ⓘ Free online encyclopedia. Did you know? page 27

Abba Sehma

Abba Sehma alikuwa mmonaki aliyefanya umisionari katika Ethiopia ya leo akaanzisha monasteri chini ya kanuni ya Pakomi huko Sedenya. Ni kati ya kundi la Watakatifu Tisa wa Kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia wanaosemekana kukimbilia nchi hiyo kuto ...

Abba Yamata

Abba Yamata alikuwa mmonaki aliyefanya umisionari katika Ethiopia ya leo akaanzisha monasteri chini ya kanuni ya Pakomi huko Garalta. Ni kati ya kundi la Watakatifu Tisa wa Kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia wanaosemekana kukimbilia nchi hiyo kut ...

Abrahamu mkaapweke

Abrahamu mkaapweke alikuwa mmonaki wa Mesopotamia katika karne ya 4 BK aliyetumwa kama padri mmisionari huko Beth-Kiduna; ndiyo sababu anaitwa Kidunaia. Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu, hasa tarehe 29 Oktoba.

Alois Beaulieu

Alois Beaulieu, M.E.P. ni mmojawapo katika kundi kubwa la Wakristo wa Kanisa Katoliki nchini Korea waliouawa kwa ajili ya imani yao katika miaka 1791–1888. Wanakadiriwa kuwa 8.000 - 10.000. Padri huyo mmisionari aliuawa pamoja na askofu Simeoni-F ...

Amando wa Maastricht

Amando wa Maastricht alikuwa mmonaki, halafu mkaapweke, tena mmisionari katika maeneo mbalimbali ya Ulaya, hasa Ubelgiji, na askofu mkuu wa Tongres na Maastricht, leo nchini Ubelgiji. Tangu kale ametambuliwa kuwa mtakatifu. Sikukuu yake ni tarehe ...

Yosefu wa Anchieta

Yosefu wa Anchieta alikuwa mmisionari katika koloni la Brazil katika karne ya 16. Pamoja na mwenzake Manuel da Nóbrega alisaidia Waindio wengi kuingia Ukristo na kuwapatanisha na wakoloni Wareno. Anchieta ni kati ya waanzilishi wa jiji la São Pau ...

Andrea wa Soveral na wenzake

Andrea wa Soveral alikuwa padri wa Brazil wakati wa ukoloni. Awali alijiunga na shirika la Wajesuiti lakini baadaye aliliacha akabaki mwanajimbo. Aliuawa na Waprotestanti pamoja na waumini 69 wakati wa kuadhimisha Misa. Padri mwingine, Ambrosio F ...

Ansgar Mtakatifu

Mtakatifu Ansgar alikuwa askofu mmisionari kutoka Ufaransa. Tangu kale ametambuliwa kuwa mtakatifu. Sikukuu yake ni 3 Februari.

Antoni Maria Claret

Antoni Maria Claret i Clarà alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki kutoka Hispania na mwanzilishi wa mashirika mawili ya kitawa ya kimisionari. Alitangazwa na Papa Pius XI kuwa mwenye heri tarehe 25 Februari 1934, halafu Papa Pius XII alimtangaza mtak ...

Antonino Fantosati

Antonino Fantosati alikuwa mtawa wa shirika la Ndugu Wadogo na askofu mmisionari wa Kanisa Katoliki aliyefia dini yake nchini China wakati wa Uasi wa Waboksa. Kabla ya hapo alitangazwa na Papa Pius XII kuwa mwenye heri tarehe 27 Novemba 1946. Ana ...

Arbogasti

Arbogasti alikuwa mmisionari katika Alsace ya leo na askofu wa Strasbourg. Tangu zamani anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 21 Julai.

Abuna Aregawi

Abuna Aregawi alikuwa mmonaki wa karne ya 6, mfuasi wa Pakomi. Anatajwa kama mwanzilishi wa monasteri ya Debre Damo katika jimbo la Tigray, kwa agizo la mfalme Gebre Mesqel wa Axum. Abba Aregawi anaheshimiwa na Waorthodoksi wa Mashariki na Wakato ...

