ⓘ Maadili

Maadili

Maadili ni mafundisho yanayotolewa katika nafasi mbalimbali, hasa katika malezi, ili kuelekeza binadamu atende namna ambayo inamjenga yeye na jamii nzima. Maadili yanayohitajiwa na watu wote kimsingi ni yaleyale, lakini mazingira yanaweza kudai yatekelezwe kwa namna tofauti kiasi. Pamoja na hayo, watu tangu zamani wametoa maadili namna maalumu kulingana na dini, utamaduni, falsafa n.k.

Maadili ya Kimungu

Katika Ukristo maadili ya Kimungu ni yale yanayotokana na Mungu na kumwezesha binadamu kuhusiana naye inavyotakiwa, yaani kwa: tumaini imani na upendo. Kwa maadili hayo, yale ya kiutu yanakuwa hai na bora, kwa mfano wa Yesu Kristo. Kadiri ya Kanisa Katoliki, tofauti na yale ya kiutu, maadili ya Kimungu hayawezi kupatikana kwa juhudi anazofanya mtu, bali kwa neema tu: yanamiminiwa rohoni, yaani katika akili na katika utashi.

Maadili bawaba

Maadili bawaba ni maadili manne ya kiutu yaliyojulikana na wanafalsafa wa Ugiriki, hasa Plato na Aristotle, kuwa ndiyo yanayotegemeza maadili mengine yote ya kiutu, kama vile bawaba zinavyotegemeza mlango uweze kufanya kazi yake vizuri. Yanaitwa pia maadili ya kiutu ya msingi au fadhila za msingi, kwa kuwa ndiyo hasa yanayomfanya mtu atende kadiri ya utu wake. Majina yake ni: busara, haki, nguvu na kiasi. Katika Ukristo yanatofautishwa na maadili ya Kimungu, yaani imani, tumaini na upendo ambayo yanatokana na Mungu na kumlenga yeye.

Maadili ya utafiti

Maadili ya utafiti yanahusu msingi wa kanuni za kimaadili kwa mada mbalimbali yanayohusiana na utafiti wa kisayansi, hivyo matumizi ya kanuni adilifu katika mada mbalimbali zinazohusu binadamu. Hizi ni pamoja na kubuni na kutekeleza utafiti juu ya binadamu na wanyama, nyanja mbalimbali za kashfa za kielimu pamoja na makosa ya kisayansi, kujulisha makosa; udhibiti wa utafiti, nk. Maadili ya utafiti yaliendelea pakubwa kama dhana katika utafiti wa tiba. Mkataba muhimu hapa ni Tamko la 1974 la Helsinki. Nurenberg Code ni mkataba wa awali, lakini bado una mipasho ya maana. Utafiti katika sayan ...

Maadili ya kiutu

Maadili ya kiutu ni yale yanayotakiwa kupatikana katika binadamu yeyote ili aweze kutenda kwa uadilifu kadiri ya utu wake unaomtofautisha na wanyama, yaani hasa akili inayomwezesha kufikiria na kuelewa maana na matokeo ya matendo yake. Kadiri ya wanafalsafa wa Ugiriki wa kale Plato na Aristotle, maadili hayo ni mengi si chini ya 40, lakini yanategemea manne maadili bawaba: busara, haki, nguvu na kiasi.

Busara

Busara ni mojawapo kati ya maadili bawaba yaliyotambulikana na wanafalsafa wa Ugiriki. Ndiyo adili linalofanya akili izingatie kwa makini hali halisi ili kutambua yaliyo mema na kuchagua njia ya kufaa kuyafikia. Aristotle alifuatwa na Thoma wa Akwino akisema busara ndiyo kanuni nyofu ya utendaji. Adili hilo halichanganyikani na woga unaomzuia mtu asitende inavyotakiwa, wala na ujanja unaotumia undumakuwili na ulaghai. Kwa Kilatini inaitwa "auriga virtutum – dreva wa maadili", kwa kuwa inatakiwa kuongoza utekelezaji wa maadili mengine yote ikiyaonyesha kanuni na kiasi. Busara ndiyo inayoong ...

                                     

ⓘ Maadili

  • Maadili ni mafundisho yanayotolewa katika nafasi mbalimbali, hasa katika malezi, ili kuelekeza binadamu atende namna ambayo inamjenga yeye na jamii nzima
  • maadili ya Kimungu ni yale yanayotokana na Mungu na kumwezesha binadamu kuhusiana naye inavyotakiwa, yaani kwa: imani tumaini na upendo. Kwa maadili hayo
  • Maadili ya utafiti yanahusu msingi wa kanuni za kimaadili kwa mada mbalimbali yanayohusiana na utafiti wa kisayansi, hivyo matumizi ya kanuni adilifu
  • Maadili bawaba ni maadili manne ya kiutu yaliyojulikana na wanafalsafa wa Ugiriki, hasa Plato na Aristotle, kuwa ndiyo yanayotegemeza maadili mengine
  • Maadili ya kiutu ni yale yanayotakiwa kupatikana katika binadamu yeyote ili aweze kutenda kwa uadilifu kadiri ya utu wake unaomtofautisha na wanyama
  • Busara ni mojawapo kati ya maadili bawaba yaliyotambulikana na wanafalsafa wa Ugiriki. Ndiyo adili linalofanya akili izingatie kwa makini hali halisi
  • wanafalsafa Plato na hasa Aristotle waliorodhesha maadili mengi yanayotegemea nne za msingi maadili bawaba busara, haki, nguvu na kiasi. Zaidi ya hayo
  • kulitekeleza k.mf. kwa njia ya usafi wa moyo na mfungo Katika Ukristo ni mojawapo kati ya maadili bawaba yanayotegemeza maadili mengine yote ya kiutu.
  • elimu jamii ni tunda la mshikamano wa watu au taasisi katika maadili ni mojawapo ya maadili bawaba katika dini ni hasa uweza wa Mungu ambao unasisitizwa
  • kutetea jambo la haki. Kuanzia Plato nguvu inatajwa kati ya maadili manne yanayoitwa maadili bawaba kwa kuwa yanategemeza maadili mengine yote ya kiutu.
                                     

