ⓘ Uchumi

Uchumi

Uchumi ni jumla ya shughuli zote za binadamu zinazolenga kutosheleza mahitaji yao. Ni hasa uzalishaji, usambazaji na utumiaji wa bidhaa pamoja na kutolewa kwa huduma kwa njia mbalimbali. Uchumi mara nyingi hutazamwa kwenye ngazi za kijiji, eneo, taifa au dunia. Sayansi ya Uchumi kwa Kiingereza economics ni tawi la elimu inayochunguza masharti ya uchumi kufaulu au kushindwa.

Supamaketi za Uchumi

Supamaketi za Uchumi ni mtandao wa supamaketi nchini Kenya ulioanzishwa mwaka wa 1975 na uliorodheshwa katika Soko la Hisa la Nairobi mwaka wa 1992.

Somo la Uchumi

Somo la uchumi ni sayansi ya kijamii ambayo hutafiti uzalishaji, usambazaji, na matumizi ya bidhaa na huduma. Neno uchumi linatokana na kitenzi "kuchuma". Jina la Kiingereza economy linatokana na neno la Kigiriki cha Kale oikonomia lenye maana ya "usimamizi wa kaya, utawala", kwa hiyo "sheria za nyumba kaya". Aina za masomo ya kiuchumi ya kisasa zilizotokana na somo pana la uchumi wa kisiasa katika miaka ya mwisho ya karne ya 19, kutokana na matamanio ya kuchukua mwelekeo jarabati unaofaa zaidi sayansi za kiasilia. Ufafanuzi unaojumuisha mengi ya masomo ya kiuchumi ya kisasa ni ule wa Lion ...

Uchumi Maduka Makubwa

Uchumi Maduka makubwa ni mfuatano wa maduka makubwa Kenya ambayo ilianzishwa mwaka 1975 na ambayo iliorodheshwa kwenye Soko la hisa la Nairobi mwaka 1992. Jina Uchumi maana yake ni "economy" katika kiingereza.

London School of Economics

Chuo kilianzishwa mwaka 1895 mjini London na leo hii ni sehemu ya Chuo Kikuu cha London. Hasa idara ya uchumi ina sifa za kimataifa. Zaidi ya wakuu wa dola 39 walisoma katika chuo hiki na 8 kati yao wanashika nafasi ya mkuu wa nchi mwaka 2007. Maprofesa pamoja na waliopata digrii chuoni hapa jumla 14 walipokea tuzo ya Nobel ya uchumi, amani au fasihi. Nafasi za kuendesha utafiti pamoja na nafasi kwa ajili ya wanafunzi huhesabiwa kati ya bora kabisa duniani.

Kilimo

Kilimo ni uzalishaji wa mazao kwenye mashamba. Kilimo kina maana pana inayojumuisha mifumo ya uzalishaji mimea, ufugaji wa wanyama, na uvuvi wa samaki. Mara nyingi kilimo cha mimea kinaenda sambamba na ufugaji wa wanyama. Watu hupanda mimea na kuitunza hadi mavuno hasa kwa uzalishaji wa chakula cha binadamu na lishe ya wanyama, lakini pia kwa shabaha ya kupata malighafi mbalimbali zinazotumiwa kwa kutengeneza nguo za watu. Siku hizi kilimo kinalenga pia nishati ya mimea. Mtu anayejihusisha na kilimo huitwa mkulima.

                                     

ⓘ Uchumi

  • Uchumi ni jumla ya shughuli zote za binadamu zinazolenga kutosheleza mahitaji yao. Ni hasa uzalishaji, usambazaji na utumiaji wa bidhaa pamoja na kutolewa
  • Supamaketi za Uchumi kifupi: Uchumi ni mtandao wa supamaketi nchini Kenya ulioanzishwa mwaka wa 1975 na uliorodheshwa katika Soko la Hisa la Nairobi
  • Uchumi Maduka makubwa ni mfuatano wa maduka makubwa Kenya ambayo ilianzishwa mwaka 1975 na ambayo iliorodheshwa kwenye Soko la hisa la Nairobi mwaka 1992
  • Wizara ya Fedha na Uchumi Kiingereza: Ministry of Finance and Economic Affairs kifupi MOF ni wizara ya serikali nchini Tanzania. Ofisi kuu ya wizara
  • Chuo cha Uchumi London London School of Economics and Political Science kwa kawaida kifupi: LSE kwa London School of Economics ni kati ya vyuo maarufu
  • hicho husaidia katika kukuza uchumi wa nchi yake ili hatimaye itakuwa imejikomboa kiuchumi. Sekta hiyo ndiyo kiinua uchumi kikubwa kwa mataifa mengi. Kwa
  • taifa hawajatengeneza, ila vipo nao huvitegemea kwa ajili ya kuendeleza uchumi wa taifa husika. Kwa mfano Tanzania ni nchi yenye rasilimali nyingi ambazo
  • inaweza kuwa sehemu maalum. Neno soko linaweza likajumuisha maana kwenye uchumi Linaweza kumaanisha njia ambayo bidhaa zinauzwa na kununuliwa. Kuna masoko
  • Kiingereza: industry, manufacturing ni neno la kutaja matawi mbalimbali ya uchumi wa nchi ambako bidhaa zinatengenezwa au huduma kutolewa. Kiasili tasnia
  • mtaji, ni dhana muhimu katika elimu ya uchumi Inataja moja kati ya vyombo vya uzalishaji kufuatana na elimu ya uchumi pamoja na ardhi, kazi na elimu. Rasilmali
                                     

