ⓘ Free online encyclopedia. Did you know? page 20

Kinu cha Warangi

Kinu cha Warangi ni aina ya chombo ambacho hutengenezwa kwa mti. Kwa Kirangi huitwa "kʉnyu". Kinu hutumika kwa kutwangia nafaka ili kuondoa makapi, maganda na kadhalika.

Kipekecho cha Warangi

Kipekecho cha Warangi kilichongwa kutokana na mti. Kwa Kirangi huitwa "lʉfire". Hutumika kwa kupekechea uji, ugali, au maziwa yaliyoganda. Kipekecho cha asili kilikuwa na masikio matatu.

Kirindo cha Warangi

Kirindo cha Warangi ni aina ya ghala ya nafaka. Kwa Kirangi huitwa "kɨome". Chombo hicho kilikuwa hutengenezwa na magome ya miti, na kilitumika hasa kuhifadhi nafaka na mazao mengineyo.

Kisu cha Warangi

Kisu cha Warangi ni kifaa cha chuma. Kwa Kirangi huitwa "lʉfyo" kwa jumla, au kama ni maalum, huitwa" nyaasʉka”. Kisu cha Warangi kilikuwa na makali pande mbili. Fimbo au mkono wake ulikuwa wa pembe ya tembo au ng’ombe. Kilitumika kwa kukatia, ku ...

Ngoma ya Warangi

Ngoma ya Warangi ni aina ya ngoma iliyowambwa ngozi ya mnyama wa porini hasa dikidiki. Kwa Kirangi huitwa "ntangasa". Ngoma hiyo hutumika wakati wa sherehe kama harusi na kadhalika.

Sagio la Warangi

Sagio la Warangi ni aina ya kifaa kilichotengezwa kutokana na mawe. Kwa Kirangi huitwa "lwaala". Sagio lilitumika kwa kusagia nafaka ili kupata unga. Sagio la asili lilikuwa la mviringo.

Sanduku la Warangi

Sanduku la Warangi ni aina ya kibuyu kikubwa kilichokatwa mdomo mkubwa. Kwa Kirangi huitwa "iduunde". Kibuyu hicho kilitumika kwa kuwekea dawa hasa zilizotumika wakati wa kutengeneza vyuma na kadhalika. Pia liliwekea vifaa vidogovidogo vya nyumba ...

Shikilio la Warangi

Shikilio la Warangi ni mti uliokaa panda. Kwa Kirangi huitwa "ntambarɨko". Mti huo ulitumika kwa kubana chungu wakati wa kupika chakula. Suruali zilipoingia Urangini Warangi waliziita pia" ntambarɨko”, yaani nguo iliyokaa panda. Ilikuwa mwiko kum ...

Shoka la Warangi

Shoka la Warangi ni aina ya kifaa ambacho hutengenezwa kwa chuma na mpini wa mti. Kwa Kirangi huitwa "chaárya" kwa jumla, na" siraanga” kama ni maalum. Shoka hili hutumika kwa kuangushia miti, kuchanja kuni, kupasulia magogo au kuchongea mizinga.

Tungu la Warangi

Tungu la Warangi ni aina ya kibuyu cha wastani. Kilitumika kwa kuchekechea maziwa yaliyoganda ili kutenganisha maziwa na mafuta ya samli. Kilichaguliwa kibuyu kizuri kisicho na alama yoyote. Kwa Kirangi huitwa "baai".

Upawa wa Warangi

Upawa wa Warangi ni aina ya chombo cha kuchotea. Kwa Kirangi huitwa "ndʉvo". Chombo hicho kilitokana na aina fulani ya maboga au mamumunya. Hutumika kwa kuchotea pombe kutoka katika mtungi.

Bikari

Kwa kundinyota angalia Bikari Bikari ing.: pair of compasses ni zana ya kazi kwa wachoraji na wanahisabati kwa kuchora duara. Pamoja na ramani inasaidia pia kupima umbali kwa hiyo ni pia zana ya ubaharia. Bikari hutengenezwa kwa metali fulani au ...

Kisu

Kisu ni kifaa cha kukata chenye bapa ambalo ni kali angalau upande moja. Kwa kawaida kuna sehemu mbili: bapa kali na shikilio. Siku hizi bapa imetengenezwa kwa metali na shikilio la ubao au plastiki.

