ⓘ Free online encyclopedia. Did you know? page 82

Rangi za Umoja wa Kiafrika

Kuna aina mbii za bendera zinazotumiwa kuonyesha Umoja wa Kiafrika au umoja wa watu wenye asili ya Afrika. Zote mbili ni tofauti na bendera rasmi ya Umoja wa Afrika, ambao ni maungano ya nchi 55 za Afrika na kutumia kijani pekee. Aina moja inafua ...

Aktiki

Aktiki ni sehemu ya kaskazini kabisa ya dunia yetu, ikijumlisha nchi na bahari inayozunguka ncha ya kaskazini. Sehemu za kaskazini za Urusi, Alaska, Kanada, Greenland, Skandinavia pamoja na bahari ya Aktiki huhesabiwa katika Aktiki. Zote huwa na ...

Kisiwa cha Dubu

Kisiwa cha Dubu ni kisiwa kwenye mpaka wa magharibi ya Bahari ya Barents; au kwa lugha nyingine kiko takriban kwenye mpaka baina ya Bahari ya Aktiki na Atlantiki ya Kaskazini. Hutazamwa kama kisiwa cha kusini kabisa cha funguvisiwa la Svalbard ha ...

Novaya Zemlya

Novaya Zemlya ni funguvisiwa la Urusi lililopo kwenye Bahari Aktiki. Eneo lake ni kilomita za mraba 90.650. Kiutawala ni Wilaya ya Novaya Zemlya katika mkoa wa Arkhangelsk Oblast. Mwaka 2010 ilikuwa na wakazi 2.429 na kati yao karibu 2.000 waliis ...

Spitsbergen

Spitsbergen ni kisiwa kikubwa cha funguvisiwa la Svalbard linaloitwa mara nyingi kwa jina la Spitsbergen vilevile kwa jumla. Kiko ndani ya Bahari ya Aktiki na eneo lake ni km² 39.044. Funguvisiwa lote ni sehemu ya ufalme wa Norwei. Mwinuko mkuu n ...

Svalbard

Svalbard ni jina la funguvisiwa la Norwei katika Bahari ya Aktika, linalojulikana pia kama funguvisiwa la Spitsbergen. Iko kati ya Norwei na ncha ya kaskazini ya dunia. Kuna wakazi 2.756 kwenye visiwa vitatu vya Spitsbergen, Bjornoya Kisiwa cha D ...

Amerika ya Kilatini

Amerika ya Kilatini humaanisha kwa kawaida nchi za Amerika ambako lugha za Kihispania na Kireno pamoja na Kifaransa hutumiwa kama lugha rasmi au lugha ya watu wengi. Lugha hizi zote zimetokana na Kilatini na hujumlishwa kama "Lugha za Kirumi".

Bolivia

Bolivia jina linatokana na shujaa Simon Bolivar ni nchi isiyo na mwambao wa bahari katika Amerika Kusini. Imepakana na Brazil, Paraguay, Argentina, Chile na Peru.

Chile

Chile ni nchi ya Amerika Kusini. Eneo lake ni kama kanda ndefu nyembamba kati ya safu za milima ya Andes na Bahari ya Pasifiki. Imepakana na Peru, Bolivia na Argentina. Ni sehemu za Chile pia maeneo ya Kisiwa cha Pasaka Rapa Nui, Kisiwa cha Salas ...

Asia ya Kusini

Asia ya Kusini ni sehemu ya Asia yenye nchi zifuatazo: Bhutan Nepal Pakistan Bangladesh Uhindi halafu nchi za visiwani Maldivi Sri Lanka Umoja wa Mataifa umehesabu pia Afghanistan na Uajemi katika kanda hili.

Asia

Asia ni bara kubwa kabisa kuliko mabara yote mengine ya dunia. Bara hili lina eneo la kilomita za mraba 44.579.000, ambalo ni sawa na asilimia 30% ya ardhi yote. Wakazi wa bara la Asia ni 3.701.000.000 kwa mujibu wa makisio 2003. Bara la Asia lin ...

Asia Ndogo

Asia Ndogo ni namna ya kutaja eneo la Anatolia ambalo ni sehemu ya Kiasia ya Uturuki. Ni hasa eneo la rasi kati ya Bahari Nyeusi na Mediteranea. Asia Ndogo Kilatini: Asia Minor ni jina la kihistoria la eneo hili. Wakati mwingine kisiwa cha Kipro ...

