ⓘ Free online encyclopedia. Did you know? page 64

Kyerere

Kyerere ni kijiji kilichoko katika kata ya Nyakatuntu. Kijiji hiki kina vitongoji vinane ambavyo ni: Omukasamba Chameizibuzinza kwaumalufu "Yerusaremu" Kalebeje Kyerere omusitesheni Msumbiji Chijea Rwagati Chitoboka Kila sehemu kuna umaarufu wake ...

Mabwepande

Mabwepande ni jina la kata ya Wilaya ya Kinondoni katika Mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania yenye postikodi namba 14134. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ina wakazi wapatao 25.460 waishio humo. Mabwepande ina msitu mkubwa ambao u ...

Maporomoko ya Kalambo

Maporomoko ya Kalambo yanatokana na mto Kalambo ambao ni mpaka wa Tanzania na Zambia. Maporomoko ya maji haya ukiachilia kuwa ni ya pili baada ya yale ya Tugela Afrika ya Kusini lakini pia ndiyo maporomoko pekee yanayogawa mpaka wa nchi mbili. Ma ...

Masaki (Dar es Salaam)

Masaki ni sehemu iliyopo Dar es Salaam katika wilaya ya Kinondoni. Masaki kuna upepo mzuri kwa sababu sehemu hii ipo karibu na bahari, makazi yake yapo katika mpangilio wa mistari iliyonyoka, hivyo kufanya wakazi wa eneo hili kupata huduma mbalim ...

Mbagala

Mbagala ni jina la kata ya Wilaya ya Temeke katika Mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania yenye postikodi namba 15113.Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ina wakazi wapatao 52.582 waishio humo. Inasemekana kata hii ni chafu, ndiyo maana ...

Mikoa ya Tanzania

Majimbo haya 10 yalirithiwa na nchi huru ya Tanganyika. Tarehe 26 mwezi wa Aprili mwaka 1964 Tanganyika na Zanzibar zikaungana. Tanzania sasa ilikuwa na majimbo 12. Majimbo haya yalibadilishwa mnamo 1966 kuwa mikoa 20. Mkoa wa Katavi, awali iliku ...

Milima ya Mhandu

Milima ya Mhandu iko magharibi mwa Tanzania katika Mkoa wa Shinyanga. Milima hii inapatikana katika Wilaya ya Kahama Vijijini katika kata za Segese, Chela na Bulige katika kijiji cha Mwaningi. Milima hii inaendelea kuelekea Mkoa wa Geita na Mwanz ...

Milima ya Udzungwa

Milima ya Udzungwa ni jina la hifadhi inayopatikana katika bara la Afrika, nchini Tanzania, mkoani Iringa karibu na mpaka wa mkoa wa Morogoro, wilaya ya Kilombero. Hifadhi iko umbali wa kilometa 350 kusini mwa Dar es Salaam, kilometa 65 kutoka ka ...

Milima ya Usambara

Milima ya Usambara ni sehemu iliyoinuka upande wa Kaskazini Mashariki wa nchi ya Tanzania. Milima ya Usambara ni milima kunjamano yaani milima iliyoshikana kutoka mlima mmoja mpaka mwingine. Ni sehemu ya Tao la Mashariki. Wenyeji wanaoishi maeneo ...

Mkindo, Hembeti

Mkindo ni kijiji cha Tanzania kipo katika kata ya Hembeti, wilaya ya Mvomero mkoa wa Morogoro. Kijiji hiki kina jumla ya shule za msingi mbili. Shule ya msingi mkindo na Shule ya msingi mkindo B. Pia kijiji kina zahanati moja na pia inagulio amba ...

Morogoro Vijijini

Wilaya ya Morogoro Vijijini ni wilaya mojawapo ya Mkoa wa Morogoro nchini Tanzania yenye Postikodi namba 67200. Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 263.920. Ni wilaya yenye utajiri mkubwa wa hali ya hewa in ...

Mto Bubu

Mto Bubu ni jina la mito minne ya mkoa wa Dodoma. Mitatu inaelekeza maji yake kwenye bahari ya Hindi kupitia mto Rufiji. Mwingine hauelekei bahari wala ziwa lolote la kudumu, ila unaunda madimbwi mengi ya kinamasi cha Bahi ziwa Sulunga.

