ⓘ Zikhona Sodlaka

                                     

ⓘ Zikhona Sodlaka

Zikhona Sodlaka ni mwigizaji wa Afrika Kusini anayejulikana zaidi kwa majukumu yake ya kuigiza katika safu ya runinga kama vile Shooting Stars, Rhythm City, Soul City, Intsika na Montana.

Sodlaka aliwahi kuteuliwa kwenye Tuzo za Filamu na Televisheni za Afrika Kusini SAFTA.

Yeye ni mwigizaji mashuhuri wa Afrika Kusini katika Tsha Tsha, Igazi, Generations safu ya Runinga ya Afrika Kusini.na filamu ya The Two of Us ya mwaka 2015 na Mandela: Long Walk to Freedom.

                                     

1. Maisha ya awali

Sodlaka alizaliwa Mthatha huko Eastern Cape, alikulia KwaZulu-Natal. Alisoma katika shule ya Excelsior SSS na aliacha akiwa darasa la 9. Alipata elimu yake yote katika shule ya Warriors Rust.

Alipata elimu ya juu katika chuo cha Shepstone ambapo alisomea Usimamizi wa Biashara. Alipata Astashada yake na kwenda Johannesburg na kusajiliwa katika Teknolojia ya Habari kama Mwanafunzi na alifanya Programu ya Kompyuta huko Havtec kabla ya kujikita kwenye sanaa.