ⓘ Free online encyclopedia. Did you know? page 77

Getrude wa Nivelles

Getrude wa Nivelles alikuwa abesi Mbenedikto katika Ubelgiji ya leo, alipoanzisha na mama yake Itta monasteri dabo. Pamoja na juhudi katika kukesha na kufunga, alifaulu kupatanishwa watawala waliochukiana. Anaheshimiwa tangu zamani kama mtakatifu ...

Goar

Goar alikuwa padri na mkaapweke aliyejenga hoteli na hospitali kwa ajili ya kuwahudumia kiroho na kimwili wapitanjia. Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake inaadhimishwa kila tarehe 6 Julai.

Godric wa Finchale

Godric wa Finchale alikuwa kwanza mfanyabiashara wa kimataifa, halafu mkaapweke nchini Uingereza. Ni maarufu kwa upole aliokuwanao kwa wanyama na kwa nyimbo na tungo zake nyingine. Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki kama mtakatifu.

Gorgonia wa Nazienzi

Gorgonia wa Nazienzi alikuwa mtoto wa Gregori Mzee na Nona, hivyo dada wa Gregori wa Nazianzo na Sesari wa Nazianzo. Aliishi huko Kapadokia, mkoa wa Dola la Roma katikati ya Uturuki wa leo. Katika ndoa yake alizaa watoto wengiwengi na kuwaleta wo ...

Grasyano wa Tours

Kadiri ya wanahistoria Wakristo. chini ya kaisari Decius 250 BK, Papa Fabian alituma maaskofu 7 kutoka Roma kwenda Gallia Ufaransa wa leo wakahubiri Injili: Grasyano huko Tours, Trofimo huko Arles, Paulo huko Narbonne, Saturnini huko Toulouse, De ...

Gregori wa Agrigento

Gregori wa Agrigento alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki huko Agrigento, Sicilia, leo nchini Italia kuanzia mwaka 590 hadi kifo chake. Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 23 Novemba ...

Grellan Mtakatifu

Mt. Grellan alikuwa Mkristo hodari wa karne ya 5 na karne ya 6 aliyejenga makanisa mbalimbali nchini Ireland. Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 10 Novemba.

Guarino wa Palestrina

Guarino wa Palestrina alikuwa kanoni, Mwaugustino, halafu askofu wa Palestrina na kardinali maarufu kwa wema wake. Tangu kale ametambuliwa kuwa mtakatifu. Sikukuu yake ni tarehe 6 Februari.

Gwido wa Anderlecht

Gwido wa Anderlecht alikuwa mkulima mkarimu ambaye baadaye aliishi bila makao maalumu, akienda hija sehemu mbalimbali, hadi Nchi Takatifu alikokaa miaka kadhaa. Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu. Sikukuu yake ni tarehe 12 Septemba.

Habetdeus wa Teudali

Habetdeus wa Teudali alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki katika mji wa Teudali. Alipelekwa uhamishoni katika dhuluma ya Genseriki, mfalme wa Wavandali. Habari zake zimeandikwa na askofu Vikta wa Vita. Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu. Sikukuu ...

Hedwig wa Andechs

Hedwig wa Andechs, pia: Hedwig wa Silesia ; alikuwa mwanamke wa ukoo tawala wa Andechs ambaye, kisha kuolewa, akawa malkia wa Polandi hadi mwaka 1238. Tarehe 26 Machi 1267 Papa Klementi IV alimtangaza mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa na Wakat ...

Helaniki na Begei

Helaniki na Begei ni kati ya Wakristo wa Misri walioishi vizuri imani yao. Helaniki alikuwa askofu na Begei padri. Kwa kuwa hayajulikani mengine kuhusu historia yao, hawaorodheshwi tena na Martyrologium Romanum. Tangu kale wanaheshimiwa kama wata ...

