ⓘ Willian

                                     

ⓘ Willian

Willian Borges da Silva ni mchezaji wa soka wa Brazil ambaye anacheza kama kiungo mshambuliaji katika klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Brazil.

Willian alianza kucheza katika timu ya Brazil mwaka 2011 na aliliwakilisha taifa lake katika Kombe la Dunia la FIFA ya 2014, Copa America ya 2015 na Copa America Centenario.

Mnamo tarehe 25 Agosti 2013, klabu ya Uingereza ya Ligi Kuu ya Chelsea ilikubali kusainiwa kwa Willian. Mpango huo ulifanyika rasmi tarehe 28 Agosti 2013 na Willian alijiunga kwa mkataba wa miaka mitano, akipokea shati namba 22 mgongoni.

Willian alianza kucheza rasmi katika klabu ya Chelsea mnamo tarehe 18 Septemba dhidi ya Basel katika Ligi ya Mabingwa. Baada ya kushinda dhidi ya Swindon Town na Steaua Bucuresti katika Kombe la Ligi ya Mabingwa,Chelsea ilicheza mechi dhidi ya Norwich City mnamo terehe 6 Oktoba na kushinda 3-1.Pia aliisaidia Chelsea kushinda 2-0 dhidi ya Liverpool.

                                     
  • Na. Nafasi Mchezaji 18 FW O. Giroud 5 MF Jorginho 22 MF Willian 23 GK Mark Schwarzer 24 DF Gary Cahill 26 DF John Terry captain 27 DF Nathan Aké 28