ⓘ Siasa

Siasa

Siasa ni njia ya kufanya maamuzi katika ngazi mbalimbali za jamii, kama vile mji, taifa, au hata dunia nzima. Sehemu muhimu ya siasa ni majadiliano kati ya watu mbalimbali wenye nguvu au mamlaka. Katika demokrasia kila mtu ana kiasi fulani cha nguvu, kwa hiyo siasa ya demokrasia ina maana ya watu wote kuchangia maamuzi. Hapa chini, mifumo mbalimbali ya kisiasa huelezwa kifupi:

Orodha ya vyama vya siasa Tanzania

Mfumo wa vyama vingi ni hali ya kuwa na chama zaidi ya kimoja,katika nchi moja.Madhumuni ya kuwa na vyama vingi vya siasa ni kuleta ushindani wa kisiasa,ili kuleta maendeleo ya nchi,upinzani wa kisiasa sio uadui kama watu wengi kwenye nchi zinazoendelea wanavyodhani,kuwa na vyama vingi ni kuongeza wigo wa demokrasia katika jamii huska. Tanzania ni nchi yenye mfumo wa vyama vingi vya siasa uliorejeshwa katika katiba ya Tanzania mwaka 1992. Chama tawala ni Chama cha Mapinduzi CCM ambacho kimetokana na muungano kati ya Tanganyika African National Union TANU na Afro Shiraz Party ASP ya Zanziba ...

Siasa ya Malawi

Siasa ya Malawi ina muundo wa taifa lenye demokrasia ya uwakilishi na mfumo wa urais. Rais wa Malawi ndiye kiongozi wa nchi na mkuu wa serikali. Mfumo wa uchaguzi unaotumika ni ule wa vyama vingi. Mamlaka ya Utendaji ’Executive power’’ inatekelezwa na serikali. Mamlaka ya Uundaji wa sheria vimepewa serikali na Bunge. Mamlaka ya kuhukumu iko huru kutoka zile ya utendaji na ya uundaji wa sheria. Serikali ya Malawi imekuwa demokrasia ya vyama vingi tangu mwaka 1994.

Waziri mkuu

Waziri Mkuu ni cheo cha kiongozi wa serikali. Neno lasema ya kwamba yeye ni mkubwa kati ya mawaziri wa serikali. Madaraka yake hutegemea na katiba ya nchi. Kwa kawaida cheo hiki kipo katika nchi ambako mkuu wa dola ambaye mara nyingi huitwa rais au pia mfalme hashughuliki mwenyewe mambo ya serikali. Lugha inaweza kuwa tofauti kati ya nchi na nchi. Anaweza kuitwa pia "Rais wa Mawaziri", "Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mawaziri" au "Chansella". Kuna hasa aina mbili za mawaziri wakuu kufuatana na katiba za nchi mbalimbali: Ujerumani chini ya rais, mfumo wa kibunge Singapore chini ya rais Tanzan ...

Siasa ya Nigeria

Siasa ya Nigeria hutendeka katika mfumo wa ushirikisho wa urais wa demokrasia wakilishi jamhuri, ambapo Rais wa Nigeria ambaye ni mkuu wa nchi na pia kiongozi wa serikali, na mfumo wa vyama vingi. Serikali ndiyo yenye mamlaka makuu. mamlaka ya bunge yako katika serikali na pia vyumba viwili vya bunge,ambayo ni Baraza la mawakilishi na Seneti. Pamoja vyumba viwili vya sheria hufanya mwili maamuzi nchini Nigeria kinachoitwa Bunge. Mahakama ya juu mkono wa serikali ya Nigeria ni Mahakama Kuu ya Nigeria. Nigeria pia hutumia nadharia yaBaron de Montesquieu katika mgawanyo wa madaraka. Kazi ya b ...

CNN

Cable News Network ni stesheni ya runinga inayotangaza habari iliyoanzishwa na Ted Turner mnamo 1980. CNN ilikuwa stesheni ya kwanza inayotangaza habari masaa 24. Makao yake makuu yako mjini Atlanta, ingawa ina vituo vingine mjini New York, Washington, D.C. na Los Angeles. Kauli yake mbiu ni The Worldwide Leader in News.