Helena Mtakatifu

Helena alikuwa mke wa kaisari Constantius Chlorus. Ni maarufu hasa kama mama Mkristo wa Konstantino Mkuu aliyemuelekeza kupenda dini yake na hivyo kuchangia uanzishaji wa uhuru wa dini katika Dola la Roma baada ya miaka 250 ya dhuluma dhidi yake. ...

Heraklemon

Heraklemon ni kati ya Wakristo wa Ethiopia ya leo walioishi vizuri imani yao utawani. Kwa kuwa hayajulikani mengine kuhusu historia yake, haorodheshwi tena na Martyrologium Romanum. Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishw ...

George Herbert

George Herbert alikuwa mwanashairi, mhubiri na kasisi maarufu wa Kanisa la Uingereza. Anaheshimiwa na Waanglikana kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 27 Februari, ila Walutheri wa Marekani wanaifanya tarehe 1 Machi.

Heribert wa Cologne

Heribert wa Cologne alikuwa Askofu mkuu wa Cologne, Ujerumani, na Chansella wa Dola Takatifu la Roma chini ya kaisari Otto III. Aliheshimiwa sana akiwa hai akatangazwa na Papa Gregori VII kuwa mtakatifu mwaka 1075 hivi. Sikukuu yake huadhimishwa ...

Hesiki wa Gaza

Hesiki wa Gaza alikuwa mkaapweke mwanafunzi wa Hilarioni wa Gaza, aliyefuatana naye katika safari zake kwenda Misri, Sicilia, Dalmatia na Kupro. Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tareh ...

Hilari wa Mende

Hilari wa Mende alikuwa askofu wa mji huo, Galia, leo Ufaransa) baada ya kuishi upwekeni. Alipinga kwa mafanikio Upagani sehemu mbalimbali za nchi. Tangu zamani anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake inaadhim ...

Hilarioni wa Gaza

Hilarioni alikuwa mkaapweke aliyetumia sehemu kubwa ya maisha yake jangwani kufuatana na mfano wa Antoni Mkuu. Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 21 Oktoba.

Hilda wa Whitby

Hilda wa Whitby alikuwa abesi mwanzilishi wa monasteri ya Whitby, iliyofuata desturi za Ukristo wa Kiselti. Ndipo palipofanyika Sinodi ya Whitbyiliyokubali kufuata desturi za Kanisa la Roma. Muhimu katika kuvuta Waangli na Wasaksoni katika Ukrist ...

Honorati wa Amiens

Honorati wa Amiens alikuwa askofu wa saba wa mji huo. Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 16 Mei.

Honorati wa Milano

Honorati wa Milano alikuwa askofu wa mji huo tangu mwaka 567 hadi kifo chake. Walombardi walipovamia Italia, aliwaokoa waumini wengi kwa kuwasaidia wahamie Genova. Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake ...

Honorati wa Vercelli

Honorati wa Vercelli anakumbukwa kama askofu wa 2 wa Vercelli kuanzia mwaka 396 hadi kifo chake. Kabla ya hapo aliishi na mtangulizi wake Eusebi wa Vercelli monasterini. Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 29 ...

Hortulani wa Afrika Kaskazini

Hortulani wa Afrika Kaskazini alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki katika Afrika Kaskazini). Alipelekwa uhamishoni katika dhuluma ya Genseriki, mfalme wa Wavandali. Habari zake zimeandikwa na askofu Vikta wa Vita. Tangu kale anaheshimiwa kama mtakat ...

Maria Kresensya Hoess

Maria Crescentia Höss, T.O.R., alikuwa mwanamke mmonaki wa Utawa Hasa wa Tatu wa Mt. Fransisko. Mwaka 1900, alitangazwa mwenye heri na Papa Leo XIII, halafu mwaka 2001 alitangazwa mtakatifu na Papa Yohane Paulo II. Sikukuu yake huadhimishwa tareh ...

