ⓘ Sheria

Sheria ya kimataifa

Sheria ya kimataifa inaweza kuashiria mambo matatu: sheria ya umma ya kimataifa, sheria ya kibinafsi ya kimataifa au mgongano wa sheria na sheria ya mashirika makubwa ya kimataifa, kama vile sheria ya Umoja wa Ulaya. Sheria ya Umma ya Kimataifa inajihusisha na uhusiano kati ya mataifa huru. Vyanzo vya maendeleo ya sheria ya umma ya kimataifa ni desturi, mwenendo na mikataba kati ya nchi huru Mikataba ya Geneva. Sheria ya umma ya kimataifa inaweza kutengezwa na mashirika ya kimataifa, kama vile Umoja wa Mataifa ambao ulianzishwa baada ya Shirikisho la Kimataifa kushindwa kuzuia Vita Vikuu v ...

Mkusanyo wa Sheria za Kanisa

Mkusanyo wa Sheria za Kanisa ni kitabu ambamo zimekusanywa kwa mpango sheria kuu za Kanisa Katoliki zinazohusu waamini wake wa mapokeo ya Kilatini. Kwa lugha asili ya Kilatini unaitwa Codex Iuris Canonici.

Kumbukumbu la Sheria

Kumbukumbu la Sheria ni kitabu cha tano katika Tanakh na cha Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo. Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Ripoti za Sheria ya Kenya

Ripoti za Sheria ya Kenya ni ripoti rasmi za sheria katika Jamhuri ya Kenya ambazo zinaweza kutajwa kesini katika mahakama ya Kenya. Hurejelewa hivi: KLR. Ushauri wa uzinduzi wa Baraza la Taifa Sheria la ripoti za Sheria ulitokana na haja ya kuunganisha pengo kati ya kuripoti sheria na kushirikisha kuripoti sheria katika muundo wa serikali ya Kenya. Baraza hilo liliundwa na kuzinduliwa rasmi tarehe 20 Mei 1996 chini ya Mhe. Bw Jaji Majid Cockar, na kisha Jaji mkuu. Baada ya uzinduzi huu, Baraza hili lilikuwa na mikutano kadhaa na kutayarisha bajeti lakini ilisitisha shughuli zake kutokana ...

Sheria za Kanisa

Sheria za Kanisa ni taratibu zilizokubaliwa na mamlaka ya Kanisa katika kuendesha shughuli zake za ndani na za nje. Awali sheria za namna hiyo zilitolewa na Mitume wa Yesu, halafu na waandamizi wao, hasa maaskofu waliokusanyika katika mitaguso na sinodi mbalimbali Umuhimu wa sheria hizo ni tofauti kadiri ya madhehebu husika. Katika karne ya 20 Kanisa Katoliki, maarufu kwa kutia maanani umoja na utaratibu, limekusanya sheria zake muhimu zaidi katika vitabu viwili vya Kilatini: kimoja kwa Kanisa la Kilatini Codex Iuris Canonici, kingine kwa Makanisa Katoliki ya Mashariki Codex Canonum Eccles ...

Sheria za soka

Sheria za soka ni kanuni zilizoundwa maalumu ili kusimamia masuala yote yanayohusu mchezo wa soka. Sheria inaelezea idadi ya wachezaji kila timu inapaswa kuwa nao, urefu wa mchezo, kipimo cha uwanja na mpira, asili na aina za faulu refa anazoweza kutoa adhabu, sheria yenye utata kuliko zote ya kuotea na sheria nyingine kadhaa. Wakati wote wa mchezo, ni jukumu la refa kufafanua na kutekeleza kwa jinsi sheria inavyoelekeza. Katikati ya karne ya 19, kulifanyika jaribio ya kugeuza sheria kuwa za ishara zaidi. Sheria hizi zina historia ya kuanzia mwaka 1863 ambapo kifungu cha sheria kiliundwa n ...

                                     

