ⓘ Free online encyclopedia. Did you know? page 71

Wamatengo

Kabila hilo linasifika kwa ukarimu na uhodari wa kazi. Kwa mujibu wa Egino Ndunguru, ambaye ameandika kwa kina kuhusu historia, mila na desturi za kabila hilo, Wamatengo wanapenda kuishi sehemu za milimani katika eneo lenye hali ya hewa nzuri na ...

Wambugwe

Wambugwe ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Manyara na hata katika mkoa wa Arusha. Wanapatikana hasa kaskazini mwa wilaya ya Babati, Tarafa ya Mbugwe katika Bonde la Ufa la Afrika Mashariki. Kabila la Wambugwe ni wa jamii ya W ...

Wambunga

Wambunga ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi upande wa kaskazini wa Wapogolo, katika wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro. Lugha yao ni Kimbunga.

Mingoko

Mingoko ni aina ya viazi vilivyo na mnasaba na kiazi kikuu. Hutumiwa kama chakula katika maeneo ya Kusini mwa Tanzania hususani katika Mkoa wa Mtwara. Mingoko hukua juu ya mizizi ya mmea utambaao unaoitwa mtipu. Mingoko kwa kawaida huwa haipandwi ...

Wampoto

Wampoto ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Ruvuma, Wilaya ya Mbinga. Eneo lao ni mwambao wa ziwa Nyasa. Wanapakana na Wanyasa kusini, Wamanda kaskazini na Wamatengo mashariki. Wanahusiana zaidi na majirani wao Wamatengo na Wan ...

Mwaka kogwa

Mwaka Kogwa ni mojawapo ya sherehe za mila ya watu wa Uswahilini pamoja na Zanzibar - Pemba na Unguja. Sherehe hizi hufanyika tarehe 23 Julai au 24 Julai ya kila mwaka. Wenyeji hupenda kusema sherehe hizi zilianzishwa katika visiwa vya Zanzibar k ...

Wamwera

Wamwera ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Lindi, hasa kwenye Wilaya ya Nachingwea, Lindi Vijijini na Ruangwa. Wamwera huwasiliana kwa lugha yao ya Kimwera wao wanasema Shimwera, lugha ambayo ina muundo unaoeleweka upande wa s ...

Wandali

Wandali ni kabila linalopatikana hasa kusini magharibi mwa nchi ya Tanzania, katika Wilaya ya Ileje, Mkoa wa Songwe. Kabla mkoa huo haujaanzishwa ilikuwa wilaya ya mkoa wa Mbeya. Pia wako nchini Malawi. Ni kabila lenye watu wakarimu sana kwa wage ...

Wandamba

Wandamba ni kabila la Tanzania wanaoishi kiasili katika mkoa wa Morogoro, Wilaya ya Malinyi na Wilaya ya Kilombero, hasa katika mji wa Ifakara pamoja na vijiji vya Mofu, Ruipa, Mbingu, Mngeta, Merera, Chita, Ngombo, Mlimba na Biro. Wa wanapatikan ...

Wandendeule

Mila zao ni nyingi. Wasichana wakishabalehe wanapelekwa porini kuchezwa unyago, na hurudishwa nyumbani kwa shangwe na vigelegele. Zao lao kuu la biashara ni tumbaku.

Wandengereko

Wandengereko ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi kusini kwa Dar es Salaam katika Mkoa wa Pwani: Wilaya ya Rufiji, Wilaya ya Mkuranga, Wilaya ya Kibiti na Wilaya ya Mafia. Katika wilaya za Kibiti na Rufiji asilimia kubwa kabisa ni Wandengereko ...

Wangindo

Wangindo ni kabila la watu wanaoishi Kusini mwa Tanzania, katika wilaya ya Liwale, mkoa wa Lindi. Lugha yao ni Kingindo. Wangindo walikuwa warushamishale maarufu na wazuri na walitumiwa sana, hasa na chifu wa Wahehe Mkwawa alipokuwa akipambana na ...

Wangoni

Wangoni ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Ruvuma, hasa upande wa Kusini wa Songea. Pia wako Msumbiji. Lugha yao ni Kingoni. Asili yao ni katika matembezi ya Wazulu walioenea kutoka Afrika Kusini wakati wa karne ya 19. Wangoni ...