Alberto Hurtado

Alberto Hurtado Cruchaga alikuwa padri wa Kanisa Katoliki na mtawa wa Shirika la Wajesuiti kutoka nchi ya Chile. Alisoma sheria na kujitahidi kwa ajili ya mafukara nchini mwake. Sababu ya kifo chake ilikuwa kansa. Mwaka 2005 alitangazwa na Papa Y ...

Ida Mtakatifu

Ida mtakatifu alikuwa Mkristo bikira wa Ireland aliyeshika maisha ya umonaki akawa abesi. Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 15 Januari.

Ifigenia wa Ethiopia

Ifigenia wa Ethiopia alikuwa mwanamke wa karne ya 1 ambaye maisha yake yanasimuliwa na kitabu Golden Legend. Humo tunasikia kwamba alikuwa bikira aliyeongokea Ukristo na kuwekwa wakfu kwa Mungu kwa njia ya Mathayo Mtume, alipokuwa anaeneza Injili ...

Ignas wa Laconi

Ignas wa Laconi, O.F.M. Cap. ni jina la kitawa la Vincenzo Peis alikuwa bruda ombaomba wa shirika la Ndugu Wadogo Wakapuchini kutoka kijiji cha Laconi, mkoani Sardinia. Alitangazwa na Papa Pius XII kuwa mwenye heri mwaka 1940, halafu mtakatifu mw ...

Ignas wa Santhià

Ignas wa Santhià alikuwa mtawa wa shirika la Ndugu Wadogo Wakapuchini na padri wa Kanisa Katoliki kutoka Italia. Jina lake la awali lilikuwa Lorenzo Maurizio Belvisotti. Papa Paulo VI alimtangaza mwenye heri tarehe 17 Aprili 1966, halafu Papa Yoh ...

Iltruda

Iltruda alikuwa bikira Mkristo aliyekataa ndoa akaenda kuishi kama mkaapweke karibu na monasteri iliyoongozwa na kaka yake, abati Guntardi. Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya ...

Iluminata wa Todi

Iluminata wa Todi alikuwa mwanamke anayeheshimiwa na Wakristo wa madhehebu mbalimbali kama mtakatifu bikira, pengine pia mfiadini. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 29 Novemba

Inosenti askofu

Inosenti askofu ni kati ya Wakristo wa Afrika Kaskazini walioishi vizuri imani yao. Kwa kuwa hayajulikani mengine kuhusu historia yake, haorodheshwi tena na Martyrologium Romanum. Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa ...

Invensyo

Invensyo alikuwa askofu wa tatu wa mji huo kuanzia mwaka 381, alipoteuliwa na Ambrosi, askofu mkuu wa Milano. Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake ni 8 Februari.

Ipasi, Asiani na Andrea

Ipasi, Asiani na Andrea walikuwa maaskofu na padri walioteswa na kaisari Leo III wa Bizanti na hatimaye kuuawa kwa kutupwa waliwe na mbwa kwa sababu ya kuheshimu picha takatifu. Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakati ...

Isaka Mkuu

Isaka Mkuu alikuwa mmonaki, mwanateolojia na askofu kutoka Armenia. Mtoto wa Nerses I na kilembwekeza wa Gregori Mletamwanga, alipofiwa mke wake alijiunga na monasteri, halafu kama Patriarki alipigania umoja wa Kanisa kwa msingi wa imani sahihi y ...

Isidora mkaapweke

Isidora mkaapweke ni kati ya Wakristo wa Misri waliofuata vizuri imani yao. Kwa kuwa hayajulikani mengine kuhusu historia yake, haorodheshwi tena na Martyrologium Romanum. Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu. Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 10 ...

Isidori mkulima

Isidori mkulima alikuwa mkulima wa Hispania maarufu kwa upendo wake kwa maskini na wanyama. Papa Paulo V alimtangaza mwenye heri tarehe 2 Mei 1619, halafu Papa Gregori XV alimtangaza mtakatifu tarehe 12 Machi 1622. Sikukuu yake huadhimishwa tareh ...