                                     

ⓘ Siasa

  • Siasa ni njia ya kufanya maamuzi katika ngazi mbalimbali za jamii, kama vile mji, taifa, au hata dunia nzima siasa ya kimataifa Sehemu muhimu ya siasa
  • chama zaidi ya kimoja, katika nchi moja.Madhumuni ya kuwa na vyama vingi vya siasa ni kuleta ushindani wa kisiasa, ili kuleta maendeleo ya nchi, upinzani wa
  • Siasa ya Malawi ina muundo wa taifa lenye demokrasia ya uwakilishi na mfumo wa urais. Rais wa Malawi ndiye kiongozi wa nchi na mkuu wa serikali. Mfumo
  • wakuu kufuatana na katiba za nchi mbalimbali: waziri mkuu kama kiongozi wa siasa ya nchi anachaguliwa na bunge. Mifano: Ethiopia, Uhindi, Uingereza au Ujerumani
  • Ufashisti ni siasa ya mrengo wa kulia ambayo ilitawala Italia tangu mwaka 1922 hadi 1943 ikiongozwa na mwanzilishi wake, dikteta Benito Mussolini 1883 - 1945
  • Uziki ni nadharia ya siasa iliyoanzishwa na Nnamdi Azikiwe, aliyekuwa kati ya waanzilishi wa Nigeria na rais wake wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia.
  • Siasa ya Nigeria hutendeka katika mfumo wa ushirikisho wa urais wa demokrasia wakilishi jamhuri, ambapo Rais wa Nigeria Umaru Musa Yar Adua ambaye ni
  • Urekebisho ni juhudi za makusudi za kuweka mambo sawa katika jambo fulani, kama vile siasa sheria, ugawaji wa ardhi, dini, utawa.
  • Cafferty, Mwanahabari Gloria Borger, Mchambuzi mkuu wa siasa Candy Crowley, Mwanahabari mkuu wa siasa Ali Velshi, Mwanahabari wa biashara Jeff Toobin, Mchambuzi
  • wao. Tamko la Arusha lina sehemu tano: Itikadi ya chama cha TANU Siasa ya ujamaa Siasa ya kujitegemea Uanachama wa TANU na Azimio la Arusha. Kiini chake
                                     

Ufashisti

Ufashisti ni siasa ya mrengo wa kulia ambayo ilitawala Italia tangu mwaka 1922 hadi 1943 ikiongozwa na mwanzilishi wake, dikteta Benito Mussolini. Kutokana nayo, aina za siasa zinazofanana zinaitwa pia ufashisti.

                                     

Uziki

Uziki ni nadharia ya siasa iliyoanzishwa na Nnamdi Azikiwe, aliyekuwa kati ya waanzilishi wa Nigeria na rais wake wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia. Azikiwe alifafanua siasa hiyo katika maandishi yake, kama vile: Renascent Africa na historia ya maisha yake: My Odyssey.

                                     

Mageuzi

Mageuzi ni mabadiliko ya taratibu hasa katika siasa ya nchi, tofauti na mapinduzi ambayo yanafanyika haraka na mara nyingi kwa kutumia nguvu.

                                     

Afrikanaizesheni

Afrikanaizesheni ni sera ya kuwapa Waafrika kazi za madaraka kwa kuwaondoa wageni wakati nchi za Afrika zilipokuwa zikipata uhuru.

                                     

G7

Kundi la G7 linaundwa na mawaziri wa fedha na magavana wa benki kuu wa nchi 7 zilizoendelea sana: Kanada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japani, Ufalme wa Muungano na Marekani ambao wanakutana ili kujadili hasa maswala ya uchumi. Umoja wa Ulaya pia unawakilishwa katika G7. Nchi hizo zinaongoza kwa utajiri wa kitaifa, zikiwa na 64% ya utajiri wote duniani $263 trilioni kadiri ya Credit Suisse Global Wealth Report October 2014.

