ⓘ Free online encyclopedia. Did you know? page 80

Timotheo IV wa Aleksandria

Timotheo IV wa Aleksandria kuanzia mwaka 517 hadi kifo chake alikuwa Patriarki wa Aleksandria na Papa wa 32 wa Kanisa la Wakopti ambalo linamheshimu kama mtakatifu kwa jina la Timotheo III. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake.

Tisyano wa Brescia

Tisyano wa Brescia alikuwa askofu wa 15 wa mji huo katika mkoa wa Lombardia, Italia Kaskazini. Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 3 Machi.

Tisyano wa Oderzo

Tisyano wa Oderzo alikuwa askofu wa mji huo. Alipinga Uario. Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 16 Januari.

Titoes

Titoes ni kati ya Wakristo wa Misri walioishi vizuri imani yao kwa kutawa. Kwa kuwa hayajulikani mengine kuhusu historia yake, haorodheshwi tena na Martyrologium Romanum. Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 26 ...

Troiani wa Saintes

Troiani wa Saintes alikuwa askofu wa mji huo miaka 511 - 532. Anafikiriwa kuwa mwandishi wa barua kwa Eumeri wa Nantes inayopatikana katika Patrologia Latina, 67. Gregori wa Tours anasimulia alivyoheshimiwa na wengi kwa maadili yake. Hata leo ana ...

Turiavo wa Dol

Turiavo wa Dol alikuwa abati na askofu huko Bretagne, leo nchini Ufaransa. Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu. Sikukuu yake inaadhimishwa kila tarehe 13 Julai.

Lorcán Ua Tuathail

Lorcán Ua Tuathail alikuwa askofu mkuu wa Dublin, Ireland, wakati kisiwa hicho kilipovamiwa na Wanormani. Alichangia sana urekebisho wa Kanisa la huko katika karne ya 12 na kupatanisha wenyeji na wavamizi. Tarehe 11 Desemba 1225 alitangazwa na Pa ...

Ubaldo wa Gubbio

Ubaldo wa Gubbio alikuwa askofu wa mji huo baada ya kuishi kama kanoni na kama mmonaki. Anaheshimiwa na Wakatoliki kama mtakatifu hasa baada ya kutangazwa na Papa Selestini III tarehe 4 Machi 1192. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 16 Mei.

Ubertino wa Casale

Ubertino wa Casale alikuwa Mfransisko wa Italia maarufu kama kiongozi mmojawapo wa Ndugu wa Kiroho, ambao walishika msimamo mkali katika utawa wa Ndugu Wadogo.

Ulrich wa Augsburg

Ulrich wa Augsburg alikuwa askofu wa mji huo tangu tarehe 28 Desemba 923 hadi alipofariki miaka 50 baadaye. Alikuwa maarufu kwa matendo ya toba na ukarimu. Ndiye Mkristo wa kwanza kutangazwa mtakatifu na Papa mwenyewe Papa Yohane XV, 4 Julai 993. ...

Umile wa Bisignano

Umile wa Bisignano, alikuwa bradha mnyenyekevu ajabu wa shirika la Ndugu Wadogo Wareformati. Jina la awali lilikuwa Luca Antonio Pirozzo. Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu. Alitangazwa kwanza mwenye heri na Papa Leo XIII tarehe 29 Ja ...

Urbani wa Jerba

Urbani wa Jerba alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki katika mji wa Jerba. Alipelekwa uhamishoni katika dhuluma ya Genseriki, mfalme wa Wavandali. Habari zake zimeandikwa na askofu Vikta wa Vita. Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu. Sikukuu yake h ...

Urbani, Theodori na wenzao

Urbani, Theodori na wenzao 78, akiwemo Menedemo, walikuwa Wakristo wa Dola la Roma, wakleri kwa walei, waliofia imani sahihi wakati wa kaisari Valens aliyefuata Uario. Walipandishwa juu ya boti ambalo lilichomwa moto kayi ya bahari. Tangu kale wa ...

