ⓘ Dini

Dini

Dini inamaanisha jumla ya imani ya binadamu kadhaa pamoja na mafundisho wanayotoa kuhusu yale ambayo wanayazingatia ama kuyasadiki, yaani mambo ya roho, kama vile kuhusiana na Mungu, maisha na uumbaji. Ibada ni nguzo mojawapo iliyo dhahiri miongoni mwa dini kadhaa katika kuunganisha dhamira za mwenye kushika dini na mhimili wa imani, lakini dini inahusu pia mafundisho kuhusu maadili, mema na mabaya, imani na jinsi ya kushiriki katika jumuiya za waumini. Kwa maana nyingine "dini" inataja jina kielelezo juu ya aina mbalimbali za imani jinsi inavyopatikana duniani, yaani jumuiya za kidini.

Dini rasmi

Dini rasmi ni dini ambayo imetangazwa na nchi fulani kuwa yake kwa namna ya pekee. Kiasi ambacho dini hiyo inapata sapoti ya sheria, serikali n.k. inategemea kwa kawaida katiba ya nchi. Si lazima serikali iwe chini ya mamlaka ya dini hiyo, wala kufuata masharti yake yote, wala kwamba uongozi wa dini uwe chini ya serikali au kwamba serikali iwe chini ya viongozi wa dini.

Dini asilia za Kiafrika

Dini asilia za Kiafrika ni kati ya dini za jadi ambazo zinadumu hata leo, ingawa wafuasi wake wanapungua mwaka hadi mwaka kulingana na dini zilizotokea Mashariki ya Kati, hasa Ukristo na Uislamu, ambazo zinazidi kuenea barani Afrika. Dini za Kiafrika zinafuata imani maalumu, sawa kabisa na hizo za nchi za ughaibuni ambazo zimeleta mfumo mpya wa kuabudu. Badala ya kuabudia mapangoni au misituni kama Waafrika walio wengi walivyofanya kwa karne nyingi, zimehimiza kujenga makanisa na misikiti kwa ajili ya kumwabudu Mungu kadiri ya ufunuo wake mwenyewe. Madhehebu mengi ya Kikristo yamekuwa yaki ...

Nchi isiyo na dini

Nchi zisizo na dini ni nchi zilizoamua kutosimama upande wa dini yoyote kati ya zile zinazofuatwa na wakazi wake. Si kwamba nchi ya namna hiyo inapinga dini, bali inakusudia kuwatendea wakazi wote na miundo yao ya dini kwa usawa, bila upendeleo, ingawa pengine busara inadai kuzingatia wingi wa watu wanaozifuata, kwa mfano katika kukubali baadhi ya sikukuu katika kalenda ya taifa. Kwa ajili hiyo siasa haitakiwi kutegemea dini yoyote, bali ustawi wa jamii unaolengwa kwa kuzingatia hoja ambazo nguvu yake inatokana na ukweli unaojulikana na akili tu.

Dini nchini Tanzania

Dini za wananchi wengi wa nchi ya Tanzania ni Uislamu, Ukristo na dini asilia za Afrika. Nje ya hao wako wachache wanaofuata Uhindu, Usikh na dini nyingine na mara nyingi hawa ni wahamiaji katika nchi au wamezaliwa katika vikundi vyenye asili ya uhamiaji kutoka nje. Siasa ya serikali na dola ni kutokuwa na dini rasmi. Katiba inatoa uhuru wa dini, na serikali inaheshimu haki hii kwa vitendo.

Uhuru wa dini

Uhuru wa dini ni mojawapo kati ya haki za msingi za kila binadamu kutokana na hadhi yake inayomtofautisha na wanyama. Yaani akili yake inamfanya atafute ukweli, jambo linalohitaji kuwa huru kutoka kwa mwingine yeyote. Uhuru huo unaendana na wajibu na haki ya kufuata dhamiri hasa katika masuala ya dini na maadili. Haki hiyo inatajwa katika Tamko la kimataifa la haki za binadamu lililotolewa na Umoja wa Mataifa mwaka 1948, ingawa haitekelezwi vizuri katika nchi nyingi, hasa zile zinazofuata rasmi dini fulani au zinapinga dini zote. Haki hiyo inajumlisha haki ya kuwa au kutokuwa na imani fula ...

                                     

ⓘ Dini

  • Dini kutoka Kiarabu اﻟدﻴن, tamka: ad - din inamaanisha jumla ya imani ya binadamu kadhaa pamoja na mafundisho wanayotoa kuhusu yale ambayo wanayazingatia
  • Dini rasmi ni dini ambayo imetangazwa na nchi fulani kuwa yake kwa namna ya pekee. Kiasi ambacho dini hiyo inapata sapoti ya sheria, serikali n.k. inategemea
  • Dini za jadi ni dini za mababu ambazo zinafuata miiko na maadili halisi ya taifa au kabila fulani. Katika bara la Afrika dini hizo zinaegemea zaidi kwenye
  • Dini asilia za Kiafrika ni kati ya dini za jadi ambazo zinadumu hata leo, ingawa wafuasi wake wanapungua mwaka hadi mwaka kulingana na dini zilizotokea
  • Nchi zisizo na dini yaani zisizo na dini rasmi ni nchi zilizoamua kutosimama upande wa dini yoyote kati ya zile zinazofuatwa na wakazi wake. Si kwamba
  • Dini nchini Kenya kwa jumla zinaishi kwa amani, ingawa miaka ya hivi karibuni baadhi ya Wakristo waliuawa na wafuasi wa Al Shabaab. Upande wa takwimu
  • Dini za wananchi wengi wa nchi ya Tanzania ni Uislamu, Ukristo na dini asilia za Afrika dini za jadi Nje ya hao wako wachache wanaofuata Uhindu, Usikh
  • Uhuru wa dini ni mojawapo kati ya haki za msingi za kila binadamu kutokana na hadhi yake inayomtofautisha na wanyama. Yaani akili yake inamfanya atafute
  • Dini nchini Urusi zimepata uhai mpya na kustawi tena tangu Ukomunisti uanguke mwaka 1989. Wafuasi wa dini hawahesabiwi katika sensa, hivyo kuna makadirio
  • Uyahudi ni mojawapo kati ya dini za kale za binadamu, lakini jina hilo lilienea baada ya makabila mengi ya Israeli kutoweka, hata wakabaki karibu watu
                                     

