ⓘ Free online encyclopedia. Did you know? page 76

Basili na Prokopi

Basili na Prokopi walikuwa wamonaki walioteswa na kufungwa na kaisari Leo III wa Bizanti kwa sababu ya kuheshimu picha takatifu. Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu. Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 27 Februari.

Basili wa Ostrog

Basili wa Ostrog alikuwa askofu wa Kanisa la Kiorthodoksi la Serbia kwa jimbo la Zahumlje na Herzegovina. Anaheshimiwa na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Batazoni, Palemoni na Garuma

Batazoni, Palemoni na Garuma ni kati ya mapadri wa Ethiopia walioishi vizuri imani yao. Kwa kuwa hayajulikani mengine kuhusu historia yao, hawaorodheshwi tena na Martyrologium Romanum. Tangu kale wanaheshimiwa kama watakatifu. Sikukuu yao huadhim ...

Bazalota na Eufemia

Bazalota na Eufemia ni kati ya wanawake wa Ethiopia walioishi vizuri Ukristo wao monasterini. Kwa kuwa hayajulikani mengine kuhusu historia yao, hawaorodheshwi tena na Martyrologium Romanum. Tangu kale wanaheshimiwa kama watakatifu. Sikukuu yao h ...

Beano wa Ireland

Beano wa Ireland alikuwa Mkristo mkaapweke nchini Ireland, labda Mo-Béoóc wa Ros Cam. Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 16 Desemba.

Belino wa Padova

Belino wa Padova anakumbukwa kama askofu wa Padova wakati mgumu kuanzia mwaka 1128 hivi hadi kifodini chake. Alitangazwa na Papa Eujeni IV kuwa mtakatifu mfiadini. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 26 Novemba.

Benedikta wa Roma

Benedikta wa Roma alikuwa bikira Mkristo wa mji huo aliyejiunga na Galla katika monasteri aliyoianzisha karibu na Basilika la Mt. Petro. Alifariki siku 30 baada yake kama alivyotabiriwa katika njozi. Sifa zake zinajulikana kupitia kitabu cha Maja ...

Beninyo wa Milano

Beninyo wa Milano alikuwa askofu wa mji huo tangu mwaka 465 hadi kifo chake. Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 22 Novemba.

Beno wa Meissen

Beno wa Meissen alikuwa askofu wa Meissen kuanzia mwaka 1066 hadi kifo chake miaka arubaini baadaye. Aliheshimiwa kama mtakatifu tangu karne ya 13, lakini alitangazwa rasmi na Papa Adrian VI tarehe 31 Mei 1523. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya ...

Benyamini na Bejoki

Benyamini na Bejoki ni kati ya wamonaki wa Misri walioishi vizuri imani yao. Kwa kuwa hayajulikani mengine kuhusu historia yao, hawaorodheshwi tena na Martyrologium Romanum. Tangu kale wanaheshimiwa kama watakatifu. Sikukuu yao huadhimishwa tareh ...

Bernardino wa Siena

Alizaliwa na kubatizwa Massa Marittima Siena tarehe 8 Septemba 1380 katika familia Albizzeschi kutoka Siena, ambako alihamia baada ya kubaki yatima, ili alelewe na kusomeshwa na ndugu zake.

Bernardo wa Corleone

Bernardo wa Corleone alikuwa bruda wa shirika la Ndugu Wadogo Wakapuchini kutoka Italia. Mwaka 1768 alitangazwa na Papa Klementi XIII kuwa mwenye heri. Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu tangu alipotangazwa na Papa Yohane Paulo II tar ...

Besa wa Misri

Besa wa Misri alikuwa mmonaki Mkristo kati ya karne ya 5 BK. Tangu kale abati huyo anaheshimiwa na Waorthodoksi na Wakatoliki kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 23 Desemba.

Betari wa Chartres

Betari wa Chartres alikuwa mkaapweke na hatimaye askofu wa mji huo, Galia, leo Ufaransa). Tangu zamani anaheshimiwa na Kanisa Katoliki, Waorthodoksi, halafu na Waanglikana kama mtakatifu. Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 2 Agosti.

Betselote na Honori

Betselote na Honori ni kati ya wamonaki Wakristo wa Ethiopia wanaokumbukwa hadi leo. Habari zao ziliandikwa na kutunzwa katika mfululizo "Corpus Scriptorum Christianorum Orientalium, 28 = Corpus Scriptorum Christianorum Orientalium, Scriptores Ae ...

Bonito wa Lyon

Bonito wa Lyon au Bonitus wa Clermont aliwahi kuwa na vyeo mbalimbali muhimu, kama vile chansela wa mfalme, gavana wa Marseilles na hatimaye kwa miaka kumi askofu wa Auvergne baada ya kifo cha kaka yake Avitus. Baada ya kungatuka, alikwenda kuish ...