ⓘ Sheria

  • Sheria kutoka neno la Kiarabu kwa Kiingereza law ni mfumo wa kanuni, ambazo kwa kawaida hutekelezwa kupitia seti ya taasisi maalumu. Inaunda siasa
  • Sheria ya kimataifa inaweza kuashiria mambo matatu: sheria ya umma ya kimataifa, sheria ya kibinafsi ya kimataifa au mgongano wa sheria na sheria ya mashirika
  • Mkusanyo wa Sheria za Kanisa la Kilatini ni kitabu ambamo zimekusanywa kwa mpango sheria kuu za Kanisa Katoliki zinazohusu waamini wake wa mapokeo ya
  • imani yake inayomuongoza katika maisha. Sheria ni kanuni zinazotungwa na jopo fulani la watu. Katika maisha sheria husaidia sana, hasa katika kuhakikisha
  • Kumbukumbu la Sheria pia: Kumbukumbu la Torati ni kitabu cha tano katika Tanakh yaani Biblia ya Kiebrania na cha Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo
  • za Sheria ya Kenya ni ripoti rasmi za sheria katika Jamhuri ya Kenya ambazo zinaweza kutajwa kesini katika mahakama ya Kenya sehemu 21 ya Sheria Hurejelewa
  • Sheria za Kanisa ni taratibu zilizokubaliwa na mamlaka ya Kanisa katika kuendesha shughuli zake za ndani na za nje. Awali sheria za namna hiyo zilitolewa
  • Sheria za familia ni sehemu za sheria ambazo zinahusika na masuala ya familia na mahusiano ya ndani ikiwa ni pamoja na: Asili ya ndoa, vyama vya muungano
  • Uwanja wa soka Sheria namba 2: Mpira wa kuchezea soka Sheria namba 3: Wachezaji wa soka Sheria namba 4: Jezi Sheria namba 5: Refa Sheria namba 6: Refa
  • Sheria Sheria inatoka wapi? au chanzo cha sheria ni nini? Kwa ufupi ni kwamba zipo dhana nyingi na tofautitofauti sana zinazoelezea asili ya sheria
                                     

Imani na sheria

Imani ni kukubaliana na kitu fulani hata kama si cha kuonekana. Kila mtu ana imani yake inayomuongoza katika maisha. Sheria ni kanuni zinazotungwa na jopo fulani la watu. Katika maisha sheria husaidia sana, hasa katika kuhakikisha kuwa usalama na amani zinakuwepo. Hapo zamani katika historia ya Kanisa sheria ilitumika hasa katika kuwaleta waliopotea katika ulimwengu wa roho. Lakini imani imekuwa mbele zaidi ya sheria Gal 3:10.

                                     

Wizara ya Sheria na Katiba

Wizara ya Sheria na Katiba ni wizara ya serikali nchini Tanzania. Ofisi kuu ya wizara hii zipo mjini Dar es Salaam.

                                     

Adhabu

Adhabu ni malipizi ambayo mtu hupewa kutokana na kosa alilofanya kwa makusudi au kwa bahati mbaya. Kadhalika kuna adhabu za aina nyingi, kama vile adhabu kubwa na adhabu ndogo. Katika nchi kadhaa kuna hata adhabu ya kifo.

                                     

Amri

Amri ni agizo au katazo linalotolewa na mamlaka yoyote kwa watu walio chini yake kwa namna moja au nyingine. Katika Biblia ni maarufu Amri Kumi za Mungu.

                                     

Chama

Chama ni kundi la watu wanaoungana kwa kusudi la kushirikiana ili kufikia lengo fulani, ambalo linaweza kuwa la aina nyingi tofauti, kwa mfano: dini, elimu, siasa, sanaa, michezo n.k. Idadi ya wanachama inaweza kuwa tofauti sana, kuanzia wachache hadi milioni kadhaa. Kwa kawaida chama kina uongozi wake unaopatikana kwa kufuata taratibu maalumu.

                                     

Chansela (kiongozi)

Chansela, pia kansela, ni cheo cha mkuu wa serikali, lakini si mkuu wa dola, katika Ujerumani na Austria. Kinafanana na cheo cha waziri mkuu.

                                     

Chifu

Chifu ni kiongozi wa jadi katika kabila fulani. Uongozi huo ulijitokeza mwishoni mwa zama za mawe na kutawala zama za chuma, mara nyingi ukisaidiwa na halmashauri ya wazee. Wakati wa ukoloni, uongozi huo uliweza kukubalika, mradi uwe chini ya himaya ya wakoloni. Hata baada ya uhuru, machifu wanaweza kuwa na madaraka fulani, k.mf. nchini Uganda.

                                     

Dhamana

Dhamana ni kitu chochote ambacho mtu anaweka au kuwekewa ili kukomboa kitu fulani au kupata huduma fulani. Dhamana inaweza kuwa pesa, gari, nyumba na hata chochote kile. Dhamana ipo katika pande nyingi, kwa mfano katika mahakama ili mshtakiwa aachiliwe kwa muda.

                                     

Hakimiliki ya mandharinyuma, mandharimbele, mandharikando na mandhariposti

Hakimiliki ya mandharinyuma, mandharimbele, mandharikando na mandhariposti ni aina nne za rasilimali ya hakimiliki kutokana na uvumbuzi.

                                     

Halmashauri

Halmashauri ni kikundi cha watu ambao wamechaguliwa au kuteuliwa wafanye kazi ya kuongoza, kutawala, kutunga sheria, kushauri na kuelekeza mambo. Pia ni chombo cha kiutawala chenye mamlaka kiasi fulani kuendesha shughuli za kiutawala za eneo husika kama vile wilaya au mji.