Dini za jadi

Dini za jadi ni dini za mababu ambazo zinafuata miiko na maadili halisi ya taifa au kabila fulani. Katika bara la Afrika dini hizo zinaegemea zaidi kwenye matambiko kwa mizimu ya ukoo ili isaidie jamaa zao. Siku hizi idadi ya wafuasi wa dini hizo inazidi kupungua na kuziachia nafasi dini za kimataifa, hasa Ukristo na Uislamu. Hata hivyo mabaki ya imani ya asili yanawaandama waliojiunga na dini hizo, hasa kwa namna inayotazamwa nazo kuwa ushirikina.

                                     

Dini nchini Kenya

Dini nchini Kenya kwa jumla zinaishi kwa amani, ingawa miaka ya hivi karibuni baadhi ya Wakristo waliuawa na wafuasi wa Al Shabaab. Upande wa takwimu, kulingana na sensa ya mwaka 2009, asilimia 82.5 ya wakazi wa Kenya walikuwa Wakristo, asilimia 11.1 ni Waislamu, asilimia 1.6 ni wafuasi wa dini za jadi, asilimia 1.7 ni wa makundi mengine ya dini, na asilimia 2.4 wanadai hawana uhusiano na dini yoyote ile.

                                     

Asili

Asili ni chanzo cha jambo fulani. Kila kitu kina asili yake, hakuna kitu duniani au ulimwenguni jumla kisichokuwa na asili. Kwa mfano, kadiri ya dini mbalimbali, asili kuu ya binadamu wote ni Mungu aliyewaumba, ingawa pia Adamu na Eva wanatazamwa kuwa asili ya wale wote waliozaliwa nao.

                                     

Belzebuli

Belzebuli ni jina lililotokana na lile la mungu mmojawapo wa Wafilisti wa Ekron, ambalo tena linahusiana na Baal, mungu mkuu wa Kanaani. Baadaye lilitumiwa na Wayahudi, Wakristo na Waislamu kama jina la mmojawapo kati ya pepo wakuu zaidi, ila badala ya kumuita Beel Zebul, yaani Baal Mfalme, walitamka Baal Zebub, yaani mungu wa nzi. Kwa Kiarabu jina limekuwa Baʿlzabūl بعلزبول.

                                     

Dhabihu

Dhabihu ni kitu, sanasana mnyama, kinachotolewa kama sadaka kwa minajili ya mizimu ama tambiko. Mahali penyewe panaitwa pia dhabihu au, vizuri zaidi, madhabahu, Katika Kanisa Katoliki ni jina la vitu vinavyotolewa altareni wakati wa Misa mkate na divai yenye maji kidogo kwa ajili ya sadaka ya ekaristi.

                                     

Dhuluma

Dhuluma ya kidini, ya kisiasa, ya kikabila n.k. ni kati ya makosa ya jinai dhidi ya utu yanayolaaniwa kimataifa, k.mf. katika Nuremberg Principles. Mtu anayetenda hivyo anaitwa dhalimu, kama yeyote anayewakosea haki wengine.

                                     

Ibilisi

Ibilisi ni jina linalomaanisha "Mpinzani"; "Mwekakiwazo" na linatumika kwa Shetani. Neno hili hutumika mara 35 katika Agano Jipya, sehemu muhimu zaidi ya Biblia ya Kikristo.

                                     

Kisasili

Kisasili ni habari inayotokeza imani na maadili ya utamaduni fulani kuhusu asili ya ulimwengu au ya mambo muhimu ya msingi katika maisha ya binadamu. Mara nyingi habari hiyo inatazamwa kuwa si ya kihistoria, ingawa inaweza kuwasilisha ukweli fulani. Lugha nyingi zinatohoa neno la Kigiriki μύθος, mythos, likitamkwa myuthos.

                                     

Kutabaruku

Katika madhehebu mbalimbali, kama Kanisa Katoliki, Orthodoksi na Anglikana, makanisa yanawekwa wakfu na askofu kwa ibada inayoitwa kutabaruku. Utaratibu mzima wa Kanisa la Kilatini unapatikana katika Caeremoniale Episcoporum, sura IX-X, na katika Missale Romanum. Desturi hiyo ni ya kale, labda kama ujenzi wenyewe wa makanisa. Mwanzoni mwa karne ya 4 inashuhudiwa sehemu nyingi. Inawezekana sana kwamba desturi hiyo ilitokana na ile ya Agano la Kale.

                                     

Maarifa

Maarifa ni njia inayotumiwa kujitoa katika shida ama kuweza kupata kitu, kwa kutumia elimu au ujuzi. Ujuzi huo unaweza ukawa wa kuzaliwa nao au ukatokana na mangamuzi ya maisha yakiwa pamoja na kusoma, kusikia au kutenda. Pia huhusisha ufahamu na uelewa, hususani wa ukweli, kama ulivyofundishwa au kuthibitishwa na Roho Mtakatifu. Neno hilo linatumika pia kudokeza mbinu za ushirikina katika kufanikisha mambo kadiri ya matakwa ya mtu.