Kinyunyizo

Kinyuyizo ni chombo cha umwagiliaji mimea, ama kwenye shamba la kilimo au katika bustani. Matumizi mengine ni kwa ajili ya kupoza joto au kwa kupambana na vumbi nyingi. Majengo ya ofisi au viwanda mara nyingi huwa pia na mfumo wa vinyuyizo kwenye ...

Mundu

Mundu ni kifaa kinachotumiwa katika kilimo kwa kukata nyasi na mavuno ya nafaka na mazao mengine. Mundu kama zana ya kilimo inajulikana tangu zama za mawe. Katika nchi nyingi za dunia haitumiwi tena sana kwa sababu nafasi yake imechukuliwa na mas ...

Airkenya

Airkenya Express ni aina ya ndege iliyo na makao mjini Nairobi, Kenya. Airkenya husafirisha watu kote nchini Kenya na hata pia hadi Tanzania. Makao yake makuu ni katika Uwanja wa ndege wa Wilson, Nairobi.

Ajali ya Helikopta ya Polisi 2012, Kenya

Ajali ya Helikopta ya Polisi 2012 nchini Kenya ilihusisha ndege iliyoanguka ya aina ya helikopta iliyomilikiwa na polisi ya Kenya mnamo 10 Juni, 2012. AS350 Eurocopter ilianguka katika eneo la Ngong, na kuua abiria wote sita na wafanyakazi waliok ...

Bandari ya Kilindini

Bandari ya Kilindini ni hori kubwa asili ya maji yenye urefu kwenda chini unaoendelea barani kutoka Mombasa, Kenya. Inatumika kama bandari ya Mombasa, na inayo uendelezaji mikoani hadi Uganda na Sudan. Bandari ya Kilindini ni sehemu kuu ya Bandar ...

East African Railways and Harbours Corporation

Shirika la reli na bandari za Afrika ya Mashariki) ilikuwa kampuni ya umma iliyosimamia reli na bandari za Kenya, Uganda na Tanganyika na baadaye Tanzania katika miaka kabla na baada ya uhuru wa nchi hizi.

Kampuni ya Kenya Pipeline

Kampuni ya Kenya Pipeline ni kampuni ya serikali yenye jukumu la kusafirisha,kuhifadhi na kuwasilisha bidhaa za aina ya mafuta kwa wateja nchini Kenya ikitumia mfumo wake unaohusisha nchi nzima. Kampuni hii hushirikiana na Shirika la Taifa la Maf ...

Matatu

Matatu ni neno la kawaida nchini Kenya na Uganda la kutaja gari aina ya daladala linalotumika kama usafiri wa umma. Jina "matatu" labda lilitokana na nauli ya sarafu tatu iliyokuwa kawaida kwa safari moja matatu yalipoanza. Matatu huhudumia njia ...

Reli ya SGR ya Kenya

Reli ya SGR ya Kenya ni mfumo mpya wa reli nchini Kenya kati ya miji wa Mombasa na Nairobi unaotumia geji sanifu. Reli hiyo ni mradi mkubwa wa miundombinu tangu uhuru mwaka 1963. Ilijengwa na kampuni ya China Road and Bridge Corporation kwa kutum ...

Safari 431 ya Kenya Airways

Kenya Airways Flight 431 ilikuwa safari ya ndege ya aina ya Airbus A310-300 ambayo ilikuwa imepangwa kimataifa katikati ya Abidjan-Lagos na Nairobi. Ndege hii ilianguka kwenye bahari karibu na pwani ya Ivory Coast, tarehe 30 Januari 2000, saa 21: ...

Barabara nchini Tanzania

Barabara nchini Tanzania ni mtandao wa barabara wenye urefu wa kilomita 91.532, ambazo kati yake kilomita 12.197 zimeainishwa kama barabara kuu na kilomita 21.298 kama barabara za kimkoa na aina hizo za barabara husimamiwa na mamlaka ya TANROADS ...

Liemba (meli)

MV Liemba ni meli ya Kitanzania inayohudumia pwani za Ziwa Tanganyika. Ni chombo cha usafiri kwa maji chenye umri mkubwa kipo tangu mwaka 1914. Meli inasukumwa na injini ya diseli na urefu wake ni mita 67, upana mita 10 na ukubwa unatajwa ama kuw ...