Wangurimi

Wangurimi ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Mara, wilaya ya Serengeti. Wanapatikana kwa wingi huko Iramba, Majimoto, Busawe, Gantamome, Kisaka Nyiboko, Nyansurumunti, Gantamome, Busawe, Mesaga, Kenyamonta, Remungoroli, Maburi ...

Wanilamba

Wanyiramba: Hizi ni koo tano za Wanyiramba na wanapopatikana Kinampanda: Wanaishi sehemu za milimani hasa huko Kinampanda Anagimbu: Wapo Iramba Mashariki Waiambi/waiyambi: Wanaishi Nkungi na Iambi Anishai: Wanapatikana Kinandili na Akimbu: Hawa w ...

Wanindi

Wanindi ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Ruvuma, Wilaya ya Songea na wilaya ya Namtumbo, hususani katika vijiji vya Matepwende-Ligera, Ligera, Limamu, Ligunga na Magazini. Lugha yao ni Kinindi ambacho labda ni lahaja ya Kind ...

Wanyakyusa

Wanyakyusa ni kabila la watu wanaoishi kwenye wilaya ya Rungwe katika sehemu za kusini za Mkoa wa Mbeya, kaskazini kwa Ziwa Nyasa. Lugha yao, inayoendelea kutumika sana, ni Kinyakyusa. Mara nyingi Wagonde upande wa kusini wa mto Songwe nchini Mal ...

Wanyambo

Wanyambo ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Kagera, Wilaya ya Karagwe. Lugha yao ni Kinyambo. Wengi huwachanganya Wanyambo na Wahaya kwa kuwa lugha zao zinafanana, ila ukitazama kwa makini Kinyambo kinashabihana na Kinyankole, ...

Wanyamwanga

Wanyamwanga ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Songwe, Wilaya ya Momba, na Mkoa wa Rukwa, Wilaya ya Sumbawanga Vijijini. Lugha yao ni Kinyamwanga, jamii ya Kifipa. Kabila hilo ni zao la makabila zaidi ya manne likiwemo kabila ...

Wanyamwezi

Wanyamwezi ni kabila la watu wa Tanzania walio wenyeji wa mikoa ya Tabora na Shinyanga. Lugha yao ni Kinyamwezi. Vyakula vikuu vya kabila hilo ni ugali, michembe matobolwa, pamoja na viazi vitamu. Pengine anaitwa Mnyamwezi mtu yeyote yule mjanjam ...

Wanyaturu

Wanyaturu ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Singida. Lugha yao ni Kinyaturu, ambacho ni jamii ya Kibantu, lakini kina fonimu nyingi za Kikushi.

Wanyiha

Wanyiha ni kabila la watu wa "Tanzania. Katika wilaya ya Mbozi Wanyiha wengi hupatikana magharibi, hasa vijiji vya Itaka, Nambizo, Mbozi mission, Shiwinga, Igamba na maeneo mengine ya huko. Pia upande wa mashariki utawakuta katika vijiji vya Nyim ...

Nyumbanitu

Nyumbanitu na msitu unaopatikana katika kijiji cha Mlevela, kata ya Mdandu, Wilaya ya Wangingombe, ni Km 15 kutoka Njombe mjini. Jina "Nyumbanitu" ni muunganiko wa maneno mawili; nyumba na nitu. Neno "Nitu" manaa yake ni Giza au Nyeusi. Hivyo Nyu ...

Wapangwa

Wapangwa ni kabila la watu kutoka Milima Livingstone karibu na pwani ya mashariki ya Ziwa Nyasa, wilaya ya Ludewa, Mkoa wa Njombe, kusini mwa nchi ya Tanzania. Mwaka 2002 idadi ya Wapangwa ilikadiriwa kuwa 150.000. Lugha yao ni Kipangwa.

Wapare

Wapare ni kabila kutoka milima ya Pare, Mkoa wa Kilimanjaro, kaskazini mwa nchi ya Tanzania. Wanakadiriwa kuwa 1.000.000 hivi. Lugha yao ni Kipare au Chasu.

Wapimbwe

Wapimbwe ni kabila la watu kutoka Mkoa wa Rukwa, magharibi mwa nchi ya Tanzania. Mwaka 1987 idadi ya Wapimbwe ilikadiriwa kuwa 29.000. Lugha yao ni Kipimbwe.