Mto Mponde (Singida)

Mto Mponde ni jina la mto wa mkoa wa Singida. Mto huo hauelekei bahari wala ziwa lolote la kudumu, ila unaunda madimbwi mengi ya kinamasi cha Bahi ziwa Sulunga.

Mto Msimbazi (Dar es Salaam)

Chanzo chake kinapatikana katika vilima vya Pugu, upande wa kaskazini wa Kisarawe. Njia yake ni km 42.5 hadi mdomo wake kwenye daraja la Selander. Mto Msimbazi unapitia eneo lote la Dar es Salaam ikiwa ni mto mkuu wa jiji hili. Mafuriko yake yana ...

Mto Songwe

Mto Songwe ni kati ya mito ya mkoa wa Songwe. Mto huo ambao umeupa mkoa jina lake una chanzo chake katika milima ya Umalila karibu na Santilya iliyopo kusini ya Mbeya ikielekea kaskazini na kuishia Ziwa Rukwa. Bonde lake limejulikana kati ya wata ...

Mto Wami

Mto Wami ni mto wa Tanzania mashariki, unaotiririka katika mkoa wa Morogoro hadi mkoa wa Pwani. Chanzo chake ni katika Milima ya Ukaguru na unaishia katika Bahari Hindi magharibi kwa Zanzibar. Beseni lake ni kubwa: km² 43.946. Matawimto yake ni M ...

Nachingwea

Wilaya ya Nachingwea ni kati ya wilaya za Mkoa wa Lindi, yenye postikodi namba 653. Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 162.081 Archived Februari 10, 2010 at the Wayback Machine. Wilaya hii imepakana na wil ...

Ngozi (mlima)

Kwa matumizi mengine ya jina hili tazama Ngozi Mlima Ngozi pia: Ngosi ni volkeno bwete katika safu ya milima ya Uporoto iliyopo kati ya miji ya Mbeya na Tukuyu nchini Tanzania. Tangu kuporomoka kwa kichwa cha volkeno, Ngozi ina umbo la kasoko yen ...

Nindai

Nindai ni kijiji kilichopo katika mwambao wa Ziwa Nyasa. Kijiji hiki kimepakana na vijiji vya Tawi, Yola na Nambingi. Kijiji kiko katika kata ya Ngumbo, Wilaya ya Nyasa. Mzee Magerumani ni mmoja wa waasisi wa kijiji hiki toka katika koo za kina S ...

Nyangaranga

Nyangaranga ni kijiji kilichopo ndani ya kata ya Mugeta, tarafa ya Chamriho iliyoko wilaya ya Bunda, mkoa wa Mara. Jamii ya kijiji hiki wengi wao ni wa kabila la Wakurya na hujishughulisha na kilimo pamoja na ufugaji. Mwanzoni mwa miaka ya 2000 w ...

Ol Doinyo Lengai

Ol Doinyo Lengai ni mlima wenye asili ya volkeno katika Tanzania ya Kaskazini. Iko takriban km 120 kaskazini-magharibi kwa Arusha na km 25 kusini kwa Ziwa Natron. Mlima una kimo cha m 2690 juu ya UB. Ni volkeno ya pekee duniani kutokana na aina y ...

Pangani (mto)

Kwa matumizi mengine ya jina hili angalia hapa Pangani Mto Pangani ni kati ya mito mikubwa ya Tanzania. Unabeba maji ya Milima ya Meru, Kilimanjaro, Pare na Usambara kwenda Bahari ya Hindi. Mdomo wake uko mjini Pangani.

Ruaha Mkuu

Ruaha Mkuu pia: Ruaha Mkubwa ni mto muhimu nchini Tanzania na tawimto la Rufiji. Huitwa "Ruaha Mkuu" kwa kuutofautisha na "Ruaha Mdogo" unaoishia ndani yake, si mbali na Iringa Mjini. Jina Ruaha kwa Kihehe linamaanisha "maji mengi".

Ruangwa

Hadi mwaka 2005 Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa ni miongoni mwa Halmashauri sita 6 ambazo zinaunda Mkoa wa Lindi, zingine ni Kilwa, Lindi mjini, Lindi Vijijini, Liwale na Nachingwea. Wilaya ipo kusini magharibi mwa Mkoa wa Lindi. Wilaya ipo kusi ...

Rufiji (mto)

Rufiji ni mto mkubwa wa Tanzania. Chanzo kiko Tanzania ya kusini-magharibi katika maungano ya matawimto ya mto Kilombero na mto Luwegu. Unafikia Bahari Hindi kwa njia ya delta yake takriban km 200 kusini kwa Dar es Salaam karibu na kisiwa cha Maf ...

