ⓘ Free online encyclopedia. Did you know? page 35

Oreste Baratieri

Oreste Baratieri alikuwa mbunge wa Italia, jenerali wa jeshi na gavana wa koloni la Eritrea aliyeongoza Waitalia katika mapigano ya Adowa waliposhindwa vibaya na Ethiopia.

Derg

Derg ni neno la Kiethiopia kwa ajili ya "kamati" au "halmashauri". Inamaanisha hasa kikundi cha wanajeshi waliompindua Kaisari Haile Selassie mwaka 1974 na kushika mamlaka ya serikali nchini Ethiopia. Derg ilikuwa kamati ya wawakilishi kutoka seh ...

Dogali

Dogali katika tambarare ya pwani la Eritrea takriban 30 km kutoka Massawa ni mahali pa mapigano yaliyotokea tarehe 24 Januari 1887 kati ya wanajeshi wa Italia na Ethiopia. Kikosi cha Waitalia 587 kilielekea kaskazini kutoka Massawa kikashambuliwa ...

Almurabitun

Almurabitun walikuwa nasaba ya Waberberi kutoka Sahara iliyotawala eneo pana la kaskazini magharibi mwa Afrika na Rasi ya Iberia wakati wa karne ya 11. Chini ya nasaba hiyo milki yao ilitawala Moroko ya leo, Sahara ya Magharibi, Mauritania, Gibra ...

Hispania Mpya

Hispania Mpya ilikuwa eneo la kikoloni la Hispania katika Amerika ya Kaskazini, Amerika ya Kati na sehemu za visiwa vya Asia kuanzia mwaka 1535 hadi 1821. Lilijumlisha nchi za leo za Mexiko, Belize, Guatemala, El Salvador, Honduras, Nikaragua, Co ...

Kastilia

Kastilia ni eneo kubwa katikati ya Rasi ya Iberia na nchi ya Hispania. Kihistoria Ufalme wa Kastilia ulikuwa chanzo muhimu cha Hispania ya baadaye. Leo hii imegawiwa katika majimbo ya Kastilia-León, Madrid na Kastilia-La Mancha.

Mfalme Dongmyeong wa Goguryeo

Mfalme Dongmyeong wa Goguryeo, "Dongmyeongseongwang" pia anafahamika kwa jina lake la kuzaliwa kama Jumong, alikuwa kiongozi mwanzilishi wa taifa la Goguryeo, huko mbali kabisa kuelekea maeneo ya kaskazini mwa Falme Tatu za Korea. Wakati wa Gwang ...

Goguryeo

Goguryeo ni nasaba ya kwanza ya Korea ya kale ambayo ilianzishwa na Jumong mnamo 37 KK. Ilianzishwa karibu na eneo la mto Dongga ambapo ni tawi mkondo wa Abrok. Korea inajivunia sana na Goguryeo ambapo ndipo mwanzo mwa taifa la Korea.

Silla

Silla ilikuwa moja kati ya Falme Tatu za Korea, na moja kati ya nasaba iliokaa kwa muda mrefu sana katika historia ya Asia. Japokuwa ilianzishwa na Mfalme Park Hyeokgeose, ambaye anafahamika kama mwanzilishi wa famili ya Kikorea yenye jina la Par ...

Usultani wa Zanzibar

Usultani wa Zanzibar ulikuwa nchi kwenye pwani ya Afrika mashariki kati ya 1856 na 1964. Tangu 1890 ilikuwa nchi lindwa chini ya Uingereza. Ilianzishwa wakati wa kugawa Usultani wa Omani mwaka 1856 ikaishia mwaka 1964 baada ya mapinduzi ya Zanzib ...

Ugomvi wa Waarabu na Israeli

Ugomvi wa Waarabu na Israeli ni ugomvi wa muda mrefu kati ya nchi za Kiarabu za Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini upande mmoja na nchi ya Israeli upande mwingine. Ugomvi ulianza wakati wa kuundwa kwa taifa la kisasa la Israeli mwaka 1948 u ...

Babeli

Babeli ulikuwa mji wa kale katika Mesopotamia, muhimu kwa karne nyingi kama mji mkuu wa milki zilizotawala maeneo makubwa ya Mashariki ya Kati. Inatajwa mara nyingi katika Biblia, hasa kwa jina la Babuloni. Maghofu yake hupatikana karibu na mji w ...