Wapogolo

Wapogolo ni kabila la watu kutoka kusini-kati ya nchi ya Tanzania, hususan mkoa wa Morogoro. Lugha yao ni Kipogolo. Mwaka 1987 idadi ya Wapogolo ilikadiriwa kuwa 185.000.

Warangi

Warangi ni mojawapo kati ya makabila yanayopatikana katika wilaya ya Kondoa, mkoa wa Dodoma, mji ambao ndiyo makao makuu ya nchi ya Tanzania. Kirangi ndiyo hasa lugha ya Warangi, ambayo wao huiita Kilaangi. Warangi wamegawanyika katika dini ya Ui ...

Rubisi

Rubisi ni jina la pombe inayotengenezwa katika wilaya za Kyerwa na Karagwe mkoani Kagera. Pombe hii ni ya kienyeji na inakubalika wilayani humo. Watu wa wilaya hizo hupenda rubisi kwa sababu bei yake ni ndogo sana na ni sehemu ya utamaduni wao.

Warufiji

Warufiji ni kabila la watu kutoka eneo la pwani ya Tanzania, karibu na Mto Rufiji. Mwaka 1987 idadi ya Warufiji ilikadiriwa kuwa 200.000. Lugha yao ni Kirufiji.

Warungu

Warungu ni kabila la watu kutoka eneo la kusini-magharibi la Tanzania na kaskazini-mashariki mwa Zambia. Mwaka 1987 idadi ya Warungu nchini Tanzania ilikadiriwa kuwa 34.000. Nchini Zambia, idadi ya Warungu haijakadiriwa peke yao, lakini mwaka 199 ...

Warungwa

Warungwa ni kabila la watu kutoka eneo la wilaya ya Mpanda, mkoa wa Katavi, magharibi mwa nchi ya Tanzania. Mwaka 1987 idadi ya Warungwa ilikadiriwa kuwa 18.000. Lugha yao ni Kirungwa. Ni dhahiri kuwa Warungwa waliishi eneo/kijiji kilichoitwa Run ...

Wasafwa

Wasafwa ni kabila la watu kutoka eneo la milima ya mkoa wa Mbeya, kusini mwa nchi ya Tanzania. Wako hasa katika wilaya za Mbeya mjini, Mbeya vijijini, Mbozi na Chunya Mwaka 1987 idadi ya Wasafwa ilikadiriwa kuwa 158.000. Lugha yao ni Kisafwa. Ran ...

Wasagara

Wasagara ni kabila la watu kutoka eneo la kati ya nchi ya Tanzania, hasa mkoa wa Morogoro. Mwaka 1987 idadi ya Wasagara ilikadiriwa kuwa 79.000. Lugha yao asili ni Kisagara, lakini wengi wao wanatumia zaidi lugha nyingine, k.mf. Kikaguru au Kihehe.

Wasandawe

Wasandawe ni kabila linaloishi hasa katika eneo la wilaya ya Chemba, mkoa wa Dodoma, katikati ya nchi ya Tanzania. Wasandawe katika wilaya ya Chemba wanaishi hasa katika tarafa mbili, yaani Farkwa na Kwamtoro. Wengi ni wafupi na wa rangi ya njano ...

Wasegeju

Wasegeju ni kabila la watu kutoka eneo baina ya Tanga na mpaka wa Kenya, pwani ya nchi ya Tanzania. Kabila hili lina mahusiano mengi na Wadhaiso. Mwaka 2003 idadi ya Wasegeju ilikadiriwa kuwa chini ya 15.000, na chini ya 7.000 tu ndio wanaosema K ...

Washambaa

Washambaa ni watu wa kabila kutoka eneo la Milima ya Usambara, kaskazini-mashariki mwa nchi ya Tanzania. Mwaka 2001 idadi ya Washambaa ilikadiriwa kuwa 664.000. Washambaa wanaishi kwenye milima ya Usambara na lugha yao kubwa ni Kisambaa. Wasambaa ...

Washubi

Wasubi ni kabila mojawapo kati ya makabila ya Mkoa wa Kagera, nchini Tanzania. Wasubi wamechanganyika na Watanzania wengine na, ukiacha sehemu kubwa ya kabila hili ambao wanaishi katika Wilaya ya Biharamulo, wanapatikana kwenye maeneo mengine nch ...