Rukwa (ziwa)

8°00′S 32°25′E Ziwa Rukwa ni ziwa kubwa la magadi nchini Tanzania. Liko upande wa kusini magharibi wa nchi, karibu na Zambia, kati ya Ziwa Tanganyika na Ziwa Nyasa. Eneo la ziwa hubadilika mara kwa mara kufuatana na wingi wa mvua inayonyesha kati ...

Rungwe (mlima)

Mlima Rungwe ni volkeno iliyozimika ya Tanzania kusini magharibi ikikadiriwa ya kwamba mlipuko wake wa mwisho ulitokea mnamo miaka 2000 hadi 5000 iliyopita. Ukiwa na kimo cha m 2960 ni mlima mkubwa wa Tanzania ya Kusini. Mlima unasimama juu ya nc ...

Ruvu (Pwani)

Kwa matumizi mengine ya jina hili angalia Ruvu Ruvu zamani Kingani pia ni mto wa Mkoa wa Morogoro na Mkoa wa Pwani nchini Tanzania. Unapokea hasa maji ya upande wa mashariki wa milima ya Uluguru na kuyapeleka Bahari Hindi. Ruvu hii haina uhusiano ...

Sekenke

Sekenke ulikuwa mji wa kwanza na mgodi wa dhahabu Tanzania wakati ulianza kufanya operesheni mwaka 1909, baada ya dhahabu kugunduliwa huko mwaka 1907. Ilikuwa ni moja ya migodi miwili ili kufungua mkoa, na nyingine kuwa Mgodi wa dhahabu wa Kirond ...

Tabata

Tabata ni kata katika mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania yenye postikodi namba 12103. Kata hiyo ipo jijini, katika wilaya ya Ilala, mtaa wa Mandela. Kata ya Tabata imegawanyika katika maeneo mengi; baadhi ya hayo ni kama Tabata Bima, Tabata Kimanga, ...

Tendaguru

Majiranukta kwenye ramani: 9.7°S 39.2°E  / -9.7; 39.2 Tendaguru ni jina la mlima mdogo uliopo karibu na kijiji cha Nambiranji, kata ya Mipingo, takriban kilomita 60 upande wa magharibi-kaskazini kutoka Lindi kusini mwa Tanzania. Kilima hiki kina ...

Ubungo

Ubungo ni jina la kata ya wilaya ya Ubungo katika Mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania yenye postikodi namba 16103. Ubungo ipo katika sehemu ya kati ya magharibi mwa wilaya na inafahamika sana Tanzania kama kitovu kikuu cha Mabasi yaelekeayo mikoani. ...

Unguja

Unguja ni kisiwa kikubwa katika Bahari Hindi mkabala wa mwambao wa Afrika ya Mashariki karibu na Dar es Salaam. Unguja ndicho kisiwa kikuu cha funguvisiwa la Zanzibar ambavyo ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Unguja ina eneo la takrib ...

Wilaya ya Chalinze

Wilaya ya Chalinze ni moja ya wilaya nane za Mkoa wa Pwani, Tanzania. Maeneo yake yalitengwa mwaka 2015 na Wilaya ya Bagamoyo na halmashauri yake ilianza kufanya kazi rasmi mwezi Julai 2016. Makao makuu yapo mjini Chalinze Eneo la Wilaya ya Chali ...

Wilaya ya Ilala

Majiranukta kwenye ramani: 6.824°S 39.249°E  / -6.824; 39.249 Wilaya ya Ilala ni wilaya mojawapo ya Mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania yenye postikadi namba 12000. Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 634.924. ...

Wilaya ya Kilwa

Kwa matumizi mengine ya jina hili tazama Kilwa Wilaya ya Kilwa iko katika Mkoa wa Lindi, takriban kilometa 220 kusini mwa Dar es salaam. Kilwa imepakana na Mkoa wa Pwani upande wa kaskazini, Bahari ya Hindi upande wa mashariki, wilaya ya Lindi Vi ...

Wilaya ya Kinondoni

Wilaya ya Kinondoni ni moja ya wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam yenye postikodi namba 14000. Kwa lugha nyingine ni manisipaa ndani ya jiji la Dar Es Salaam. Eneo lake ni sehemu za kaskazini za jiji. Kinondoni inaanza upande wa pwani kwenye Selande ...

