ⓘ James Watt

                                     

ⓘ James Watt

James Watt alikuwa mhandisi kutoka Uskoti. Amekuwa maarufu kwa kuboresha injini ya mvuke kufikia kiwango kilichowezesha matumizi ya mashine hii kwa viwanda. Kwa njia hiyo alikuwa katiy a watu waliweka msingi kwa mapinduzi ya viwanda wa karne ya 18 na karne ya 19.

                                     

1. Mafunzo yake

Alizaliwa Uskoti katika familia ya kipresbiteri kama mtoto wa mjenzi wa meli. Shuleni alipenda hisabati na kusoma mengi lakini lugha na historia aliacha kando. Angependa kuwa daktari lakini wazazi walishindwa kumgharamia masomo ya chhuoni. Alipofikia umri wa miaka 17 aliingia katika mafunzo ya fundi makanika huko London. Aliamwacha fundi mwalimu alipoona hajifunzi kitu kipya tena bila kusubiri kutimiza miaka saba ya kawaida na kwa sababu hiyo hakutambuliwa kama fundi kamili.

                                     

2. Fundi wa Chuo Kikuu cha Glasgow

Watt alibahatika alipopata kazi ya fundi kwa vifaa vya upimaji kwenye chuo kikuu cha Glasgow. Alipendwa na walimu na wanafunzi waliokutana katika karakana ndogo ya Watt kwa majadiliano. Profesa wa fizikia Joseph Black na mwanauchumi Adam Smith wakawa marafiki zake.

Mwaka 1760 Watt alimwoa Margaret Miller. Kati ya watoto wao ni mwanawe James pekee aliyeishi kufikia umri mkubwa.

                                     

3. Kukutana na injini ya mvuke

Mwaka 1764 rafiki mwingine Profesa John Robison alimwonyesha injini ya mvuke. Watt alianza kusoma yote juu ya teknolojia hii yaliyopatikana kwake. Chuo kikuu kilikuwa na injini moja iliyoharibika na Watt alipewa kazi ya kuitengeneza. Alifaulu lakini aliona ya kwamba injini ilikuwa na tatizo la muundo wake kwa sababu kiasi kikubwa cha nishati kilipotea badala ya kufanya kazi.

                                     

4. Jitihada za kubuni injini mpya

Watt alitengeneza sampuli ndogo ya injini bora. Marafiki kwenye chuo kikuu walimsaidia kwa kumpa pesa alipotengeneza injini kubwa. Utengenezaji wa mashine hizi ulikuwa na matatizo makubwa. Wafanyakazi wa wakati ule hawakuzoea kutekjeleza shughuli kwa umakinifu uliohitajika kwa mashine hii. Mtajiri aliyomsaidia kwa pesa alishindwa kuendelea na mwenye kiwanda mwingine aliingia akiamini ubora wa muundo wa Watt.

Ilichukua miaka kadhaa na msaada wa watu mbalimbali hadi injini ya mvuke iliyoboreshwa ilikuwa tayari kwa uzalishaji na matumizi. Tangu 1785 kiwanda cha Watt na mwenzake kilianza kuleta faida ya kifedha na hali yake ya kiuchumi kilikuwa nzuri.

Watt aliendelea kutengezea aina mpya za gia kwa mashine yake iliyowezesha matumizi yake kwa shughuli nyingi. Alibuni pia kizio cha kupima nguvu akaiita "nguvu ya farasi" horsepower kinachoendelea kutumiwa duniani kama kipimo kwa nguvu ya injini hata kama kipimo kipya cha SI kinachoitwa "Watt" wati kimechukua nafasi yake kitaalamu.                                     
 • Makala hii inahusu mwaka 1736 BK Baada ya Kristo 19 Januari - James Watt mhandisi kutoka Uskoti Wikimedia Commons ina media kuhusu: 1736
 • mwaka. Mpaka uishe zinabaki siku 346 347 katika miaka mirefu 1736 - James Watt mhandisi kutoka Uskoti 1975 - Adrian Siaga, mwigizaji wa filamu kutoka
 • 1877 - 1881 7 Septemba - Thomas Hendricks, Kaimu Rais wa Marekani 1885 19 Agosti - James Watt mhandisi kutoka Uskoti Wikimedia Commons ina media kuhusu: 1819
 • kimataifa. Imepewa jina lake kwa heshima ya mwanafizikia na mhandisi James Watt 1736 - 1819 Wati moja ni sawa na volti - ampea moja 1 V A Uwezo wa
 • 1680 - Mtakatifu Yohane Eudes, padri mwanzilishi kutoka Ufaransa 1819 - James Watt mhandisi kutoka Uskoti 1994 - Linus Pauling, mshindi wa Tuzo ya Nobel
 • lakini wakati wke teknolojia haikupatikana ilikuwa mchoro tu. Wengine kama James Watt walitambua pia uwezo wa rafadha lakini hawakuitumia katika mitambo. Mwaka
 • mbalimbali zilizowahi kutumia awali nguvu ya wanadamu au ya wanyama. Mhandisi James Watt anakumbukwa kwa uboreshaji wa injini za kwanza. Injini ya mvuke ilikuwa
 • Coulomb wa Ufaransa, Alessandro Volta wa Italia, Georg Ohm wa Ujerumani na James Watt wa Uskoti. Jina la Ampere liko kati ya majina 72 yaliyoandikwa kwenye
 • na kusababisha mwendo wa injini. Injini ya mvuke jinsi ilivyobuniwa na James Watt ilitumiwa mwanzoni kabisa kuendesha pampu ya maji katika migodi ya makaa
 • Massachusetts Press. ISBN 0 - 87023 - 811 - 6Script error: No such module check isxn . Watt Ian. 1996 Myths of Modern Individualism. Cambridge: Cambridge University
 • 83 91 Watt Ian. Introduction Jane Austen: A Collection of Critical Essays. Ed. Ian Watt Englewood Cliffs, NJ: Prentice Hall, 1963. Watt Ian, ed