Wasimbiti

Wasimbiti ni kabila la Tanzania kaskazini. Wanaishi kando ya Ziwa Nyanza katika wilaya ya Rorya karibu na mpaka wa Kenya na wa wilaya ya Musoma mjini. Wanaongea lugha ya Kisimbiti. Wasimbiti wenyewe wanakadiriwa kuwa watu 33.000 hivi, pamoja na v ...

Wasizaki

Wasizaki ni kabila la watu kutoka kaskazini-magharibi mwa nchi ya Tanzania, karibu na Ziwa Viktoria. Mwaka 1987 idadi ya Wasizaki ilikadiriwa kuwa 82.000. Lugha yao ni Kisizaki.

Wasuba

Wasuba ni kabila kutoka eneo la Ziwa Viktoria, nchini Tanzania, karibu na mpaka wa Kenya. Mwaka 1987 idadi ya Wasuba wa Tanzania ilikadiriwa kuwa 30.000. Lakini wengi zaidi huishi nchini Kenya, idadi yao ni 129.000. Lugha yao ni Kisuba japo wengi ...

Wasukuma

Jina "Wasukuma" lina maana ya watu wa Upande wa "Kaskazini", lakini maana hii haiwakilishi maana halisi ambayo watu wengi huitafsiri kwa mfano Wasukuma hutumia alama ya utambulisho dira kwa eneo fulani kwa viashirio vya makabila, kwa mfano wa jin ...

Wasumbwa

Wasumbwa ni kabila la Watu kutoka eneo la wilaya ya Bukombe, Mkoa wa Geita, Kaskazini mwa nchi ya Tanzania. Mwaka 1987 idadi ya Wasumbwa ilikadiriwa kuwa 191.000. Lugha yao ni Kisumbwa, jamii ya Kisukuma na Kinyamwezi.

Watemi

Watemi ni watu wa kabila kutoka eneo la Arusha, nchini Tanzania, karibu na mpaka wa Kenya. Mwaka 2002 idadi ya Watemi ilikadiriwa kuwa 30.000. Lugha yao ni Kitemi. Ni miongoni mwa makabila machache nchini yenye idadi ndogo ya watu kwa sababu ya m ...

Watiriko

Watiriko ni kabila dogo lililokaa kusini mwa wilaya ya Mpwapwa, mkoa wa Dodoma ulio katikati ya nchi ya Tanzania, hasa Kibakwe, Chamtumile, Ikuyu na maeneo ya karibu na hayo. Kabila hilo lina asili ya mchanganyiko wa kabila la Wahehe na kabila la ...

Watongwe

Watongwe ni kabila la watu kutoka eneo la Ziwa Tanganyika, Wilaya ya Kigoma Vijijini, sehemu ya magharibi ya nchi ya Tanzania. Lugha yao ni Kitongwe. Mwaka 2000 idadi ya Watongwe ilikadiriwa kuwa 31.551. Inawezekana kwamba idadi ya Watongwe ni ku ...

Watumbuka

Watumbuka ni Kabila la Watu kutoka eneo la mpaka baina ya Malawi, Tanzania, na Zambia. Mwaka 2001 idadi ya Watumbuka ilikadiriwa kuwa 940.000 katika Malawi na 392.000 nchini Zambia, lakini idadi ya Watumbuka wanaoishi Tanzania haijulikani.

Wavidunda

Wavidunda ni kabila la watu wa Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro katika Mashariki-kati ya nchi ya Tanzania. Jina linamaanisha kuwa wanaishi milimani. Mwaka 1987 idadi ya Wavidunda ilikadiriwa kuwa 32.000. Lugha yao ni Kividunda. Wavidunda wanazo ...

Wavinza

Wavinza ni kabila la watu kutoka kaskazini-magharibi mwa nchi ya Tanzania. Mwaka 1987 idadi ya Wavinza ilikadiriwa kuwa 10.000. Lugha yao ni Kivinza.

Waakie

Waakie ni kabila dogo la watu wa Tanzania wanaoishi upande wa magharibi wa Mkoa wa Arusha. Mwaka 2000 walihesabiwa kuwa 5.268. Waakie, kama makabila mengine ya wawindaji wa Kenya na Tanzania, wanaitwa pengine Wadorobo au Wandorobo. Wengi wao hawa ...