Wilaya ya Mafia

Mafia ni moja kati ya wilaya 6 za mkoa wa Pwani katika Tanzania yenye postikodi namba 61700. Eneo lake ni hasa Kisiwa cha Mafia na visiwa vidogo karibu nacho. Mji mkuu na makao makuu ya wilaya ni Kilindoni. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2 ...

Wilaya ya Ubungo

Ubungo ni jina la wilaya mojawapo ya Mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania yenye postikodi namba 16000. Ubungo inafahamika sana Tanzania kama kitovu kikuu cha Mabasi yaelekeayo mikoani pia ni sehemu ya pekee ttanzania ambayo ina barabara za juu Kituo c ...

Yombo Vituka

Yombo Vituka ni jina la kata ya Wilaya ya Temeke katika Mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania yenye postikodi namba 15115. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2002, kata ina wakazi wapatao 59.975 waishio humo. Yombo Vituka awali kwenye miaka ya 1 ...

Ziwa Kingili

Ziwa Kingili ni kati ya maziwa madogo ya Tanzania. Linapatikana katika mkoa wa Mbeya, mpakani mwa Busokelo na Kyela, likizungukwa na vijiji vya Ntaba kwa upande wa kaskazini na kijiji cha Kingili kwa upande wa kusini. Lina uzuri wa aina yake kuto ...

Ziwa Natron

02°25′S 36°00′E Ziwa Natron ni ziwa la chumvi lililopo kaskazini mwa Tanzania, katika Mkoa wa Arusha, karibu na mpaka wa Kenya, katika tawi la Afrika mashariki la Bonde la Ufa. Ziwa hilo hulishwa na mto Ewaso Ngiro wa Kusini na pia chemchemi zili ...

Adria

Bahari ya Adria au kwa kifupi Adria ni ghuba ya Mediteranea kati ya Rasi ya Italia na Rasi ya Balkani. Nchi zinazopakana nayo ni Italia upande wa magharibi, halafu Slovenia, Kroatia, Bosnia na Herzegovina, Montenegro na Albania upande wa masharik ...

Albania

Jamhuri ya Albania ni nchi ya Ulaya Kusini Mashariki. Imepakana na Montenegro, Kosovo, Masedonia Kaskazini na Ugiriki. Upande wa magharibi kuna pwani ya ghuba ya Adria ya bahari ya Mediteranea. Albania ni kati ya nchi zinazoendelea na imeomba kuj ...

Alpi

Alpi ni safu ya milima kunjamano katika Ulaya inayotenganisha Ulaya ya Kati na Ulaya ya Kusini, hususan rasi ya Italia.

Andorra

Utemi wa Andorra Kikatalani: Principat dAndorra, Kifaransa: Principauté dAndorre ni nchi ndogo katika Ulaya ya kusini magharibi. Katiba yake ni ya utemi lakini kuna watemi wawili, nao wako nje ya nchi. Mmoja ni rais wa Ufaransa na mwingine ni ask ...

Austria

Austria kwa Kijerumani: Österreich ni nchi ya Ulaya ya Kati. Imepakana na Ujerumani, Ucheki, Slovakia, Hungaria, Slovenia, Italia, Uswisi na Liechtenstein. Mji mkuu ni Vienna.

Bahari Nyeusi

Bahari Nyeusi ni bahari ya pembeni ya Mediteranea inayozungukwa na nchi kavu pande zote iliyoko kati ya Ulaya ya Mashariki na Asia ya Magharibi. Imeunganishwa na Bahari ya Mediteranea kwa njia ya Bahari ya Marmara pamoja na milango ya bahari ya B ...

Bahari ya Aegean

Majiranukta kwenye ramani: 39°N 25°E Bahari ya Aegean pia: Aegeis ; tamka a-e-ge-is ni moja kati ya sehemu za Bahari ya Mediteranea. Ipo kati ya Ugiriki na Anatolia Uturuki. Kupitia mlangobahari wa Dardaneli imeungana na Bahari ya Marmara, Bospor ...

Bahari ya Baltiki

Bahari ya Baltiki ni bahari ya kando ya Atlantiki katika Ulaya ya Kaskazini. Imezungukwa na nchi kavu pande zote isipokuwa kati ya Denmark na Uswidi kuna mlangobahari mwembamba wa kuiunganisha na Bahari ya Kaskazini.