Austremoni

Austremoni alikuwa askofu kutoka Roma ambaye aliinjilisha mji wa Clermont Ferrand na Auvergne kwa jumla. Kadiri ya wanahistoria Wakristo. chini ya kaisari Decius 250 BK, Papa Fabian alituma maaskofu 7 kutoka Roma kwenda Gallia Ufaransa wa leo wak ...

Beninyo wa Dijon

Beninyo wa Dijon alikuwa padri ambaye aliinjilisha mkoa wa Burgundy na hatimaye alifia dini ya Ukristo huko. Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 1 Novemba.

Yakobo Berthieu

Yakobo Berthieu, S.J. alikuwa padri na mmisionari Mjesuiti nchini Madagaska. Wakati wa Uasi wa Menalamba mwaka 1896 alipata kuwa mfiadini wa kwanza wa nchi hiyo kutangazwa mwenye heri halafu mtakatifu. Papa Paulo VI alimtangaza mwenye heri tarehe ...

Petro wa Betancur

Petro wa Betancur, alikuwa mmisionari kutoka Hispania katika Amerika ya Kati. Alijulikana kama "Mt. Fransisko wa Amerika", naye ni mtakatifu wa kwanza mzaliwa wa visiwa vya Kanaria, pia anahesabiwa wa kwanza katika Guatemala na Amerika ya Kati. P ...

Bonifas mfiadini

Bonifas alikuwa mmonaki Mbenedikto kutoka Uingereza aliyetumwa kama mmisionari huko Ujerumani, halafu akawa askofu na hatimaye mfiadini katika Uholanzi wa leo. Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na wengineo kama mtakatifu, akiitwa pengine ...

Pierre Borie

Pierre-Rose-Ursule Dumoulin-Borie alikuwa padri Mkatoliki wa Ufaransa aliyefanya kazi kama mmisionari wa Paris Foreign Missions Society huko Vietnam. Papa Leo XIII alimtangaza mwenye heri tarehe 27 Mei 1900, halafu Papa Yohane Paulo II alimtangaz ...

Bruno Gutmann

Bruno Gutmann alikuwa mmisionari wa Kilutheri kwa niaba ya Misioni ya Leipzig katika Afrika Mashariki ya Ujerumani na Tanganyika na mtafiti wa kitaalamu wa utamaduni wa Wachagga. Sehemu kubwa ya maandiko ya Gutmann hayajatafsiriwa, yanapatikana k ...

Bruno wa Querfurt

Bruno wa Querfurt, O.S.B.Cam. alikuwa mmonaki wa urekebisho wa Wabenedikto wa Camaldoli, askofu, mmisionari na hatimaye mfiadini pamoja na wenzake 18 katika Ulaya mashariki. Tangu kale Bruno na wenzake wanaheshimiwa kama watakatifu. Sikukuu yao h ...

Carl Gotthilf Büttner

Carl Gotthilf Büttner alikuwa mchungaji wa Kiprotestanti, mmisionari na mtaalamu wa lugha kutoka Ujerumani.

Charles Lavigerie

Charles Martial Lavigerie alikuwa askofu mkuu wa Algiers, Aljeria, na kardinali wa Kanisa Katoliki. Ni maarufu hasa kwa kuanzisha mwaka 1868 shirika la Wamisionari wa Bibi Yetu wa Afrika kifupi: Wamisionari wa Afrika, M. Afr. linalojulikana kwa K ...

Daniel Comboni

Daniele Comboni, alikuwa mmisionari wa Kanisa Katoliki nchini Sudan. Ndiye aliyeanzisha shirika la Wamisionari wa Moyo Mtakatifu wa Yesu na shirika la Masista wa Afrika, wanaojulikana kama Wamisionari Wakomboni na Masista Wakomboni. Alitangazwa n ...