Asia ya Magharibi

Asia ya Magharibi ni sehemu ya magharibi-kusini ya bara la Asia. Inatajwa kati ya kanda za dunia ya UM.

Bara Arabu

Bara Arabu ni ile sehemu ya dunia iliyoko baina ya Bara la Afrika na Bara la Asia ambayo sehemu kubwa yake imezungukwa na bahari, upande wa magharibi Bahari ya Shamu, upande wa kusini na Bahari ya Hindi na ule wa Mashariki Ghuba ya Uajemi. Sehemu ...

Indochina

Indochina ni jina la kijiografia linalojumlisha maeneo ya kibara ya Asia ya Kusini-Mashariki upande wa kusini ya China na upande wa mashariki ya Uhindi. Kihistoria ilitaja koloni ya Indochina ya Kifaransa iliyojumlisha maeneo ya nchi za Vietnam L ...

Siberia

Siberia ni eneo kubwa mashariki mwa Urusi. Ni zaidi ya nusu ya eneo la Urusi wote. Eneo lake lote ni kilomita za mraba milioni 9.6 ambayo ni karibu sawa na Ulaya yote.

Atlantiki

Atlantiki ni bahari kubwa inayotenganisha Amerika upande wa magharibi na Afrika na Ulaya upande wa mashariki. Eneo lake ni kilometa za mraba 106.200.000 au sehemu ya tano ya uso wa dunia pamoja na bahari za pembeni kama bahari ya Baltiki na Medit ...

Bahari kuu

Bahari Kuu ni jina linalotumika kutaja jumla ya maeneo makubwa ya maji ya chumvi duniani yanayopakana na kufuatana kama gimba moja. Kwa maana hii bahari kuu inafunika zaidi ya theluthi mbili za uso wa dunia. Bahari Kuu imegawiwa na ardhi ya mabar ...

Bahari ya Kaspi

Bahari ya Kaspi ni ziwa kubwa kabisa duniani lenye eneo la km² 371.000 na mjao wa km³ 78.200. Liko kati ya Azerbaijan, Urusi, Kazakhstan, Turkmenistan na Uajemi. Kimo chake kinafikia mita 1.025. Huitwa "bahari" kwa sababu maji yake ni ya chumvi i ...

Bahari ya Kusini ya China

Bahari ya Kusini ya China ni bahari ya kando ya Pasifiki mbele ya pwani la kusini ya China. Imepanuka kati ya Taiwan upande wa kaskazini na Singapur upande wa kusini. Upande wa mashariki hupakanwa na visiwa vya Indonesia na Ufilipino, upande wa m ...

Bahari ya Ross

Bahari ya Ross iligunduliwa na nahodha Mwingereza James Ross mnamo 1841. Magharibi mwa Bahari ya Ross kipo Kisiwa cha Ross. Mashariki kiko Kisiwa cha Roosevelt. Sehemu ya kusini imefunikwa na barafu. Katika magharibi mwa bahari ya Ross kuna banda ...

Bahari ya Scotia

Bahari ya Scotia ni eneo la bahari kati ya Antaktiki na Amerika Kusini pale ambako Bahari ya Kusini na Atlantiki Kusini zinakutana. Eneo la Bahari ya Scotia ni takribani kilomita za mraba 900.000. Mipaka yake ni Mapito ya Drake upande wa magharib ...

Maji kujaa na kupwa

Maji kujaa na kupwa ni mabadiliko ya uwiano wa bahari unaopanda na kushuka kila siku. "Maji kujaa" ni hali ya juu na "maji kupwa" ni hali ya chini ya maji ya bahari. Tofauti kati ya hali hizi inaweza kufikia hadi mita kadhaa. Mabadiliko ya maji k ...

Mkondo wa bahari

Mkondo wa bahari ni mwendo mfululizo wa maji ndani ya bahari. Ni kama mto ndani ya bahari. Maji ya mkondo huwa na halijoto tofauti na maji ya mazingira. Kwa kawaida huwa mikondo ya bahari yahusu maji karibu na uso wa bahari. Kwa hiyo kama mto wa ...

Nyasi-bahari

Nyasi-bahari ni mimea ya baharini ya familia 4 za oda Alismatales: Cymodoceaceae, Hydrocharitaceae, Posidoniaceae na Zosteraceae, inayofanana na nyasi za kweli.