                                     

Jamhuri

Jamhuri inataja aina za serikali zisizo na mfalme, malkia, sultani au mtemi wowote. Mara nyingi wananchi humchagua kiongozi wao akiitwa mara nyingi rais. Kuna pia vyeo vingine. Katika nadharia jamhuri inatakiwa kufuata muundo wa demokrasia. Lakini kuna pia jamhuri pasipo na serikali inayochaguliwa zikifuata kwa mfano muundo wa udikteta au utawala wa kijeshi. Kinyume chake kuna pia muundo wa ufalme pamoja na demokrasia, kwa mfano Uingereza au Uswidi.

                                     

Kura ya maoni

Kura ya maoni zinatumika katika demokrasia ili kuchagua viongozi wa nchi au kuamua kama sheria fulani itumike. Kawaida kura ya maoni hupigwa na wale wote wenye umri halali wa kupiga kura ili kukubali au kukataa pendekezo, sera, sheria, mabadiliko ya katiba, katiba mpya, kukataa au kumuunga mkono kiongozi fulani. Kura ya maoni huchukuliwa kuwa ni aina mojawapo ya demokrasia ya moja kwa moja.

                                     

Meya

Meya katika taratibu za nchi nyingi duniani, ndiye kiongozi wa juu kabisa katika manispaa, mji au jiji. Majukumu yake yanategemea ukubwa wa eneo lake, idadi ya wakazi, sheria n.k.

                                     

Mkuu wa mkoa

Mkuu wa Mkoa ni kiongozi mkuu wa serikali katika mkoa. Jukumu la kiutawala la Mkuu wa Mkoa ni kuhakikisha kwamba mifumo ya utawala katika wilaya zake inafanya kazi vizuri na kwa ufanisi. Kwa Tanzania kiongozi huyo huteuliwa na Rais. Ndiye mwakilishi wa Rais katika Mkoa.

                                     

Mkuu wa wilaya

Mkuu wa wilaya ni kiongozi mkuu wa serikali katika wilaya. Jukumu la kiutawala la Mkuu wa Wilaya ni kuhakikisha kwamba mifumo ya utawala katika wilaya yake inafanya kazi vizuri na kwa ufanisi. Kwa Tanzania kiongozi huyo huteuliwa na Rais. Ndiye mwakilishi wa Rais katika wilaya.

                                     

Mpigania uhuru

Mpigania uhuru ni mtu ambaye hujihusisha na harakati za kujikomboa au kukomboa watu wengine. Anaweza kuwa anatumia mikakati ya vita au majadiliano ili kuletea anaowatetea uhuru.

                                     

Pogromu

Pogromu ni ghasia kali inayolengwa dhidi ya kundi maalumu kama vile wafuasi wa dini au kabila fulani. Neno latokana na ghasia za fujo katika Urusi wa karne ya 19 ambako Wayahudi walishambuliwa, maduka na nyumba zao kuharibiwa na idadi ya watu kuuawa hovyo. Kwa hiyo neno "pogromu" lataja hasa mashambulio dhidi ya Wayahudi katika Ulaya. Lakini inatumiwa pia kwa mashambulio dhidi ya vikundi vingine.

                                     

Serikali ya muungano

Serikali ya muungano ni serikali inayoundwa na nchi mbili au zaidi ambapo nchi hizo huwakilishwa kimataifa kama nchi moja. Mfano mmojawapo ni serikali ya Tanzania ambayo ni serikali ya Jamhuri ya Muungano; kielelezo chake ni serikali ya Ufalme wa Muungano wa Britania na Ireland Kaskazini.

                                     

Ushikiliaji Ukale

Ushikiliaji Ukale ni wazo la kisiasa. Wafuasi wa ushikiliaje ukale, wanaushikilia ukale, kama jinsi mambo yalivyo kwa sasa, au kama jinsi mambo yalivyokuwa hapo awali. Washikiliaje ukale wanaitaka serikali kutenda aidha kulinda jinsi maisha ya sasa yalivyo, au kurejea katika hali nzuri ya maisha tulivyokuwa tukiishi na kuifurahia. Kifupifupi hawataki mabadiliko mapya na maisha haya tunayoishi, bali yale ya kale.