ⓘ Évariste Ndayishimiye

                                     

ⓘ Évariste Ndayishimiye

Evariste Ndayishimiye ni askari mwanasiasa ambaye amekuwa Rais wa Burundi tarehe 18 Juni2020 baada ya kifo cha Pierre Nkurunziza tarehe 8 Juni 2020.

                                     

1. Maisha

Alizaliwa katika familia ya Wahutu nchini Burundi. Wakati wa kuanzishwa kwa vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Burundi alikuwa mwanafunzi wa sheria kwenye chuo kikuu cha Burundi. Baada ya mashambulio dhidi ya wanafunzi Wahutu alijiunga na chama cha CNDD–FDD akaendelea kuwa kiongozi wa tawi lake la wanamgambo. Baada ya mapatano ya kumaliza vita alikuwa makamu wa mkuu wa jeshi la kitaifa.

Baada ya uchaguzi wa kiongozi wa CNDD-FDD Pierre Nkurunziza kuwa rais, Ndayishimiye alikuwa waziri wa mambo ya ndani hadi mwaka 2007 na baadaye mwangalizi wa jeshi lote hadi 2014.

Mwaka 2016 alikuwa katibu mkuu wa chama cha CNDD-FDD. Nkurunziza alipokubali kutogombea tena urais alimkubali Ndayishimiye kuwa mgombea wa chama kama rais.

Katika uchaguzi wa mwaka 2020 Ndayishimiye alishinda kwa kupata asilimia 68 za kura zote. Nkurunziza aliaga dunia ghafla tarehe 8 Juni 2020 mara baada ya uchaguzi. Mahakama Kuu ya Burundi ilikubali kuwahishwa kwa kuapishwa kwa rais mpya na tarehe 18 Juni Ndayishimiye alikula kiapo cha kuhudumia kama rais wa taifa.

Anaishi katika ndoa na Angeline Ndayubaha. Anajulikana kama Mkristo mwaminifu wa Kanisa Katoliki.

                                     
  • mara ya pili 30 Aprili 2003 26 Agosti 2005 Domitien Ndayizeye 26 Agosti 2005 8 Juni 2020 Pierre Nkurunziza 18 Juni 2020 Évariste Ndayishimiye
  • Kirundi, Kiswahili Mji Mkuu Gitega au Bujumbura Serikali Jamhuri Rais Évariste Ndayishimiye Eneo km² 27, 834 Eneo la Rwanda Kazembe km² 123.553 Idadi ya wakazi