Bara la Antaktiki

Antaktiki ni bara lililopo kwenye ncha ya kusini ya dunia, kati ya bahari za Pasifiki, Atlantiki na Bahari Hindi. Jina "Antaktiki" linatokana na lugha ya Kigiriki likimaanisha "kinyume cha Aktiki", ambapo Aktiki ni eneo karibu na ncha ya kaskazin ...

Ulaya

Ulaya asili ya jina ni neno la Kiarabu ولاية, wilaayatun ; inaitwa pia Uropa ni bara lenye eneo la km² 10.600.000 tu, lakini wakazi ni milioni 700. Wengi wenye asili ya Ulaya wakati wa ukoloni walitawanyika duniani, hasa Amerika, wakiathiri kote ...

Jiji

Kimataifa kulikuwa na makubaliano kwenye mkutano wa kimataifa wa takwimu ya mwaka 1887 ya kuhesabu kila mji wenye wakazi zaidi ya 100.000 kama "mji mkubwa", miji kati ya wakazi 20.000 na 100.000 kama miji ya wastani na ile kati ya wakazi 5.000 na ...

Bamba la Antaktiki

Bamba la Antaktiki ni bamba la gandunia linalobeba bara la Antaktiki na sehemu za sakafu ya bahari jirani. Bamba hilo huwa na eneo la Km² 60.900.000. Mabamba yanayopakana ni Bamba la Nazca, Bamba la Amerika ya Kusini, Bamba la Afrika, Bamba la Au ...

Bamba la Cocos

Bamba la Cocos ni bamba la gandunia katika Pasifiki ya mashariki lililopo mbele ya pwani ya Amerika ya Kati. Jina lake limetokana na Kisiwa cha Cocos.

Bamba la Nazca

Bamba la Nazca ni moja kati ya mabamba ya gandunia yaani mapande ya miamba yanayounda ganda la Dunia. Bamba hilo limepokea jina lake kutokana na mji wa bandari wa Peru wa Nazca. Bamba la Nazca liko mbele ya pwani la magharibi la Amerika Kusini. N ...

Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki

Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki ni maumbile ya kijiolojia inayoanza katika Mashariki ya Kati na kuendelea hadi Msumbiji. Ni kati ya maajabu makubwa ya dunia hii. Ufa hii imetokea tangu miaka milioni 35 kutokana na mwendo wa mabamba ya ganduni ...

Ghuba ya Carpentaria

Ghuba ya Carpentaria ni sehemu ya bahari kwenye kaskazini ya Australia. Pande za kusini, magharibi na mashariki iko Australia bara, upande wa kaskazini iko Bahari iliyopo baina ya Australia na Guinea Mpya. Kwenye kinywa chake, ghuba ina upana wa ...

Ghuba ya Hudson

Ghuba ya Hudson ni ghuba kubwa ya Bahari Atlantiki ndani ya ardhi ya Kanada mashariki. Eneo lake ni 819.000 km². Ina umbo kama ziwa la ndani ya nchi kavu ikiunganishwa na bahari ya Labrador kwa njia nyembamba ya mlango wa Hudson yenye upana wa ki ...

Ghuba ya Uthai

Ghuba ya Uthai imepakana na nchi za Kambodia, Uthail na Vietnam. Ncha ya kaskazini ya ghuba hiyo ni Hori ya Bangkok kwenye mdomo wa Mto Chao Phraya. Eneo la maji ni karibu km² 320.000. Mpaka wa ghuba hufafanuliwa na mstari kutoka Rasi Bai Bung ku ...

Jangwa Kubwa la Victoria

Jangwa Kubwa la Victoria ni jangwa kubwa zaidi nchini Australia. Linaenea kwa km² 348.750 katika kusini magharibi ya bara hili. Uso wake ni mchanganyiko wa matuta ya mchanga, vilima vidogo, tambarare za nyasi, maeneo makubwa ya changarawe, na maz ...

Mbuga ya Patagonia

Mbuga ya Patagonia ni eneo kubwa lenye tabianchi yabisi yaani kavu likiwa na kilometa za mraba 673.000. Linapatikana katika Patagonia ambayo ni sehemu ya kusini ya Argentina. Upande wa magharibi unapakana na milima ya Andes na upande wa mashariki ...

Jiolojia

Jiolojia ni fani ya sayansi inayochunguza maumbile ya dunia na tabia zake za kifizikia na kikemia. Inachungulia pia historia ya dunia na nguvu zinazoendelea kubadilisha maumbile ya dunia. Neno "geologia" liliwahi kutumiwa mara ya kwanza mnamo 177 ...