Ursino wa Bourges

Ursino wa Bourges alikuwa askofu wa kwanza wa mji huo. Gregori wa Tours alisimulia habari zake kwa kuzichanganya na hadithi zisizoaminika kihistoria. Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yak ...

Valeri wa Trier

Valeri wa Trier alikuwa askofu wa pili wa mji huo. Tangu zamani anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini. Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 29 Januari au 11 Septemba.

Valeriano wa Avensano

Valeriano wa Avensano alikuwa askofu wa Avensa, leo Bordj-Hamdouna, Tunisia, katika karne V, ambaye pamoja na maaskofu wenzake 8 alifukuzwa na mfalme Genseriko wa Wavandali kwa amri ya kwamba mtu yeyote asimkaribishe nyumbani wala shambani. Kwa h ...

Batista Varano

Batista Varano, O.S.C. alikuwa mtoto wa mtawala wa Camerino aliyejitunza bikira na kuwa mfuasi wa Fransisko wa Asizi katika Utawa wa Mtakatifu Klara. Ni maarufu hasa kwa vipaji vyake katika sala, alipozama katika mateso ya kiroho ya Yesu. Alitang ...

Venansi wa Tours

Venansi wa Tours alikuwa abati wa monasteri ya huko. Kwanza aliwahi kuoa bado kijana, lakini alipotembelea wamonaki alivutiwa na maisha yao akakubaliwa na mke wake ajiunge nao. Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiorthodoksi ...

Vendelini wa Trier

Vendelini wa Trier alikuwa mkaapweke katika jimbo la Trier kuanzia mwaka 561 au 565 hadi kifo chake. Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 21 Oktoba.

Veneri mkaapweke

Veneri alikuwa mmonaki padri, halafu mkaapweke karibu na La Spezia, na ndipo alipofariki, baada ya kuleta Waario wengi katika Kanisa Katoliki. Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa ta ...

Veneri wa Milano

Veneri wa Milano alikuwa Askofu wa mji huo tangu mwaka 400 hadi kifo chake. Alipokuwa shemasi wa Ambrosi wa Milano, alihudhuria kifo chake. Kama askofu alituma wakleri kusaidia Kanisa la Afrika Kaskazini, mmojawao akiwa mwanahistoria Paulino Shem ...

Verano wa Cavaillon

Verano wa Cavaillon alikuwa askofu wa mji huo maarufu kwa maadili yake, hasa huruma kwa wagonjwa. Gregori wa Tours alisimulia baadhi ya miujiza yake. Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kati ya watakatifu. Sikukuu yake huadhimis ...

Verano wa Vence

Verano wa Vence alikuwa askofu wa 4 wa mji huo wa Gaul. Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 11 Novemba.

Verena wa Zurzach

Verena wa Zurzach alikuwa msichana aliyelelewa Kikristo na familia yake na hatimaye alibatizwa. Alifuatana na ndugu yake askari wa Kikosi cha Thebe hadi Uswisi alipoishi kwanza kama mkaapweke halafu akawa anasaidia wengi. Tangu kale anaheshimiwa ...

Veronika Giuliani

Veronika Giuliani alikuwa mmonaki wa urekebisho wa Wakapuchini wa Utawa wa Mt. Klara. Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu bikira. Ingawa aliheshimiwa hivyo mara baada ya kufa, kesi ya kumtangaza rasmi ilicheleweshwa na uchunguzi wa maa ...

Veruli, Sekundini, Sirisi, Felisi, Servuli, Saturnini na Fortunati

Veruli, Sekundini, Sirisi, Felisi, Servuli, Saturnini na Fortunati na wenzao kumi na tisa ni kati ya Wakristo wa Afrika Kaskazini waliouawa na Wavandali Waario kwa ajili ya imani yao ya Kikatoliki. Kwa kuwa hayajulikani mengine kuhusu historia ya ...