Mamlaka ya Bandari Tanzania

Mamlaka ya Bandari Tanzania ni shirika la umma linalofanya kazi zake chini ya Wizara ya Miundombinu na Maendeleo, hiyo ndiyo inajukumu zima la kuongoza na kuendesha bandari ya bahari na bandari ya maziwa ya nchini Tanzania. Mamlaka haya yapo mjin ...

Reli ya SGR Tanzania

Reli ya SGR Tanzania au Reli ya geji sanifu ya Tanzania ni mradi wa kuunganisha Tanzania na nchi jirani kwa njia ya reli ya geji sanifu. Njia ya geji sanifu inalenga kufika Rwanda na Uganda, na kupitia nchi hizi mbili, hadi Burundi na Jamhuri ya ...

Reli ya Tanganyika

Reli ya Tanganyika ilikuwa jina la njia ya reli kuanzia Dar es Salaam kwenda Kigoma kwenye Ziwa la Tanganyika iliyojengwa katika miaka 1905 hadi 1914 zamani za koloni la Afrika ya Mashariki ya Kijerumani.

Shirika la Reli Tanzania

Shirika la Reli Tanzania au Tanzania Railways Limited ni kampuni ya umma inayoendesha usafiri kwenye mtandao mkubwa zaidi wa reli nchini Tanzania. Inaendesha hasa usafiri kwenye njia za reli zifuatazo katika Tanzania Reli ya kati kuanzia Daressal ...

TAZARA

TAZARA ni shirika ya reli ya pamoja ya nchi za Zambia na Tanzania. Inaunganisha bandari ya Dar es Salaam nchini Tanzania na kituo cha New Kapiri Mposhi iliyopo kwenye njia ya reli kati ya Lusaka na Kitwe kwenye ukanda wa shaba wa Zambia.

Reli ya Kenya-Uganda

Makala hii yaeleza habari za njia ya reli ya kihistoria kati ya Mombasa na Uganda. Kwa habari za Shirika ya Reli ya Uganda ya kisasa tazama Uganda Railways Corporation. Reli ya Kenya-Uganda ni jina kwa reli kati ya Mombasa na Kampala iliyojengwa ...

Bamboo Airways

Bamboo Airways ni kampuni ya ndege ya taifa ya Vietnam yenye makao makuu jijini Hanoi. Kampuni hii ilianza kufanya kazi zake mwaka 1996 baada ya kuvunjika kwa Cong ty Hang khong Tre Viet kulikopelekea kuvunjika kwa "hang khong Tre Viet". Hivi sas ...

Uwanja wa Ndege wa Dong Hoi

Kiwanja cha Ndege cha Dong Hoi ni kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Dong Hoi nchini Vietnam. Jina kamili kwa Kivietnam ni Sân bay Dồng Hới au kwa Kiingereza Cảng hàng không Dồng Hới. Inahudumiwa na Vietnam Airlines. Ilianzishwa kama kiwanja cha ...

Apollo 11

Apollo 11 ilikuwa chombo cha angani cha kwanza kufikisha watu kwenye Mwezi. Hii yote ilifanywa na NASA. Kilirushwa angani mnamo 16 Julai 1969 kikibeba wanaanga watatu Neil Armstrong, Buzz Aldrin na Michael Collins.

Perseverance (Mirihi)

Perseverance ni jina la gari la upelelezi lililopelekwa kwenye sayari ya Mirihi kwenye Februari 2021. Kusudi lake ni kuzunguka katika kasoko ya Jezero na kukusanya data zake. Ilirushwa na mamlaka ya anga-nje ya Marekani NASA. Ilifika kwenye uso w ...

Chomboanga

Chomboanga ni chombo cha usafiri chochote kinachoruka juu ya ardhi katika angahewa ya dunia yetu. Vyombo vinvyopita kimo cha kilomita 100 juu ya ardhi huhesabiwa kati ya vyombo vya angani la nje. Vyomboanga hupatikana kwa namna mbili:

Kepler (chomboanga)

Kepler ni darubini ya anga-nje iliyorushwa angani na taasisi ya NASA kwa shabaha ya kugundua sayari za nje zinazozunguka nyota nje ya mfumo wa Jua letu. Jina lilichaguliwa kwa heshima ya mwanaastronomia Mjerumani wa karne ya 17 Johannes Kepler, K ...