Changarawe

Changarawe ni mawe madogo. Kama ukubwa wa kila kijiwe ni chini ya 2 mm ndipo mchanga. Kama ni kubwa zaidi kuliko 60-75 mm si changarawe tena ni jiwe. Changarawe imetokea kutokana na mmomonyoko wa mawe au mwamba. Idadi kubwa ya changarawe hutokana ...

Makaa mawe

kwa makaa yanayotengenezwa kutokana na kuni tazama makaa Makaa mawe ni aina ya mwamba mashapo au mwamba metamofia na fueli kisukuu muhimu. Ilitokea kutokana na mabaki ya mimea ya kale iliyogeuzwa kuwa aina ya mwamba katika mchakato wa miaka mamil ...

Kimbunga Irma

Kimbunga Irma ni kimbunga kikali mno kilichotokea juu ya Bahari ya Atlantiki mwezi Septemba 2017. Kinadaiwa kuwa ndicho kimbunga kikali zaidi kuwahi kutokea katika eneo la Bahari ya Atlantiki kwa miongo kadhaa iliyopita. Kimbunga Irma kinatajwa k ...

El Ninyo

El Ninyo, pia El Nino ni tukio la halihewa linalotokea kwenye nusutufe ya kusini ya dunia kila baada ya miaka kadhaa. Dalili za El Ninyo ni kuongezeka kwa mvua kushinda hali ya kawaida. El Ninyo ni tukio la eneo la Bahari Pasifiki lakini athari z ...

Kituo cha metorolojia

Kituo cha metorolojia ni mahali ambako hali ya hewa inachunguliwa kwa njia ya upimaji wa mfululizo na kutunza vipimo hivyo kwa muda mrefu. Data kutoka vituo hivyo ni msingi wa kujenga metorolojia ambayo ni tawi la sayansi kuhusu angahewa, tabianc ...

Monsuni

Monsuni ni upepo wa majira unaoendelea kwa muda wa miezi kadhaa kuelekea upande mmoja na kubadilika baada ya kipindi hiki kuelekea kinyume. Neno hili lilitumiwa mara ya kwanza katika eneo la Bahari Hindi ambako inajirudiarudia kwa nguvu hasa. Ina ...

Tabianchi

Tabianchi inamaanisha jumla ya halijoto, unyevuanga, kanieneo ya angahewa, upepo, usimbishaji na tabia nyingine zinazoathiri hali ya hewa katika sehemu fulani ya uso wa dunia kwa muda mrefu. Tabianchi ni tofauti na halihewa ikitazama vipindi vire ...

Theluji

Theluji ni aina ya pekee ya barafu ya maji. Inapatikana kama usimbishaji unaotelemka kwa maumbile ya barafu ya fuwelia. Fuwele za theluji ni ndogo; muundo wa fuwele unaonekana kwa macho matupu kama fuwele ni kubwa. Vipande vyake ni vyembamba sana ...

Wingu

Asili yake ni mvuke wa maji unaotokea wakati jua linabadilisha maji kuwa gesi ya H²O; mvuke unapanda juu kwa sababu ni nyepesi kuliko hewa. Baada ya kupanda kiasi cha kutosha hufikia umbali penye baridi na mvuke unatonesha kuwa matone madogo ya m ...

Dola-mji

Dola-mji ni dola ambalo eneo lake ni mji mmoja pekee. Katika historia kuna mifano mingi ya dola-miji. Mwaka 2015 kulikuwa bado na miji mitatu duniani ambayo ni dola-miji ya kujitegemea kabisa. Pamoja nayo kuna pia madola au majimbo ndani ya nchi ...

Mji mkuu

Mji mkuu kwa kawaida ni mji wenye makao makuu ya serikali ya nchi fulani. Katika nchi nyingi mji huo ni pia mji mkubwa na muhimu zaidi kushinda miji mingine nchini. Huo ni sehemu yenye maendeleo makubwa sana katika nchi yoyote: ina kila huduma mu ...

Kilima

Kilima ni mwinuko wa ardhi ambao uko juu kuliko eneo linalouzunguka lakini ni mdogo kuliko ule wa mlima. Vilima ni miinuko ya chini kuliko milima. Kwa lugha nyingine ni mlima mdogo, kama Kiswahili kinavyoonyesha wazi. Uso wa kilima ni imara kulik ...