ⓘ Zinedine Zidane

                                     

ⓘ Zinedine Zidane

Zinedine Yazid Zidane alikuwa mchezaji wa mpira wa miguu kutoka Ufaransa na klabu ya Real Madrid aliyecheza kama kiungo mshambuliaji. Kwa sasa ni kocha wa Real Madrid.

Alicheza kama kiungo mshambuliaji kwenye timu ya taifa ya Ufaransa na Cannes, Bordeaux, Arsenal, Juventus and Real Madrid. Anajua kuchezesha, ana maamuzi ya haraka, kuumiliki mpira, mbinu.

Zidane anajulikana kama mchezaji bora kutoka Ulaya kwa miaka 50 iliyopita kwenye UEFA Golden Jubilee Poll mwaka 2004. Anatambulika kama mchezaji bora kuwahi kutokea.

Kwenye ngazi ya klabu, Zidane alishinda taji La Liga na UEFA Champions League akiwa na Real Madrid,mataji mawili ya Serie A akiwa na Juventus na kombe la mabara na UEFA Super Cup na mataji yote akishinda kwa timu zote zilizotajwa.Uhamisho wake wa 2001 kutoka Juventus kwenda Real Madrid uliweka rekodi ya dunia ya £77.5 milioni.

Mguu wake wa kushoto ulimpa ushindi wa UEFA Champions League mwaka 2002 na goli lake kuwa zuri kutokea kwenye mashindano hayo.

Kwenye ngazi ya kimataifa na Ufaransa, Zidane alibeba kombe la dunia mwaka 1998, akishinda magoli mawili na kuwa shujaa wa timu, na kwenye UEFA Euro akipewa jina la mchezaji bora wa mashindano. Kombe la dunia lilimfanya kuwa shujaa wa Ufaransa,na alipewa tuzo ya mchezaji bora wa Ufaransa Légion dhonneur mwaka 1998.

Zidane alikuwa mchezaji bora wa FIFA wa dunia wa mwaka mara tatu, 1998, 2000, 2003, alishinda tuzo ya Ballon dOr. Alikuwa mchezaji bora wa mwaka 1996, mchezaji bora wa mwaka wa Serie A 2001 na mchezaji bora wa kigeni wa La Liga mwaka 2002. Mwaka 2004 alijumuishwa kwenye FIFA 100,majina ya wachezaji bora wanaoishi wanaoonwa na Pelé. Zidane alipewa mpira wa dhahabu kwenye kombe la dunia mwaka 2006 licha ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwenye fainali dhidi ya Italia kwa kumpiga kichwa Marco Materazzi kifuani. Baada ya fainali alitangaza kustaafu.Baada ya mafanikio kwenye klabu hata kimataifa, Zidane ni mmoja kati ya wachezaji saba walioshinda Kombe la dunia, ballon d`Or na UEFA Champions League.

Baada ya kustaafu alikuwa kocha msaidizi wa Real Madrid chini ya Carlo Ancelotti msimu wa 2013-14. Baada ya kushinda UEFA Champions League na Copa del Rey, Zidane alikuwa kocha wa Real Madrid B.

Zidane alimuoa Véronique Fernández mwaka 1994. Wana watoto wanne: Enzo Alan Zidane Fernández alizaliwa tarehe 24 Machi 1995, Luca Zinedine Zidane Fernández alizaliwa 13 Mei 1998, Theo Zidane Fernández aliyezaliwa 24 Mei 2002, na Elyaz Zidane Fernández aliyezaliwa 28 Desemba 2005. Enzo anachezea timu ya Deportivo Alavés, Luca anachezea timu ya Real Madrid, na Elyaz yuko Real Madrid Academy.

                                     

1. Maisha ya mwanzo

Zinedine Zidane alizaliwa 23 Juni 1972 katika mji wa La Castellane, Marseille, kusini mwa Ufaransa. Zidane ana asili ya Algeria kutokana na uzao wake.Wazazi wake, Smaïl and Malika,walihamia mji wa Paris kutoka kijij cha Aguemoune kaskazini mwa Algeria.

Mwaka 1972, Zidane alizaliwa Marseille akiwa wa mwisho kati ya watoto watano.Baba yake alikuwa mlinzi wa usiku na mama yake akiwa mama wa nyumbani.Maisha yao yalikuwa ya hali ya kawaida kutokana na uchache wa ajira.Baba yake alikuwa mkali na mwenye malezi mazuri yaliyosaidia kwenye makuzi mazuri ya Zidane.

