ⓘ David Woodard

                                     

ⓘ David Woodard

David Woodard ni mwandishi Mmarekani na muongozaji. Wakati wa miaka ya 1990 alitunga neno" prequiem”, ambalo ni muunganiko kati ya maneno" preemptive” na" requiem”, ili kuelezea ushiriki wake wa Kibuddha wa kutunga nyimbo maalumu za kuchezwa wakati wa au muda kidogo kabla ya kifo cha kiumbe.

Huduma za ukumbusho wa kifo zinazopatikana Los Angeles ambapo Woodard alitumikia kama muongozaji au kiongozi wa muziki ni pamoja na sherehe ya kiraia ya mwaka 2001 katika uwanja wa ndege ambao hautumiki na sasa ni reli ya Angels Flight wakikumbuka ajali iliyosababisha kifo cha Leon Praport na kumjeruhi mjane Lola. Amefanya" prequiem” kwa Wanyama pori, kwa ajili ya California Brown Pelician katika eneo la pwani pembezoni mwa ufukwe mahali ambapo mnyama alifia.

Woodard anajulikana kwa kutengeneza chombo kinachofanana na Dreamachine, taa yenye athari za kisaikolojia, ambayo imeonyeshwa katika makumbusho ya Sanaa duniani kote. Huko Ujerumani na Nepal anajulikana kwa michango yake kwenye jarida la fasihi la Der Freund, ikiwemo machapisho yake juu ya karma kwa jamii mbalimbali za viumbe, ufahamu wa mimea na makazi ya Waparaguay Nueva Germania.

                                     

1. Nueva Germania

Mnamo mwaka 2003 Woodard aliteuliwa kuwa mjumbe wa baraza huko Juniper Hills Los Angeles Vijijini, California. Katika nafasi hii alipendekeza uhusiano na mji wa Nueva Germania, Paraguay. Ili kuendeleza mpango wake, Woodard alisafiri kuelekea eneo lililokuwa ni sehemu iliyopendwa na watu wanaokula mboga za majani tu / watetezi wa haki za wanawake na kukutana na uongozi wa manispaa. Kufuatia ziara yake ya kwanza, alichagua kuachana na mpango huo wa kutafuta uhusiano lakini katika jumuiya hiyo alipata kitu cha kujifunza kwa ajili ya machapisho ya baadae. Kitu ambacho kilimvutia ni mawazo ya kiproto-transhumanist ya waliobashiriwa kuwa waandaaji Richard Wagner na Elisabeth Förster-Nietzsche, ambaye pamoja na mume wake Bernhard Förster walianzisha na waliishi katika koloni kati ya 1886 na 1889.

Kuanzia mwaka 2004 mpaka 2006 Woodard aliongoza safari nyingi kwenda Nueva Germania, akipata msaada kutoka kwa aliyekuwa Makamu wa Raisi wa Marekani Dick Cheney. Mwaka 2011 Woodard alimpatia ruhusa mwandika riwaya wa Uswisi Christian Kracht ya kuchapisha mahusiano yao ya kawaida, mengi yakihusisha Nueva Germania, kwa matoleo mawili chini ya Chuo cha Hannover imprint Wehrhahn Verlag. Katika mabadilishano ya barua, Frankfurter Allgemeine Zeitung anasema, wamevunja mipaka iliyopo kati ya maisha na sanaa.” Der Spiegel anapendekeza kwamba toleo la kwanza, Five Years, ni" kazi iliyoandaliwa kiroho” kwa riwaya ya Kracht iliyofuata ya Imperium.

Kwa mujibu wa Andrew McCann, Woodard alijitosa kwenye" safari ya kwenda kwenye kilichobaki, mahali ambapo wakazi asili wa kwanza waliishi katika hali ngumu kimaisha” na kuendelea kwenda" kukuza zaidi mambo ya asili ya jamii, na pia kujenga nyumba ndogo kama ya Bayreuth ya opera katika eneo ambalo kwa kipindi fulani familia ya Elisabeth Förster-Nietzsche iliishi.” Katika miaka ya hivi karibuni Nueva Germania imebadilika na kuwa sehemu ya kutembelea, ikiwa na kitanda na chakula cha asubuhi na makumbusho ya kihistoria.

                                     

2. Dreamachine

Kuanzia mwaka 1989 mpaka 2007 Woodard alitengeneza mfano wa Dreamachine, mashine inayowakawaka mwanga iliyobuniwa na Brion Gysin na Ian Sommerville ambayo ina silinda iliyo wazi, iliyotengenezwa na madini ya shaba au karatasi, ikizunguka taa ya umeme - inapotazamwa na macho yaliyofungwa mashine hii inaweza kusababisha hisia za kifikra zinazoweza kufanana na kuleweshwa na madawa au kuota.

Baada ya kuchangia Dreamachine kwa William S. Burroughs katika maonyesho ya LACMA mwaka 1996 Ports of Entry, Woodard alijenga urafiki na mwandishi na kumpatia" Bohemian model” karatasi ya Dreamachini kama zawadi ya sherehe yake ya 83 kuzaliwa ambayo ndiyo ilikuwa ya mwisho. Sothebys alipiga mnada mashine halisi kwa mnunuzi binafsi mwaka 2002, na nyingine imebakia kama mkopo uliokabidhiwa kutoka kwa Burroughs katika Makumbusho ya Sanaa ya Spencer.

                                     
  • hurejea miaka 56 KK na 56 BK. 56 Minutes Dakika 56 muundo wa 2007 wa David Woodard kwa piano, violin, cello na synthesizer. Currie, N., Takemitsu and
  • Horst Störmer, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia mwaka wa 1998 1964 - David Woodard mwandishi na mwanamuziki kutoka Marekani 1520 - Raphael, msanii kutoka