Bononi abati

Bononi abati, O.S.B. alikuwa abati nchini Italia kwa miaka 30 baada ya kuishi tangu ujanani kama mmonaki, hasa nchini Misri. Papa Yohane XIX mwaka 1026 alimtangaza mtakatifu. Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe ya kifo chake.

Luigi Carlo Borromeo

Luigi Carlo Borromeo alikuwa askofu Mkatoliki nchini Italia. Alipata upadrisho tarehe 30 Machi 1918. Tangu 1951 hadi 1952 alikuwa askofu msaidizi wa Jimbo la Lodi, akawa askofu wa Jimbo la Pesaro hadi kifo chake.

Bretanioni

Bretanioni alikuwa askofu wa mji huo kuanzia mwaka 360. Tangu zamani anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 25 Januari.

Aleksanda Briant

Aleksanda Briant, S.J. alikuwa padri Mjesuiti kutoka Uingereza. Baada ya kuacha ushirika wa Anglikana ili kujiunga na Kanisa Katoliki, alipata upadrisho huko Ufaransa mwaka 1578 akatumwa kwao alipofanya utume miaka 3. Alipokuwa gerezani alijiunga ...

Brisi wa Tours

Brisi wa Tours alikuwa askofu wa mji huo kwa miaka 47 baada ya mwalimu wake Martino wa Tours. Gregori wa Tours aliandika maisha yake. Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 13 Novemba.

Bruno wa Segni

Bruno wa Segni, O.S.B. alikuwa padri, mmonaki, halafu abati wa Montecassino na askofu wa Segni, Italia. Tarehe 5 Septemba 1181 Papa Lucius III alimtangaza kuwa mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 18 Julai

Bruno wa Wurzburg

Bruno wa Wurzburg alikuwa chansela wa Italia kwa niaba ya ndugu yake kaisari Konrad II, halafu askofu na mtawala wa Wurzburg hadi kifo chake. Bruno aliandika pia kitabu cha ufafanuzi wa Zaburi na tenzi kumi za Biblia, kwa kutumia madondoo ya Maba ...

Paulo Burali

Paulo Burali wa Arezzo alikuwa askofu mkuu wa Napoli na kardinali kutoka shirika la Wateatini. Ujuzi wake wa sheria ulimpa vyeo vikubwa katika mahakama za Napoli pamoja na nafasi za kutetea haki za wananchi. Hata hivyo aliacha kila kitu ili kufua ...

Cuthbert wa Lindisfarne

Cuthbert wa Lindisfarne alikuwa mmonaki, askofu na hatimaye mkaapweke wa Ukristo wa Kiselti mipakani mwa Uingereza na Uskoti wa leo. Tangu kale anaadhimishwa kama mtakatifu, hasa tarehe 20 Machi, lakini pia 31 Agosti na 4 Septemba.

Dado

Dado alikuwa askofu na waziri wa Wafaranki. Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waanglikana kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 24 Agosti.

Dagobert II

Dagobert II alikuwa mfalme wa Austrasia. Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 23 Desemba, siku alipouawa.

Danieli wa Mnarani

Danieli wa Mnarani alikuwa mmonaki ambaye alipata umaarufu kwa kuishi miaka 33 juu ya mnara karibu na Konstantinopoli. Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi na Wakatoliki kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 11 Desemba.

Danilo II

Danilo II alikuwa askofu mkuu wa Waserbia miaka 1324-1337. Akiwa kwanza mmonaki, aliandika kumbukumbu za watu na matukio mbalimbali ambazo ni kati ya maandishi muhimu ya Kiserbia. Anaheshimiwa na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Daudi Lewis

Daudi Lewis, S.J., alikuwa padri Mjesuiti aliyefanya uchungaji kwa siri muda wa miaka 30 huko Welisi. Mtoto wa kasisi wa Anglikana, aliongokea Kanisa Katoliki huko Paris Ufaransa akasomea upadri huko Roma Italia. Miaka mitatu baada ya kupadrishwa ...

Daudi wa Wales

David wa Wales alikuwa mmonaki, halafu askofu wa Mynyw. Alitunga kanuni ya kimonaki na alipinga vikali Upelaji. Wafuasi wake wengi waliinjilisha nchi za kandokando. Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu na msimamizi ...

Dekoroso wa Capua

Dekoroso wa Capua alikuwa askofu wa mji huo katika nusu ya pili ya karne ya 7. Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 15 Februari.

Delfino wa Bordeaux

Delfino wa Bordeaux alikuwa askofu wa mji huo kwa zaidi ya miaka ishirini akiueneza sana Ukristo. Baada ya kupata uaskofu alishiriki mitaguso kadhaa akauitisha mmoja huko Bordeaux katika juhudi zake dhidi ya uzushi wa Waprisiliani. Tangu kale ana ...

Demetriani

Demetriani alikuwa askofu wa 16 wa Antiokia kuanzia mwaka 253 hadi kifo chake, ingawa muda wote alikuwa uhamishoni na hatimaye gerezani kutokana na dhuluma ya mfalme Sapur I. Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tareh ...