Damian de Veuster

Damian de Veuster alikuwa padri wa Kanisa Katoliki na mtawa wa Shirika la Mioyo Mitakatifu maarufu kama Picpus. Kwa miaka mingi alikuwa mmisionari katika kisiwa cha Molokai, alipojitosa kutumikia wagonjwa wengi wa ukoma waliotengwa huko hata akaa ...

Deikolo abati

Deikolo abati alikuwa mmonaki wa Ukristo wa Kiselti, mwanafunzi wa Kolumbani na kaka wa Gall. Alifanya nao kazi kubwa ya kueneza imani na umonaki huko Britania, halafu zaidi Ufaransa alipoendelea kuinjilisha hadi kifo chake katika monasteri aliyo ...

Deklan wa Ardmore

Deklan wa Ardmore alikuwa Mkristo wa Eire katika karne ya 5. Pamoja na kufanya umisionari, alianzisha monasteri ya Ardmore Ard Mór. Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 24 Julai.

Diego wa Alkala

Diego wa Alkala, O.F.M. alikuwa bruda wa shirika la Ndugu Wadogo. Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu. Alitangazwa kuwa hivyo na Papa Sixtus V mwaka 1588. Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 12 Novemba.

Erardo Mskoti

Erardo Mskoti alikuwa askofu wa mji huo wa Ujerumani. Kama Wakristo Waselti wengine wengi, kutoka visiwa vya Britania alihamia Ulaya bara ili kuinjilisha na kueneza umonaki. Anaheshimiwa na Wakatoliki kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tar ...

Filani wa Pittenweem

Filani wa Pittenweem, O.S.B. alikuwa mmonaki Mbenedikto kutoka kisiwa cha May, Uskoti. Filani alihama monasteri ya huko akaenda Pittenweem huko Fife akaongoa wakazi wake kuingia Ukristo. Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Fransisko Saveri

Fransisko Saveri ni jina la kawaida la Francisco de Jasso y Azpilicueta alikuwa padri wa Shirika la Yesu, ambalo alichangia kulianzisha pamoja na Ignas wa Loyola. Baadaye alitangaza Injili katika nchi nyingi za Ulaya, Afrika na Asia hata akawa ka ...

Fronti wa Perigueux

Fronti wa Perigueux alikuwa Mkristo ambaye aliinjilisha mji huo. Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 25 Oktoba.

Fursei abati

Fursei abati alikuwa mmonaki wa Ukristo wa Kiselti aliyefanya kazi kubwa kueneza imani na umonaki kotekote katika visiwa vya Britania, hasa kati ya Waanglia. Umaarufu wake ulipomvutia umati wa watu, alihamia Ufaransa alipoendelea kuinjilisha hadi ...

Gall Mtakatifu

Gall, Gallen au Gallus alikuwa mwanafunzi wa Kolumbani akamfuata kutoka Ireland kwenda kuinjilisha sehemu mbalimbali za Ulaya Bara akaishia katika Uswisi wa leo. Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake h ...

Helier Mtakatifu

Helier Mtakatifu alikuwa mkaapweke anaheshimika kama mmisionari wa kisiwa cha Jersey, karibu na Ufaransa. Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini. Sikukuu yake huadhimishwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waanglikana tarehe 16 Julai.

Inosenti wa Alaska

Inosenti wa Alaska, alikuwa padri mmisionari wa Kanisa la Kiorthodoksi la Urusi ambaye akawa askofu wa kwanza wa Kiorthodoksi katika bara la Amerika na hatimaye askofu mkuu wa Moscow na Russia yote. Alitangazwa na Patriarki Pimen I kuwa mtakatifu ...

Jean-Baptiste-Frézal Charbonnier

Jean-Baptiste-Frézal Charbonnier, M.Afr. alikuwa mmisionari Mkatoliki wa Wamisionari wa Afrika ambaye alikuwa Kasisi wa Kitume wa Tanganyika kuanzia Januari 1887 hadi Machi 1888.

Jose Vaz

Jose Vaz, CO, alikuwa padri wa Oratorio ya Mt. Filipo Neri, mmisionari nchini Sri Lanka. Vaz alifika huko wakati kisiwa hicho kimetekwa na Waholanzi, ambao wataka kulazimisha Ukalvini uwe dini rasmi. Bila kujali dhuluma yao, Jose aliizunguka nchi ...