Tiglath-pileseri I

Jina lake kwa lugha ya kwao iliandikwa "Tukulti-apil-esharra I" lakini "Tiglat-pileseri" ni umbo lililo kawaida kutokana na taarifa ya Biblia kuhusu mfalme mwenye jina hilihili Tiglath-pileseri anayetajwa katika Kitabu cha pili cha Wafalme, mlang ...

Uhamisho wa Babeli

Uhamisho wa Babeli unamaanisha kipindi cha Wayahudi kulazimishwa na Wababuloni kuishi ugenini hasa baada ya Yerusalemu kutekwa na kuangamizwa na mfalme Nebukadreza II.

Jumba la makumbusho la kitaifa la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MNRDC)

Jumba la makumbusho la kitaifa la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ni jumba la makumbusho lililopo Kinshasa, mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Ni sehemu muhimu ya historia ya kitamaduni ya makabila mengi na nyakati za kihistoria za nc ...

Katanga

Katanga ilikuwa jimbo la kusini-mashariki la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mji mkuu ulikuwa Lubumbashi iliyoitwa Elizabethville hadi 1966. Eneo lake lilikuwa km² 496.871 na wakazi 4.125.000. Kiswahili kilitumiwa kama lugha rasmi. Jimbo ni maa ...

Kongo ya Kibelgiji

Kongo ya Kibelgiji ni jina la koloni la Ubelgiji katika Afrika ya Kati hasa katika beseni ya mto Kongo kati ya mwaka 1908 hadi 1960. Leo hii ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Katika miaka 1925 hadi 1946 maeneo ya Rwanda na Burundi yalitawaliwa ...

Kenya African Union

Kenya African Union ilikuwa shirika la siasa liliyoundwa mwaka wa 1944 kwa kueneza malalamiko ya wananchi wa Kenya dhidi ya utawala wa kikoloni wa Uingereza wa wakati huo. Shirika la KAU ilidai haki za kuingia mashamba ya Kenya Highlands, ambayo ...

Kilima cha Hyrax

Kilima cha Hyrax ni eneo la kihistoria ya zamani mjini Nakuru katika mkoa wa Bonde la Ufa nchini Kenya. Inachukuliwa kama mmojawapo wa maeneo muhimu zaidi ya neolithic nchini Kenya. Mlima Hyrax iligunduliwa mnamo 1500 BK na iligubuliwa na Louis L ...

Koitalel Arap Samoei

Koitalel Arap Samoei alikuwa kiongozi shubavu wa Wanandi aliyeongoza vita vikali dhidi ya serikali ya upepari ya uingereza katika Africa Mashariki.Alikataa ujenzi wa reli iliyotekelezwa na wabeberu kwa sababu reli ilionekana kuwa mzingi kunyakua ...

Mashambulio ya kigaidi ya 7 Agosti 1998 katika Afrika ya Mashariki

Mashambulio ya kigaidi ya 7 Agosti 1998 katika Afrika ya Mashariki yalitokea katika miji ya Daressalam na Nairobi kwa kulipusha malori yaliyojaa baruti mbele ya balozi za Marekani kila mahali. Angalau watu 224 waliuawa na maelfu kujeruhiwa. Waten ...

Ngome ya Yesu

Ngome ya Yesu ni ngome ya kale mjini Mombasa. Iko kwenye kisiwa cha Mombasa ikitazama mlango wa bandari ya kale. Ilijengwa mwaka 1593 na msanifu Giovanni Battista Cairato kwa niaba ya Wareno na ilikuwa kituo muhimu cha Wareno kwenye njia ya mawas ...

Pwani na Bara ya Afrika Mashariki 1800-1845

Jumuiya za pwani zilikuwa zimetengana, kila moja ikiwa huru kutoka kwa nyingine na kila moja ikiwa na watawala wake. Athari za jumla za Waarabu wa Oman zilikuwepo Mombasa, Zanzibar na Kilwa tu, na hata katika maeneo hayo Waarabu hao waligawana ma ...

Uasi wa kijeshi wa 1982 nchini Kenya

Tarehe 1 Agosti 1982, siku ya Jumamosi, kundi la wanajeshi wa anga walivamia kituo cha Redio ya Sauti ya Kenya wakidai kuwa wamepindua serikali. Kiongozi wao alikuwa Hezekiah Ochuka ambaye alikuwa afisa wa ngazi ya chini ya jeshi akishirikiana na ...