Yohane Maria Vianney

Yohane Baptista Maria Vianney, alikuwa padri mwanajimbo wa Kanisa Katoliki kutoka Ufaransa; kwa miaka mingi alifanya kazi ya uchungaji kama paroko wa kijiji cha Ars, huku sifa zake zikivuta watu kutoka nchi za nje ya Ulaya pia. Alitangazwa na Pap ...

Viatori wa Lyon

Viatori wa Lyon alikuwa Mkristo wa mji huo, leo nchini Ufaransa, ambaye miaka yake ya mwisho alimfuata askofu wake Yusto wa Lyon kwenda kuishi jangwani na wamonaki wa Misri. Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Si ...

Viche wa Sabrata

Viche wa Sabrata alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki katika mji wa Sabrata. Alipelekwa uhamishoni katika dhuluma ya Genseriki, mfalme wa Wavandali. Habari zake zimeandikwa na askofu Vikta wa Vita. Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu. Sikukuu yak ...

Vikta mkaapweke

Vikta mkaapweke alikuwa mkaapweke aliyesifiwa na Bernardo wa Clairvaux. Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 26 Februari.

Vikta wa Le Mans

Vikta wa Le Mans alikuwa askofu wa mji huo kuanzia mwaka 450. Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 1 Septemba.

Viktori wa Vita

Viktori wa Vita ni kati ya wafiadini wa Kanisa Katoliki waliouawa kikatili sana na Wavandali katika karne ya 5, wakati wa utawala wa mfalme Huneriki aliyekuwa Mwario. Habari zao zimeandikwa na askofu Vikta wa Vita. Tangu kale anaheshimiwa kama mt ...

Viktoryo wa Utica

Viktoryo wa Utica alikuwa askofu wa mji huo wa kale katika karne ya 4 BK. Alishiriki mtaguso wa Arles wa mwaka 314. Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 23 Agosti.

Vinsenti Romano

Vinsenti Romano, alikuwa padri mwanajimbo wa Kanisa Katoliki aliyefanya uchungaji kama paroko, akiwajibika sana katika malezi ya watoto na huduma kwa wafanyakazi na wavuvi. Papa Paulo VI alimtangaza mwenye heri tarehe 17 Novemba 1963, halafu tare ...

Vladimir Mkuu

Vladimir Mkuu alikuwa mtemi wa Kiev na Novgorod kuanzia mwaka 980 hadi kifo chake. Mwaka 988 alipokea ubatizo kutoka kwa mapadre wa Kanisa la Bizanti uliofuatwa na ubatizo wa familia na wananchi wa Kiev). Tukio hilo liliathiri moja kwa moja utama ...

Volusiano wa Tours

Volusiano wa Tours alikuwa askofu wa mji huo kuanzia mwaka 491, lakini alipelekwa uhamishoni na Wavisigothi. Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake ni tarehe 18 Januari.

Wafiadini wa Aquae Regiae

Wafiadini wa Aquae Regiae walikuwa Wakristo wa Kanisa Katoliki ambao waliuawa na Wavandali Waario chini ya mfalme Genseriki kwa ajili ya imani yao wakiwa kanisani kuadhimisha Pasaka katika mji huo. Tangu kale wanaheshimiwa kama watakatifu wafiadi ...

Wafiadini wa Gorkum

Wafiadini wa Gorkum (walifariki Brielle, Uholanzi, 9 Julai 1572, ni Wakristo 19 wanaoheshimiwa na Kanisa Katoliki kama watakatifu wafiadini kwa kuwa waliuawa na Waprotestanti kwa kukataa kujiunga nao na kujitenga na Papa. Baadhi yao ni: Antoni wa ...

Wafiadini wa Ijumaa Kuu wa Aleksandria

Wafiadini wa Ijumaa Kuu wa Aleksandria walikuwa Wakristo wa Aleksandria ambao waliuawa makanisani siku ya Ijumaa Kuu wakati wa dhuluma ya kaisari Kostansi kwa kushikilia imani sahihi na kukataa Uario. Wanaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodo ...