Juliani wa Le Mans

Juliani wa Le Mans alikuwa askofu wa kwanza wa mji huo. Tangu zamani anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 27 Januari.

Julius wa Novara

Julius wa Novara alikuwa padri mmisionari. Tangu zamani anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 31 Januari.

Anjelo Klareno

Angelo ni maarufu kama mwanzilishi na kiongozi wa kundi mojawapo la Fraticelli, Wafransisko wa karne ya 14 walioshikilia ufukara kiasi cha kushindana na viongozi wa shirika na wa Kanisa Katoliki. Hao ndugu wenye nia ya kushika kanuni ya Ndugu Wad ...

Kolumba

Kolumba alikuwa mmonaki mmisionari kutoka Ireland aliyeeneza Ukristo kati ya Wapikti wa Scotland na anahesabiwa kati ya Mitume kumi na wawili wa Ireland. Anaheshimiwa na madhehebu mbalimbali kama mtakatifu. Sikukuu yake ni tarehe ya kifo chake, 9 ...

Korbiniani

Korbiniani alikuwa mmonaki kutoka Ufaransa au Visiwa vya Britania aliyetumwa kama mmisionari halafu akawa askofu katika Bavaria ya leo. Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake ni tarehe ya kifo chake.

Kyrilo wa Saloniki

Mtakatifu Kyrilo alikuwa mmisionari, mmonaki na mtaalamu wa Kigiriki aliyeweka msingi wa utamaduni wa Kikristo kati ya mataifa ya Waslavoni. Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya ...

Laurenti-Maria-Yosefu Imbert

Laurenti-Maria-Yosefu Imbert, M.E.P. ni mmojawapo katika kundi kubwa la Wakristo wa Kanisa Katoliki nchini Korea waliouawa kwa ajili ya imani yao katika miaka 1791–1888. Wanakadiriwa kuwa 8.000 - 10.000. Askofu huyo mmisionari na wafiadini wenzak ...

Leo wa Bayonne

Leo wa Bayonne alikuwa askofu mkuu wa Rouen, Ufaransa, halafu askofu wa Bayonne mmisionari kati ya Waeuskara kati ya Ufaransa na Hispania ambaye hatimaye aliuawa na Wavikingi kwa kukatwa kichwa. Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waort ...

Maloni wa Rouen

Maloni wa Rouen alikuwa askofu wa Rouen. Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 22 Oktoba.

Margarita Bourgeoys

Margerita Bourgeoys, CND, alikuwa mtawa wa Ufaransa na mwanzilishi wa Shirika La Notre Dame wa Montreal katika koloni la New France, ambayo sasa ni sehemu ya Québec, Kanada. Alitangazwa rasmi mwenyeheri na Papa Pius XII tarehe 12 Novemba 1950, ha ...

Marie-Nicolas-Antoine Daveluy

Marie-Nicolas-Antoine Daveluy, M.E.P. ni mmojawapo katika kundi kubwa la Wakristo wa Kanisa Katoliki nchini Korea waliouawa kwa ajili ya imani yao katika miaka 1791–1888. Wanakadiriwa kuwa 8.000 - 10.000. Askofu huyo mmisionari na wafiadini wenza ...

Martin-Luc Huin

Martin-Luc Huin, M.E.P. ni mmojawapo katika kundi kubwa la Wakristo wa Kanisa Katoliki nchini Korea waliouawa kwa ajili ya imani yao katika miaka 1791–1888. Wanakadiriwa kuwa 8.000 - 10.000. Padri huyo mmisionari na wafiadini wenzake 102 walitang ...

Methodio

Methodio wa Thesalonike alikuwa mmisionari wa Waslavoni wa Ulaya ya kusini-mashariki katika karne ya 9 BK akishirikiana na kaka yake Sirili. Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu pamoja na kaka yake. Sikukuu yao hua ...