Uchezaji wake wa kwanza wa mpira ulianzia Castellane ambapo alianza kucheza mpira akiwa na miaka mitano.July 2011,Zidane aliwataja wachezaji wa zamani wa Marseille, Blaž Slišković, Enzo Francescoli na Jean-Pierre Papin kama ni watu aliokuwa akiiga mfano wao wakati akikuwa. Akiwa na miaka kumi, Zidane alipata kibali cha uchezaji akijiunga na timu ya mtaani kutoka Castellane inayoitwa US Saint-Henri.Baada ya kuitumikia US Saint-Henri kwa mwaka mmoja na nusu, Zidane alijiunga na SO Septèmes-les-Vallons ambapo kocha wa timu hiyo Robert Centenero alipomshawishi meneja watimu hiyo kumchukua Zidane.Zidane alikaa Septèmes mpaka alipofikia umri wa miaka 14,mpaka alipochaguliwa kwenda kwenye majaribio ya siku tatu ya CREPS Regional Centre for Sports and Physical Education huko kwenye jimbo la Aix-en,ambayo huendeshwa na shirikisho la mpira wa miguu la Ufaransa.Ni hapo ambapo Zidane alipochaguliwa na Jean Varraud mchezaji wa zamani wa AS Cannes kuitumikia timu hiyo.Akiwa na umri wa miaka 14 akiangalia kombe la dunia la mwaka1986,uwezo wa Diego Maradona uliacha alama isiyofutika kichwani pake,ambapo alipoanza kusema kuwa Maradona ni mwenye uwezo mkubwa sana.

                                     

2. Ngazi ya klabu

Cannes

Zidane alienda AS Cannes kwa muda wa wiki sita,lakini akiishiia kukaa kwenye klabu kwa miaka minne.Ambapo aliacha familia yake alikaribishwa na meneja wa Cannes,Jean-Claude Elineau alipokaa na wenzake kama familia alikuta ushindani mkubwa.

Akiwa Cannesndipo ambapo makocha walipougundua uwezo wa Zidane. Kocha wake wa kwanza, Jean Varraud,alimshauri sana asiwe na hasira bali aweze kucheza mchezo kivyake bila hasira.Zidane alitumia wiki zake za kwanza akitumikia adhabu ya kumpiga mpinzani aliyemcheka kuhusu mabweni yao.

                                     
  • Luca Zinedine Zidane Fernández alizaliwa Mei 13, 1998 ni mchezaji wa soka wa Ufaransa ambaye anacheza kama kipa wa klabu ya Real Madrid. Yeye ni mtoto
  • cha Real Madrid, alipandishwa moja kwa moja kwenye hifadhi na meneja Zinedine Zidane Tarehe 23 Septemba 2017, mkataba wa Llorente uliongezewa muda mpaka
  • Tarehe 2 Machi 2016, kutokana na kuumia kwa Karim Benzema, meneja Zinedine Zidane alimpa Borja Mayoral nafasi ya kucheza kwa mara ya kwanza katika mechi
  • tatu kwenye kinyang anyiro cha mchezaji bora wa dunia. Mwaka 2009 Zinedine Zidane na Pelè walimchagua kuwa mchezaji bora wa dunia. Gerrard alikuwa na
  • Brondby IF kama mchezaji mdogo mwenye umri wa miaka 14. Anatazama Zinedine Zidane kama mfano wake. Alipokuwa na miaka 5 tu, Hojbjerg alianza kuhudhuria
  • kama zizou mpya yaani mchezaji matata wa kitambo wa ufaransa, Zinedine Zidane baada ya kufurahisha katika klabu ya Marseille wakati wa ujana wake
  • ya nahodha Didier Deschamps na mchezaji wa FIFA wa Dunia wa ZIFA, Zinedine Zidane Ufaransa ilishinda Kombe la Dunia ya FIFA mwaka 1998. Miaka miwili
  • Cristiano Ronaldo wa Ureno Wayne Rooney Ruud Van Nistelrooy Patrick Viera Zinedine Zidane wa Ufaransa Mchezo ulipelekwa Afrika na Waingereza wakati wa ukoloni