafanya yaeleweke na watu wengi wa kawaida. Pia alikuwa mkurugenzi wa kwanza wa UNESCO. Alipewa c ...

Democratic Party (Kenya)

Democratic Party au Chama cha Demokrasia ni chama cha kisiasa nchini Kenya. Kilianzishwa 1991 na Mwai Kibaki baada ya kuondoka kwake katika chama tawala cha KANU. Chama kilikuwa na athira na uwezo hasa katika maeneo ya Wakikuyu. Kiliteua Kibaki k ...

FORD-Asili

FORD-Asili ni chama cha kisisasa nchini Kenya. Jina ni kifupi cha Forum for the Restauration of Democracy-Asili. FORD-Asili ilianzishwa 1992 baada ya farakano ya harakati ya FORD ya pamoja.

FORD-Kenya

FORD-Kenya ni chama cha kisisasa nchini Kenya. Jina ni kifupi cha Forum for the Restauration of Democracy-Kenya. FORD-Kenya ilianzishwa 1992 baada ya farakano ya harakati ya FORD ya pamoja.

FORD-People

FORD-People ni chama cha kisiasa nchini Kenya. Kwa Kiingereza ni Forum for the Restoration of Democracy for the People. Chama hiki ilianzishwa mwaka wa 1997 baada ya farakano la chama cha FORD-Asili.

Forum for the Restauration of Democracy

Ilianzishwa mwaka 1991 na wanasiasa waliopinga mfumo wa chama kimoja na utawala wa KANU chini ya rais Daniel arap Moi. Shabaha ilikuwa mabadiliko ya kuruhusu vyama vingi na uhuru wa kidemokrasia. Wakati ule chama cha pekee kilichoruhusiwa kilikuw ...

Kenya African National Union

Kenya African National Union au KANU ni chama cha kisiasa nchini Kenya. KANU ilikuwa chama tawala cha nchi tangu uhuru katika mwaka 1963 hadi kushindwa katika uchaguzi wa 2002.

LDP (Kenya)

Liberal Democratic Party ni chama cha kisiasa nchini Kenya. Ilikuwa na wabunge 59 baada ya uchaguzi wa Kenya wa 2002 ikiwa sehemu ya NARC yaani maungano ya kisiasa tawala katika Kenya baada ya 2002. Haikugombea bunge kwa jina lake katika uchaguzi ...

NARC-Kenya

National Rainbow Coalition–Kenya ni chama cha kisiasa nchini Kenya. Kilianzishwa kama farakano katika NARC asilia baada ya kura maalumu juu ya katiba ya Kenya 2005. NARC-Kenya ilipangwa kuwa chama kipya cha kumrudisha Mwai Kibaki kama rais wa Ken ...

National Alliance Party of Kenya

National Alliance Party of Kenya ilikuwa maungano ya vyama vya kisiasa nchini Kenya yaliyoanzishwa kabla ya uchaguzi wa rais na bunge wa mwaka 2002. Kusidi lake lilikuwa kuunganisha vikundi vyote vilipinga utawala wa rais Daniel arap Moi na chama ...

National Development Party of Kenya

National Development Party ilikuwa chama cha kisiasa nchini Kenya. Ilikuwa maarufu kama chama cha Waluo hasa tangu 1994 hadi kuungana na KANU mwaka 2001.

National Rainbow Coalition

Ilikuwa muungano wa vyama mbalimbali vya upinzani dhidi ya KANU na rais Daniel arap Moi. Ilikuwa hasa na pande mbili: Chama cha LDP kilichounganisha wanasiasa walioondoka katika KANU baada ya Uhuru Kenyatta kutangaziwa kuwa mgombea wa urais. Kati ...

Orange Democratic Movement

Orange Democratic Movement na Kalonzo Musyoka ODM-Kenya. Sababu ya farakano ilikuwa suala la nani atakuwa mgombea wa urais upande wa ODM.

Chama cha Mapinduzi

CCM ilizaliwa tarehe 5 Februari 1977 baada ya kuungana kwa vyama vya Tanganyika African National Union TANU kilichokuwa kikitawala Tanzania Bara na Afro-Shirazi Party ASP kilichokuwa chama tawala cha Zanzibar wakati huo. Chama cha TANU kilikuwa k ...

Frances Ames

Frances Rix Ames alikuwa bingwa wa nyuroni, daktari wa magonjwa ya akili, na mpiganaji wa haki za binadamu nchini Afrika Kusini. Amefahamika kwa ubora wake katika kuongoza uchunguzi wa kifo cha mwanaharakati Steve Biko aliyepinga ubaguzi wa rangi ...

Vasil Levski

Vasil Levski alikuwa mwanaharakati na ni shujaa wa kitaifa wa Bulgaria. Levski alitengeneza harakati ya mapinduzi ya kuifungua Bulgaria kutoka Utawala wa Ottoman. Alianzisha Shirika la Mapinduzi ya Ndani, akijaribu kuhamasisha uasi wa taifa kupit ...