Wizara ya Fedha na Uchumi

Wizara ya Fedha na Uchumi) ni wizara ya serikali nchini Tanzania. Ofisi kuu ya wizara hii zipo mjini Dar es Salaam.

                                     

Maliasili

Maliasili ni vitu ambavyo watu au taifa hawajatengeneza, ila vipo nao huvitegemea kwa ajili ya kuendeleza uchumi wa taifa husika. Kwa mfano Tanzania ni nchi yenye rasilimali nyingi ambazo ni kama mbuga za wanyama, madini na mengine mengi. Suala ni hizo maliasili zinatumikaje katika kuendeleza uchumi wa nchi. Ingewekeza katika uendelezaji wa maliasili, nchi ingekuwa na uchumi wa hali ya juu. Pia wananchi wanatakiwa kuzitunza na kuzijali ili zitumike vyema katika ukuaji wa uchumi wetu.

                                     

Bajeti

Bajeti ni makadirio ya mapato na matumizi ya fedha katika kipindi fulani ili kuhakikisha mipango inafanikiwa kwa wakati uliotarajiwa.

                                     

Bei

Bei inaweza kufafanuliwa namna tofauti. Pengine ufafanuzi rahisi ni kusema "bei ni thamani ya bidhaa au huduma". Bei inaonyeshwa kwa bidhaa nyingine, huduma, au kwa pesa.

                                     

Bidhaa

Bidhaa ni kitu chochote kinachotoka kwenye soko na kinachoweza kuridhisha watu. Kwenye utengenezaji kwa kawaida hununuliwa kama malighafi kama vile vyuma na kuuzwa kama bidhaa. Bidhaa hatarishi ni zile zinazoweza kusababisha madhara kwa jamii. Mazao ya kilimo na huduma ni aina nyingine ya bidhaa kuu.

                                     

Bima

Bima ni njia ya ulinzi wa kiuchumi dhidi ya hasara ya kifedha au hata dhidi ya kifo ambayo watu au kampuni wanafuata kwa kulipa kiasi fulani kwa shirika la bima kadiri ya mkataba maalumu, hivi kwamba shida ikitokea shirika litoe fidia.

                                     

Chumvini

Chumvini ni mahali ambapo chumvi huvunwa kwa wingi. Nchini Tanzania chumvi huvunwa hasa katika mkoa wa Lindi na mikoa mingine mingi yenye bahari. Chumvi hutolewa ikiwa ya mawe na hupelekwa viwandani kwa ajili ya kusagwa na pengine kuongezewa madini mbalimbali kama kalisium, iodini n.k.

                                     

Fidia ya kifedha

Fidia ya kifedha inamaanisha kitendo cha kumpatia mtu pesa au vitu vingine vyenye thamani ya kiuchumi badala ya bidhaa zake, malipo ya kazi aliyofanya, au kulipia gharama za hasara ambayo amepata. Aina ya fidia ya kifedha ni pamoja na: Uharibifu Ujira Malipo Fidia ya utaifishaji inayolipwa kukitokea kutaifishwa kwa mali Fidia iliyoahirishwa Fidia ya mtendaji Mirabaha Mshahara Faida za mfanyakazi Fidia ya wafanyakazi, kulinda wafanyakazi ambao wamepata majeraha yanayohusiana na kazi

                                     

Ingizo la shajara

Katika biashara, ingizo la shajara ni tendo la kuzishika au kuzirekodi shughuli za kibiashara za kiuchumi au zile zisizo za kiuchumi.

                                     

Kipato

Kipato ni kitu chochote au malipo anayopata mtu baada ya kufanya kazi fulani. Kila mmoja lazima awe na kipato chake, haijalishi ni kiasi gani, tena kipato cha mtu ni siri yake mwenyewe. Hata hivyo watafiti wanajitahidi kujua kipato cha taifa zima na cha wastani wa wananchi wake ili kuratibu uchumi n.k.