Kiasi

Kiasi ni adili linaloratibu matumizi ya vitu, binadamu asije akatawaliwa na tamaa. Pamoja na falsafa, dini nyingi zinasifu adili hilo na kuhimiza kulitekeleza k.mf. kwa njia ya usafi wa moyo na mfungo. Katika Ukristo ni mojawapo kati ya maadili bawaba yanayotegemeza maadili mengine yote ya kiutu.

                                     

Nguvu (adili)

Nguvu ni adili la kiutu linalomfanya mtu awe imara na kudumu kulenga mema hata katika matatizo. Linathibitisha nia ya kushinda vishawishi na kushinda mapingamizi katika njia ya uadilifu. Linawezesha kushinda hofu hata ya kifo na kuvumilia majaribu na dhuluma. Hivyo mtu anakuwa tayari kuuawa ili kutetea jambo la haki. Kuanzia Plato nguvu inatajwa kati ya maadili manne yanayoitwa maadili bawaba kwa kuwa yanategemeza maadili mengine yote ya kiutu.

                                     

Vigano

Vigano ni hadithi fupifupi zinazosimuliwa kwa lengo la kueleza makosa au maovu ya watu fulani ili kutoa maadili mema yanayofaa kwa wanajamii. Masimulizi ya vigano mara nyingi hutumia methali kama msingi wake wa maadili. Methali hiyo ndiyo hujengewa masimulizi yanayolenga kumwonya mwanajamii anayetenda kinyume na maadili ya jamii yake. Kwa kawaida vigano hujengwa juu ya tukio kisa kimoja moja ambalo hutumiwa kuelezea maisha halisi ya jamii husika.

                                     

Fadhila

Fadhila ni kitu ambacho binadamu hulipa kwa kitu ulichomsaidia kufanya; inaweza ikawa amesaidiwa fedha au amesaidiwa kitu fulani ambacho alikuwa na shida nacho.

                                     

Heshima

Heshima ni kitu anachopewa mtu kama alama ya kuthaminiwa kwake. Kwa maana nyingine ni thamani ya utu. Heshima inadaiwa na wenye cheo na mamlaka, kuanzia wazazi kutoka kwa watoto wao. Pia heshima inatarajiwa na watu wenye sifa na maadili bora. Heshima kuu ni ile anayoistahili Mwenyezi Mungu tu na ambayo inaitwa ibada. Heshima mara nyingi inaendana na usikivu na utiifu.

                                     

Kijicho

Kijicho ni hisia au kilema kinachomfanya binadamu asikitikie mambo mema waliyonayo wengine. Kutokana nacho mtu anawatenda namna isiyopendeza na kusababisha matatizo makubwa katika maisha ya jamii. Kwa sababu hiyo katika maadili ya Kanisa Katoliki, kijicho ni kati ya vilema vikuu, yaani mizizi ya dhambi nyingine.

                                     

Majivuno

Majivuno ni tabia ya mtu kujipongeza mno kutokana na sifa alizonazo. Yanatokana na kiburi na kufikia hatua ya majigambo ya uongo ambayo ni chukizo kwa wengine. Katika maadili ni kimojawapo kati ya vilema vikuu au vichwa vya dhambi vinavyozaa dhambi nyingine nyingi. Jina la Kilatini vanitas au vanagloria linahusisha tabia hiyo na ubatili.

                                     

Moyo mkuu

Moyo mkuu ni adili linaloonyesha ukuu wa mitazamo na miguso ya mtu. Linaendana na utayari wa kukabili magumu na hatari kwa lengo fulani muhimu. Kwa Kigiriki linaitwa megalopsuchia, ambalo Aristotle alilitaja kama "taji la maadili yote". Kwa Kilatini linaitwa magnanimitas, neno lenye maana ile ya moyo mkuu.

                                     

Rushwa

Rushwa ni aina ya mwenendo usio wa uaminifu au usiofaa kwa mtu aliyepewa mamlaka, kumbe anatumia nafasi hiyo ili kupata faida binafsi. Ufisadi unaweza kuhusisha shughuli nyingi ikiwa ni pamoja na rushwa na udhalimu, ingawa inaweza pia kuhusisha mazoea ambayo ni ya kisheria katika nchi nyingi. Upande wa serikali, au kisiasa, rushwa hutokea wakati mmiliki wa ofisi au mfanyakazi mwingine wa serikali anafanya kazi rasmi kwa faida binafsi.

                                     

Shujaa

Shujaa ni mtu ambaye ameshinda juu ya jambo fulani, kwa mfano vita, au anaweza kukabili jambo lolote kwa ujasiri, bila kuzuiwa na woga. Katika fasihi ni mhusika mkuu wa utendi. Mifano ya mashujaa ni kuanzia wahusika wa kubuniwa wa kale kama Gilgamesh, Akile na Ifigenia, hadi watu halisi wa kale kama Yoana wa Arc au Sophie Scholl, mashujaa wa siku hizi kama Alvin York, Audie Murphy na Chuck Yeager, tena mashujaa wa katuni kama Superman, Spider-Man, Batman na Captain America.