Leptis Magna

Leptis Magna ilikuwa mji muhimu wa Dola la Roma katika jimbo la Afrika. Magofu yake yapo takriban kilomita 130 mashariki ya Tripoli. Mji ulianzishwa na Wafinisia ikawa chini ya Karthago halafu ikaingizwa katika Dola la Roma. Ilikuwa kitovu muhimu ...

Jamhuri ya Texas

Jamhuri ya Texas ilikuwa sehemu ya Mexiko iliyojitenga mwaka 1836 na kuendelea kama nchi ya kujitegemea hadi 1845 ilipotekwa na Marekani na kuwa jimbo la Texas ndani ya Maungano ya Madola ya Amerika. Chanzo cha harakati ya kujitenga ilikuwa idadi ...

Shirikisho la Madola ya Marekani

Kifupi chake cha Kimarekani mara nyingi ni CSA kwa Confederate States of America Shirikisho la Madola ya Marekani) lilikuwa serikali ya muda mfupi ambayo ilikuwepo kusini mwa Mareka wakati wa Vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Marekani. Lilianzishwa ...

Azteki

Azteki ilikuwa jina la ustaarabu muhimu nchini Mexiko kabla ya kufika kwa Wahispania. Waazteki walitawala nyanda ja juu za Mexiko ya Kati pamoja na mji mkuu Tenochtitlan uliokuwa Jiji la Meksiko jinsi uanvyoitwa leo.

Mexico (mji)

Jiji la Meksiko ni mji mkuu pia mji mkubwa wa nchi ya Mexiko. Uko kwenye nyanda za juu za Mexiko kwenye kimo cha m 2000 juu ya UB katika bonde refu linalopakana na milima mirefu. Kati ya milima hii ni volkeno za Popocatepetl na Iztaccihuatl na ny ...

Tenochtitlan

Tenochtitlan ilikuwa mji mkuu wa milki ya Azteki na mji mtangulizi wa Jiji la Mexiko. Ilianzishwa kwenye kisiwa ndani ya ziwa la Texcoco mnamo mwaka 1325 na Waazteki wahamiaji walipofika kwenye bonde la Mexiko kutoka kaskazini. Mji uliharibiwa na ...

Mapatano juu ya matumizi ya maji ya mto Nile ya 1929

Mapatano juu ya matumizi ya maji ya mto Nile yalifikiwa baina ya serikali za Misri na Ufalme wa Maungano mwaka 1929 kwa njia ya kubadilishana nyaraka za kidiplomasia. Misri ilikubali kuongezeka kwa maji yaliyotumiwa kwa umwagiliaji nchini Sudan k ...

Nasaba ya Waptolemaio

Kuhusu mtaalamu mashuhuri wa karne ya 2 BK angalia Klaudio Ptolemaio Nasaba ya Waptolemaio kwa Kigiriki Πτολεμαῖοι, Ptolemaioi walikuwa mlolongo wa watawala wa Misri ya Kale na familia zao tangu mwaka 305 KK hadi mwaka 30 BK. Waptolemaio walikuwa ...

Biafra

Biafra ilikuwa jamhuri iliyojitenga na Nigeria kati ya 1967 hadi 1970 iliyotambuliwa na nchi chache tu na kurudishwa Nigeria baada ya vita kali. Eneo la Biafra ilikuwa katika kusini-mashariki ya Nigeria inayokaliwa na Waigbo hasa wakati ule lilit ...

Francisco Pizarro

Francisco Pizarro alikuwa conquistador Mhispania aliyevamia Peru na kuharibu Dola la Inka mwaka 1533. Pizarro alizaliwa 1471 au 1478 mjini Trujillo Hispania. Mwaka 1509 aliondoka Hispania kwenda Amerika katika koloni mpya za Hispania.

Chekoslovakia

Chekoslovakia ilikuwa nchi ya Ulaya kati ya 1918 na 1992 iliyounganisha nchi za leo za Ucheki na Slovakia. Tangu 1 Januari 1993 Chekoslovakia imegawiwa kwa amani kuwa nchi mbili za Jamhuri ya Kicheki na Jamhuri ya Slovakia. Chekoslovakia ilianzis ...

Somalia ya Kiitalia

Somalia ya Kiitalia ilikuwa koloni ya Italia kwenye eneo la Somalia tangu miaka ya 1880 hadi 1960 mwaka wa uhuru. Kuanzia 1888 Italia ilijipatia mikataba ya ulinzi na masultani mbalimbali waliotawala maeneo madogo kwenye pembe la Afrika. Walitang ...