Isidori wa Misri

Isidori wa Misri ni kati ya mapadri wa Misri walioishi vizuri imani yao jangwani. Alimuunga mkono Athanasius dhidi ya Uario. Kwa sababu hiyo alidhulumiwa. Tangu kale wanaheshimiwa kama mtakatifu lakini haorodheshwi tena na Martyrologium Romanum. ...

Isidori wa Pelusio

Isidori wa Pelusio alikuwa mmonaki padri wa Misri. Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi wa Mashariki na Wakatoliki kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 4 Februari.

Isidori wa Skete

Isidori wa Skete ni kati ya mapadri wa Misri walioishi vizuri imani yao jangwani. Kwa kuwa hayajulikani mengine kuhusu historia yake, haorodheshwi tena na Martyrologium Romanum. Tangu kale wanaheshimiwa kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa t ...

Matthias Joseph Isuja

Matthias Joseph Isuja alikuwa askofu Mkatoliki nchini Tanzania. Aliwekwa wakfu na Kardinali Laurean Rugambwa mwaka 1972. Tangu mwaka huo hadi 2005, alipostaafu, alikuwa askofu wa Jimbo la Dodoma. Kwa asili, Askofu Isuja ni Mrangi aliyetokea Haubi.

Jacques Paul Migne

Jacques Paul Migne alikuwa padri kutoka Ufaransa. Ni maarufu hasa kwa kukusanya na kuchapisha maandishi ya kale ya mababu wa Kanisa na ya mapapa, pamoja na kuandika mwenyewe vitabu vya teolojia. Matoleo yake maarufu ni hasa Patrologia Latina na P ...

Jeanne dArc

Jeanne dArc alikuwa msichana Mfaransa anayeheshimiwa kama shujaa wa uhuru wa Ufaransa na mtakatifu wa Kanisa Katoliki. Tarehe 18 Aprili 1909 alitangazwa na Papa Pius X kuwa mwenye heri na tarehe 16 Mei 1920 Papa Benedikto XV alimtangaza mtakatifu ...

Jeradi Majella

Jeradi Majella alikuwa bradha wa shirika la Mkombozi. Alitangazwa na Papa Leo XIII kuwa mwenye heri tarehe 29 Januari 1893 akatangazwa na Papa Pius X kuwa mtakatifu tarehe 11 Desemba 1904.

Jeradi wa Potenza

Jeradi wa Potenza alikuwa askofu wa mji huo kuanzia mwaka 1111 akawa maarufu kwa miujiza yake. Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu, ingawa alitangazwa na Papa Kalisti II mwaka uliofuata kifo chake bila maandishi. Sikukuu yak ...

Jerlando wa Agrigento

Jerlando wa Agrigento alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki huko Agrigento, Sicilia, leo nchini Italia. Alitangazwa mtakatifu mwaka 1159. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 25 Februari.

Jermano wa Capua

Jermano wa Capua alikuwa askofu wa mji huo kuanzia mwaka 516. Kabla ya hapo alikuwa ameuza mali aliyorithi kwa familia yake tajiri ili kusaidia maskini akaishi kitawa. Rafiki wa Benedikto wa Nursia, tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na W ...

Jiminyano wa Modena

Jiminyano wa Modena alikuwa askofu wa mji huo wa Italia Kaskazini kuanzia mwaka 342/344 ingawa kwanza alikimbia jukumu hilo alipochaguliwa akiwa bado shemasi tu. Alimaliza Upagani jimboni na kupambana na Uario akishirikiana na Ambrosi wa Milano n ...

John Knox

John Knox alikuwa Mskoti mwenye akili kali, mwanateolojia, na mwandishi ambaye alikuwa kiongozi wa madhehebu ya Wapresbiteri yaliyoenea nchini Uskoti katika karne ya 16.