ⓘ Historia

Historia

Historia ni somo kuhusu maisha ya binadamu na utamaduni wao wakati uliopita. Mara nyingi neno hilo lina pia maana ya maarifa yoyote kuhusu wakati uliopita, yawe au yasiwe maarifa ya watu kwa mfano "historia ya ulimwengu". Historia ni hasa mfululizo wa habari za mambo yaliyotokea pamoja na sababu zake. Binadamu anaziandika ili kuelewa maisha yake, yaani ametokea wapi, amepata mafanikio gani na matatizo gani. Historia inatufundisha kuishi: kumbukumbu za mambo ya zamani zinatuwezesha kuendelea vizuri zaidi. Wanahistoria wanapata maarifa yao kutoka maandishi ya zamani hasa kwa historia andishi ...

Historia ya awali

Historia ya awali ni kipindi kirefu sana cha historia, kikichukua miaka yote tangu binadamu walipotokea duniani mpaka historia andishi ilipoanza. Ingawa muda ni mrefu sana na ni wa msingi kwa historia yote iliyofuata, watu hawakuwa wengi kama walivyozidi kuwa kadiri ya maendeleo yao. Maisha yao hayakuwa marefu kutokana na ugumu wa mazingira na utovu wa vifaa na dawa mbalimbali.

Historia ya Afrika

Historia ya Afrika ni historia ya bara hilo lililo asili ya binadamu wote. Kwa ujumla, historia ni kumbukumbu ya maisha ya mwanadamu duniani, hasa ile tarehe iliyosajiliwa na kuhifadhiwa katika vitabu, maandishi mbalimbali, na simulizi au hekaya za mapokeo. Ingawa historia iliyobebwa katika simulizi na hekaya huchukuliwa na baadhi kuwa haina nguvu kwa kukosa ithbati ya maandishi, bado hivi ni vyanzo muhimu vya historia. Mara nyingi historia iliyoko katika maandishi huwa imehifadhiwa katika simulizi na hekaya kwa muda mrefu kabla ya kuandikwa.

Historia ya Uturuki

Waturuki waliwahi kuwa kiini cha Milki ya Osmani pia: Ottomani iliyounganisha mataifa mengi chini ya Sultani wa Konstantinopoli. Hilo dola kubwa lilitawala upande wa mashariki wa Mediteranea pamoja na nchi nyingi za Mashariki ya kati ya karne ya 14 na mwaka 1922. Milki ilianzishwa na Waturuki Waosmani ikachukua nafasi ya ukhalifa wa Waabbasi na Milki ya Bizanti. Mji wake mkuu ulikuwa Konstantinopoli leo: Istanbul na mtawala wake mkuu alikuwa Sultani wa Waosmani. Imani rasmi ya milki ilikuwa Uislamu hata kama katika maeneo mengi idadi kubwa ya wakazi walikuwa Wakristo. Tabaka la viongozi wa ...

Historia ya Uhindi

Binadamu walifika India kutoka Afrika kabla ya miaka 55.000 iliyopita. Uwepo wao wa muda mrefu, kwanza kama wawindaji-wakusanyaji waliozagaa barani, umefanya watu wa eneo hilo wawe na tofauti kubwa kati yao upande wa urithi wa kibiolojia, ambayo inapitwa na Waafrika tu. Makazi ya kudumu yalianza magharibi, katika beseni la mto Indus, miaka 9.000 iliyopita, hata kuzaa ustaarabu maalumu Indus Valley Civilisation katika milenia ya 3 KK.

Historia ya Lithuania

Kuanzia karne ya 13 Lithuania ilikuwa nchi huru na imara iliyoteka maeneo mengi; kufikia karne ya 15, ikiwa pamoja na Polandi, ilikuwa kubwa kuliko nchi zote za Ulaya. Mwaka 1795 nchi hizo mbili zilifutwa, na Lithuania ikawa sehemu ya Dola la Urusi. Mwaka 1918, ikawa tena nchi huru, lakini mwaka 1940 Warusi waliiteka tena. Miaka 1940 - 1990 nchi ilikuwa jamhuri mwanachama wa Umoja wa Kisovyeti. Baada ya umoja huo wa majimbo 15 kusambaratika, Lithuania ilijitangaza nchi huru. Lithuania imekuwa nchi mwanachama ya Umoja wa Ulaya tangu tarehe 1 Mei 2004.

                                     

ⓘ Historia

  • Historia ya Asia Historia ya Australia Historia ya Ulaya Historia ya Wokovu Historia ya Kanisa Historia ya teolojia Historia ya utawa Historia ya Kanisa Katoliki
  • Historia ya awali kwa Kiingereza: prehistory ni kipindi kirefu sana cha historia kikichukua miaka yote tangu binadamu walipotokea duniani mpaka historia
  • Historia ya Afrika ni historia ya bara hilo lililo asili ya binadamu wote. Kwa ujumla, historia ni kumbukumbu ya maisha ya mwanadamu duniani, hasa ile
  • Historia ya Kanisa ni fani inayochunguza historia ya Ukristo na ya miundo yake mbalimbali tangu Kanisa lilipoanzishwa na Yesu Kristo katika karne ya 1
  • Historia ya Uhindi inahusu historia ya maeneo ambayo leo yanaunda jamhuri ya India. Binadamu walifika India kutoka Afrika kabla ya miaka 55, 000 iliyopita
  • Historia ya Uturuki inahusu eneo ambayo siku hizi linaunda Jamhuri ya Uturuki. Waturuki waliwahi kuwa kiini cha Milki ya Osmani pia: Ottomani iliyounganisha
  • Historia ya Japani inahusu eneo ambalo leo linaunda ufalme wa Japani. Visiwa vyake vilikaliwa na binadamu tangu miaka 30, 000 KK. Wakazi wa sasa wametokana
  • Historia ya Lithuania inahusu eneo la Ulaya ambalo wakazi wake leo wanaunda Jamhuri ya Lithuania. Kuanzia karne ya 13 Lithuania ilikuwa nchi huru na imara
  • Historia ya Moroko inahusu eneo ambalo leo ni nchi ya Afrika kaskazini - magharibi. Habari za kimaandishi za kwanza ni kutoka karne za kwanza KK. Wafinisia
  • Historia ya Denmark inahusu eneo ambalo leo linaunda ufalme wa Udani. Utafiti wa akiolojia umeonyesha ya kwamba Denmark iliwahi kuwa na vikundi vya wawindaji
                                     

Historia ya Japani

Historia ya Japani inahusu eneo ambalo leo linaunda ufalme wa Japani. Visiwa vyake vilikaliwa na binadamu tangu miaka 30.000 KK. Wakazi wa sasa wametokana na mchanganyiko wa makabila asili kama Waainu na Wakorea waliovamia visiwa hivyo kuanzia 500 KK.

                                     

Aathari

Aathari ni masalio ya vitu na utamaduni wa watu fulani. Mfano wa masalia ni magofu ya kale, vitu vya utamaduni na kadhalika. Wataalamu wa akiolojia ndio wanaotafuta na kuchunguza mabaki hayo ili kuelewa zaidi mambo ya kale yalikuwaje na watu wa wakati huo waliishi vipi.