Ndegeputo

Ndegeputo ni chomboanga kinachoelea kwa nguvu elezi ya gesi iliyoko ndani ya ganda lake. Chini ya chumba cha gesi inabeba behewa ya abiria na mizigo. Inasukumwa na injini za parapela. Kimsingi kuna aina mbili za ndegeputo:

Puto

Puto ni chombo cha usafiri anagani inatumia nguvu elezi ya gesi nyepesi kwa kubeba abiria na mizigo juu hewani. Inatembea kwa kusukumwa na upepo na njia ya pekee ya kuiongoza ni kuipandisha au kushusha. Ni tofauti na ndegeputo yenye injini inayow ...

Daraja la Umoja

Daraja la Umoja ni daraja la kuvukia mto Ruvuma linalojengwa kwa shabaha ya kuunganisha nchi mbili za Tanzania na Msumbiji. Mahali pa daraja ni takriban km 240 kutoka mdomo wa mto Ruvuma kati ya mkoa wa Mtwara, wilaya ya Nanyumbu na mkoa wa Cabo ...

Daraja la Kimataifa la Rusumo

Daraja la kwanza ni feleji lenye urefu wa mita 64 lililotengenezwa huko Torino nchini Italia kuanzia mwaka 1966, kusafirishwa hadi Tanzania na kuunganishwa mahali pake mwaka 1972. Tarehe 28 Aprili 1994, wakati wa mauaji ya kimbari ya Rwanda, zaid ...

Daraja la Rusumo

Daraja la kwanza ni feleji lenye urefu wa mita 64 lililotengenezwa huko Torino nchini Italia kuanzia mwaka 1966, kusafirishwa hadi Tanzania na kuunganishwa mahali pake mwaka 1972. Tarehe 28 Aprili 1994, wakati wa mauaji ya kimbari ya Rwanda, zaid ...

Daraja la Julius Nyerere

Daraja la Kigamboni ni daraja ambalo linavuka mkondo wa Kurasini jijini Dar es Salaam nchini Tanzania. Daraja hilo lina urefu wa mita 680, upana wa mita 32 na njia sita za kupitisha magari. Ndilo daraja kubwa katika Afrika ya Mashariki. Lilizindu ...

Daraja la Mkapa

Daraja la Mkapa ni daraja lenye urefu wa mita 970 linalovuka mto Rufiji nchini Tanzania. Liko katika Mkoa wa Pwani ya Ikwiriri na Nyamwage. Linapitiwa na barabara ya B2. Daraja lilifunguliwa rasmi na rais Benjamin Mkapa kwenye tarehe 2 Agosti 200 ...

Daraja la Selander

Daraja la Selander ni daraja kwenye Barabara ya Ali Hassan Mwinyi ambalo linavuka mto Msimbazi jijini Dar es Salaam, Tanzania. Daraja hili lilitengenezwa mwaka 1929 likapewa jina kwa kumbukumbu ya John Einar Selander aliyekuwa mkurugenzi wa kwanz ...

Chelezo

Chelezo ni chombo sahili cha usafiri kwenye maji. Kinafanywa na vitu vinavyoweza kuelea juu ya maji vinavyofungwa pamoja ili kuwa na uso bapa ambako watu wanaweza kukaa na kusafiri kwenye maji.

Kituo cha reli

Kituo cha reli ni mahali ambako abiria wanaweza kuingia na kutoka kwenye treni, na ambako mizigo inaweza kupakiwa au kutolewa. Mara nyingi kituo cha reli huwa na angalau jukwaa moja la kupandia kwenye treni na jengo ambako tiketi zinauzwa pamoja ...

Ibn Battuta

Abu Abdullah Muhammad Ibn Battuta alikuwa mpelelezi na mtaalamu Mwarabu wa karne ya 14. Kwa usafiri mgumu wa siku zile alitembelea nchi mbalimbali na kuvuka umbali mkubwa kushinda mtu yeyote wa siku zile anayejulikana. Kutoka kwake tunayo taarifa ...

Oskar Baumann

Oskar Baumann alikuwa mwanajiografia na mchunguzi wa Afrika kutoka Austria. Anakumbukwa kwa ramani na vitabu ambako alieleza kwa umakini maeneo mbalimbali ya Afrika, hasa katika Tanzania na Rwanda ya leo, aliyowahi kupita kwenye safari zake pamoja.

Alexander von Humboldt

Friedrich Wilhelm Heinrich Alexander Freiherr von Humboldt alikuwa mpelelezi na mwanasayansi kutoka Prussia katika Ujerumani. Alexander alifanya utafiti muhimu katika jiografia na biolojia.