Historia ya Wapare

Kabla ya kuingia huko, inasemekana walikuwa Taveta, Kenya, kwa zaidi ya karne moja iliyopita na wakati huo walikuwa wakijulikana kwa jina la Waasu. Masimulizi yanasema walipoingia Tanganyika, walitamani kufanya makao yao kwenye miteremko ya Mlima ...

Kalenga

Kalenga ni jina la kata ya Wilaya ya Iringa Vijijini katika Mkoa wa Iringa, Tanzania yenye Postikodi namba 51201. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 6.963 waishio humo. Msimbo wa posta ni 51201. Hadi mw ...

Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki

Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki) ilikuwa shirika ya binafsi iliyoundwa na Karl Peters ikaanzisha koloni ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani.

Karagwe

Karagwe ni eneo la kihistoria ya Tanzania ya kaskazini magharibi upande wa magharibi wa Ziwa Viktoria Nyanza karibu na mpaka wa Burundi. Sehemu kubwa ya eneo hili leo ni wilaya ya Karagwe katika Mkoa wa Kagera. Kihistoria ilikuwa utemi au ufalme ...

Konde

Konde ni jina la kihistoria kwa ajili ya Unyakyusa katika wilaya ya Rungwe nchini Tanzania na pia sehemu ya kaskazini ya Malawi kando la Ziwa Nyassa ambako umbo la jina ni "ngonde". Wenyeji wake waliitwa Wakonde tofauti na Makonde au Wamakonde wa ...

Lugalo

Lugalo ni kata ya Wilaya ya Kilolo, Mkoa wa Iringa nchini Tanzania yenye Postikodi namba 51313. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 12.359 waishio humo. Lugalo iko karibu na barabara kuu ya TANZAM, takri ...

Mkoa wa Pangani

Mkoa wa Pangani ulikuwa mkoa wa kihistoria katika koloni la Afrika ya Mashariki ya Kijerumani ukahesabiwa kama mkoa wa tatu kati ya mikoa 24 ya koloni hilo lililojumlisha Tanzania bara, Rwanda na Burundi za kisasa.

Muziki wa Tanzania

Muziki wa Tanzania ni jina la kutaja muziki wenye asili ya Tanzania ya leo. Kama ilivyokuwa kwa binadamu wengine, wakazi wa eneo ambalo hatimaye limekuwa nchi ya Tanzania, walikuwa na utamaduni wao. Utamaduni huu ulikuwa ukitofautiana kati ya kab ...

Wangulu

Wangulu ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi mipakani mwa mikoa minne ya Tanga, Dodoma, Manyara na Morogoro, hasa upande wa Kusini-Magharibi mwa mkoa wa Tanga ambako sasa ni wilaya ya Kilindi na upande wa Kaskazini-Mashariki mwa mkoa wa Morogo ...

Karl Peters

Karl Peters au Carl Peters alikuwa mpelelezi na mwanasiasa Mjerumani aliyeanzisha koloni la Afrika ya Mashariki ya Kijerumani.

Rugaruga

Jina "Rugaruga" lilikuwa maarufu tangu miaka ya 1860 kama jina la askari wa Mtemi Mirambo aliyekuwa mtemi wa Wanyamwezi katika magharibi ya Tanzania ya leo. Mirambo aliwahi kutajirika kama mfanyabiashara kwa njia ya misafara kati ya pwani ya Baha ...

Sanamu ya Askari

Sanamu ya Askari au Askari Monument ni sanamu iliyopo penye kitovu cha jiji la Dar es Salaam mahali ambapo mitaa ya Samora na Azikiwe zinakutana. Sanamu inamwonyesha askari Mwafrika katika sare ya kijeshi ya Kings African Rifles wakati wa Vita Ku ...

Shirika kwa Ukoloni wa Kijerumani

Shirika kwa Ukoloni wa Kijerumani lilikuwa shirika la binafsi nchini Ujerumani lililoweka msingi kwa koloni la Afrika ya Mashariki ya Kijerumani katika eneo la Tanzania ya leo.

Tongoni

Tongoni ni jina la kata iliyopo ndani ya eneo la Jiji la Tanga katika Mkoa wa Tanga, Tanzania yenye Postikodi namba 21207. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ina wakazi wapatao 4.594 waishio humo. Tongoni iko takriban kilomita 1 ...