Demetrius I wa Aleksandria

Demetrius I wa Aleksandria alikuwa Patriarki wa 12 wa jiji hilo la Misri lililowahi kuinjilishwa na Mtakatifu Marko. Kabla ya hapo alikuwa mkulima na kuishi na mke na ndugu. Klementi wa Aleksandria alipoacha kuongoza shule ya Aleksandria, Demetri ...

Didier wa Cahors

Didier wa Cahors alikuwa askofu wa Cahors baada ya ndugu yake Rusticus wa Cahors. Chini yake jimbo lilistawi katika miaka 630-655. Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 15 Novemba.

Domesi Mganga

Domesi Mganga alikuwa mmonaki wa Kapadokia aliyeishi katika pango la mlima Quros katika Armenia ya Kale. Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 5 Julai.

Donasyani, Presidi na wenzao

Donasyani, Presidi na wenzao Mansueti, Jermano na Foskolo walikuwa maaskofu wa Kanisa Katoliki katika Afrika Kaskazini walioteswa kikatili sana na Wavandali katika karne ya 5, wakati wa utawala wa mfalme Huneriki aliyekuwa Mwario. Hatimaye walipe ...

Donato Mkuu

Donato Mkuu kutoka Casae Negrae alikuwa askofu wa Karthago kuanzia mwaka 313. Alishika msimamo mkali dhidi ya Wakristo walioasi ili kuokoa uhai wao wakati wa dhuluma ya kikatili ya Dola la Roma dhidi yao, hasa chini ya Kaisari Dioklesian. Kwa aji ...

Donato Mskoti

Donato Mskoti alikuwa askofu wa Fiesole kuanzia mwaka 829. Kabla ya hapo alilelewa na wamonaki na kupata elimu kubwa akawa mwalimu na mshairi. Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ...

Dorotea wa Aleksandria

Dorotea wa Aleksandria alikuwa mwanamke bikira wa mji huo wa Misri, ambaye alikataa katakata vishawishi vya kaisari Maksiminus Daia na kwa sababu hiyo alinyanganywa utajiri wake wote na kupelekwa uhamishoni huko Arabia. Masimulizi haya yaliandikw ...

Doroteo wa Aleksandria

Doroteo wa Aleksandria alikuwa Mkristo wa mji huo wa Misri, ambaye aliteswa na Waario kwa kushika imani sahihi ya Kanisa Katoliki. Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 9 Oktoba.

Dorotheo wa Gaza

Dorotheo wa Gaza alikuwa mmonaki na mwandishi wa Kikristo. Baada ya kusoma sana, mwaka 525 hivi aliamua kutawa. Kisha kupata malezi kutoka kwa Yohane Nabii na Barsanufi wa Gaza, alianzisha monasteri mpya alipoishi hadi kifo chake, kati ya miaka 5 ...

Dositeo wa Gaza

Dositeo wa Gaza alikuwa mmonaki karibu na Gaza, Palestina, ingawa labda alitokea Misri. Alifariki bado kijana kutokana na ugumu wa maisha aliyoyashika chini ya Dorotheo wa Gaza. Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Siku ...

Droktovei

Droktovei alikuwa mmonaki nchini Ufaransa anayetajwa kama mfuasi wa Jermano wa Autun ambaye, baada ya kuchaguliwa kuwa askofu, alimchukua naye, halaku akamweka kuongoza monasteri mpya ambayo chini yake ilistawi sana. Venansi Fortunati alimsifu sa ...

Eberigisili

Eberigisili alikuwa Askofu mkuu wa Cologne, Ujerumani, wa tano kati ya wale wanaojulikana kwa hakika, na wa kwanza mwenye jina la Kifaranki. Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 24 Oktoba.

Edilburga

Edilburga alikuwa mtoto wa mfalme Anna wa Anglia Mashariki, katika Uingereza wa leo, halafu mmonaki na hatimaye abesi baada ya dada yake Seathrid. Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tar ...

Edmundi Gennings

Edmundi Gennings alikuwa Mkristo wa Kanisa la Anglikana kabla hajajiunga na Kanisa Katoliki. Baada ya kuhamia Ufaransa, aliingia seminari kwa lengo la kurudi kwao kufanya uchungaji usioruhusiwa na serikali, akapewa daraja ya upadri 1590. Hapo ali ...

Efebo wa Napoli

Efebo wa Napoli alikuwa askofu wa 8 wa Napoli, Italia anayesifiwa kwa juhudi zake kama mchungaji wa waumini na kwa miujiza yake. Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 23 Mei.

Egbert wa Ripon

Ecgberht alikuwa sharifu wa Kigermanik wa Northumbria.Mwaka 664, akiwa kijana, alikwenda kusoma katika monasteri ya Ireland. Huko alimfahamu Chad wa Mercia. Alipopatwa na tauni akiwa na umri wa miaka 25 aliweka nadhiri ya kufanya daima toba nje y ...