Wafiadini wa imani sahihi wa Afrika (12 Oktoba)

Wafiadini wa imani sahihi wa Afrika ni Wakristo 4.996 waliofia imani ya Kanisa Katoliki mahali mbalimbali pa Afrika Kaskazini mwaka 483 kwa agizo la mfalme wa Wavandali Huneriki aliyekuwa Mwario. Tangu kale wanaheshimiwa kama watakatifu wafiadini ...

Wafiadini wa imani sahihi wa Aleksandria (13 Mei)

Wafiadini wa imani sahihi wa Aleksandria walikuwa Wakatoliki wengi wa mji huo wa Misri, ambao walifia imani sahihi katika kanisa la Theonas wakati wa dhuluma ya Waario dhidi yao chini ya Kaisari Valens. Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na W ...

Wafiadini wa imani sahihi wa Aleksandria (356)

Wafiadini wa imani sahihi wa Aleksandria walikuwa Wakristo wengi wa Misri, ambao walifia imani sahihi kanisani wakati wa liturujia kutokana na dhuluma ya Waario dhidi yao. Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu waf ...

Wafiadini wa imani sahihi wa Aleksandria (9 Februari)

Wafiadini wa imani sahihi wa Aleksandria walikuwa Wakristo wengi wa Misri, ambao walifia imani sahihi wakati wa ibada kutokana na dhuluma ya Waario dhidi yao. Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini. Sikuk ...

Wafiadini wa imani sahihi wa Misri (21 Mei)

Wafiadini wa imani sahihi wa Misri walikuwa Wakatoliki wengi wa mji huo wa Misri, ambao walifia imani sahihi wakati wa dhuluma ya Waario dhidi yao na wengine chini ya Kaisari Juliani Mwasi. Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi k ...

Wafiadini wa Mlango wa Shaba

Wafiadini wa Mlango wa Shaba walikuwa Wakristo waliouawa na kaisari Leo III wa Bizanti kwa sababu ya kuheshimu picha takatifu na kutaka kuzuia isivunjwe ile ya Mwokozi kwenye Mlango wa Shaba. Walikuwa wengi, lakini kati yao wanatajwa kwa jina Jul ...

Wafiadini wa Pentekoste wa Aleksandria

Wafiadini wa Pentekoste wa Aleksandria walikuwa Wakristo Wakatoliki wa mji huo wa Misri ambao waliuawa kwenye Pentekoste kwa amri ya askofu Mwario Joji chini ya kaisari Konstanti II. Tangu kale wanaheshimiwa kama watakatifu wafiadini. Sikukuu yao ...

Wafiadini Waabrahamu

Wafiadini Waabrahamu ni kundi la wamonaki wa mji huo ambao waliuawa wakati wa dhuluma ya kaisari Teofilo wa Bizanti kwa sababu ya kuheshimu picha takatifu. Wanaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini. Sikukuu yao in ...

Yohane Wall

John Wall, O.F.M., alikuwa padri wa shirika la Ndugu Wadogo Warekoleti aliyefia dini ya Ukristo huko Uingereza, alipouawa kwa kunyongwa na kuchanwa utumbo baada ya kukamatwa wakati wa kuadhimisha Misa kwa siri kutokana na dhuluma ya mfalme Charle ...

Wamonaki wafiadini wa Konstantinopoli

Wamonaki wafiadini wa Konstantinopoli walikuwa wamonaki waliouawa kwa kuwasilisha barua ya Papa Felix III ya kutetea imani sahihi dhidi ya Patriarki Acacius. Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki kama watakatifu wafiadini. Sikukuu yao huadhimish ...

Wiliamu wa Bourges

Wiliamu wa Bourges alikuwa padri ambaye alijiunga na umonaki wa Citeaux na baadaye alipata kuwa askofu mkuu wa Bourges kuanzia mwaka 1200 hadi kifo chake. Alijulikana kwa kuwa na maisha magumu, kwa kuheshimu sana Ekaristi na kwa kuongoa wakosefu ...