ⓘ Lugha

Lugha

Lugha ni utaratibu wa kuwasiliana kati ya binadamu. Somo la lugha linaitwa maarifa ya lugha au isimu. Mwaka wa 2008 ulikuwa Mwaka wa Lugha wa Kimataifa.

Lugha za Kibantu

Lugha za Kibantu ni kundi la lugha ambalo ni tawi la lugha za Niger-Kongo. Lugha za Kibantu huzungumzwa hasa katika nchi za Nigeria, Kamerun, Guinea ya Ikweta, Gabon, Jamhuri ya Kongo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya, Tanzania, Komori, Msumbiji, Malawi, Zambia, Zimbabwe, Angola, Namibia, Botswana, Lesotho, Swaziland na Afrika ya Kusini. Uenezi huo unaonyesha kwamba kundi la lugha za Kibantu ni kubwa kabisa barani Afrika, na idadi ya wanaozitumia ni takriban watu milioni 310. Neno Bantu, maana yake ni watu katika lugha nyingi za kundi hilo. Shina lake ni -nt ...

Lugha rasmi

Lugha rasmi ni lugha iliyopewa cheo maalumu katika nchi fulani. Kwa kawaida ni lugha inayotumiwa hasa na serikali kwa mawasiliano kati ya ofisi zake na pia kwa matangazo rasmi, kwa mfano kwa kutangaza sheria. Ni pia lugha ya kuendesha kesi mahakamani na kuandika hukumu. Kuna nchi zenye lugha rasmi moja tu lakini nchi nyingi huwa na lugha mbalimbali zinazokubaliwa kama lugha rasmi kwenye ngazi tofauti za serikali. Katika nchi mbalimbali lugha rasmi imetajwa katika katiba ya taifa au katika sheria mahsusi, lakini nchi nyingine hazina sheria juu ya lugha rasmi hata kama hali halisi ipo na kue ...

Lugha ya kwanza

Lugha ya kwanza ni lugha ambayo mtu anaiongea kama lugha yake ya kwanza tangu utotoni, umri ambamo ni rahisi zaidi kuathiriwa na mazingira na hivyo pia kujifunza kusema kama watu wa kandokando. Pia lugha hiyo huitwa lugha mama kwa Kiingereza "mother tongue" kwa vile watu wengi hujifunza lugha yao ya kwanza kutoka kwa mama mzazi. Lakini hiyo si lazima: mara nyingine mtoto halelewi na mama, au kama analelewa, anatumia muda mrefu zaidi na watoto wenzake hasa shuleni, hivyo anazoea lugha yao kuliko ile ya nyumbani, hata kama ni tofauti kabisa. Kwa sababu hiyohiyo wapo watu wenye lugha mama zai ...

Lugha za Kihindi-Kiulaya

Lugha za Kihindi-Kiulaya ni jamii ya lugha iliyo kubwa kuliko zote duniani. Imekadiriwa kuna lugha hai 445 za jamii hiyo na wasemaji bilioni 3.2 katika mabara yote. Uenezi huo umetokana hasa na historia ya ukoloni wa Kizungu uliopeleka lugha za Ulaya pande zote za dunia. Lugha zenye wasemaji zaidi ya milioni 100 ni: Kihispania, Kiingereza, Kihindustani Kihindi/Kiurdu, Kireno, Kibengali, Kipanjabi na Kirusi. Nyingine zenye wasemaji zaidi ya milioni 50 ni: Kijerumani, Kifaransa, Kimarathi, Kiitalia na Kiajemi.

Lugha za Kiafrika-Kiasia

Lugha za Kiafrika-Kiasia ni familia ya lugha barani Afrika na Asia. Katika familia hiyo kuna lugha zaidi ya 300 zenye wasemaji milioni 350 kati ya Afrika ya Kaskazini na Asia ya Magharibi, hasa Kiarabu, lakini pia Kihausa, Kioromo, Kiamhara, Kisomali, Kiebrania n.k. Lugha inayozungumzwa zaidi ni Kiarabu. Pia ni lugha inayozungumzwa zaidi katika tawi la Kisemiti, kabla ya Kiamhari lugha ya pili ya Kisemiti inayozungumzwa zaidi. Kiarabu ina karibu wasemaji milioni 290, haswa iliyojilimbikizia Mashariki ya Kati, Afrika Kaskazini na Pembe ya Afrika. Mbali ya lugha zinazozungumzwa leo, kundi hi ...

                                     

ⓘ Lugha

  • jamii Lugha hutolea elimu Lugha huleta mawasiliano katika jamii Lugha hukuza utamaduni lugha huburudisha Lugha huwa na tabia zifuatazo: Lugha huzaliwa:
  • Lugha za Kibantu ni kundi la lugha ambalo ni tawi la lugha za Niger - Kongo. Lugha za Kibantu huzungumzwa hasa katika nchi za Nigeria, Kamerun, Guinea ya
  • Lugha rasmi ni lugha iliyopewa cheo maalumu katika nchi fulani. Kwa kawaida ni lugha inayotumiwa hasa na serikali kwa mawasiliano kati ya ofisi zake na
  • Lugha za Kiaustronesia ni familia ya lugha ambazo huzungumzwa katika visiwa vya Pasifiki, vya Asia ya Kusini - Mashariki na kisiwa cha Madagaska. Katika
  • Lugha za Kiniger - Kongo ni familia ya lugha barani Afrika. Katika familia hiyo kuna lugha takriban 1400 zenye wasemaji milioni 370 katika Afrika Magharibi
  • Lugha za Kivuka - Guinea Mpya pia Lugha za Kitrans - Niugini ni familia kubwa ya lugha ambazo huzungumzwa katika kisiwa cha Guinea Mpya pande zote mbili
  • Lugha ya kwanza ni lugha ambayo mtu anaiongea kama lugha yake ya kwanza tangu utotoni, umri ambamo ni rahisi zaidi kuathiriwa na mazingira na hivyo pia
  • Lugha za Kisino - Tibeti ni familia kubwa ya lugha ambazo huzungumzwa katika bara ya Asia, hasa nchini Uchina. Idadi ya lugha katika familia hiyo ni zaidi
  • Lugha za Kihindi - Kiulaya ni jamii ya lugha iliyo kubwa kuliko zote duniani. Imekadiriwa kuna lugha hai 445 za jamii hiyo na wasemaji bilioni 3.2 katika
                                     

Lugha za Kiaustronesia

Lugha za Kiaustronesia ni familia ya lugha ambazo huzungumzwa katika visiwa vya Pasifiki, vya Asia ya Kusini-Mashariki na kisiwa cha Madagaska. Katika familia hiyo kuna lugha zaidi ya 1200 zenye wasemaji milioni 386. Lugha ya Kiaustronesia yenye wasemaji wengi zaidi ni Kimalay ambayo huzungumzwa na watu milioni 180.

                                     

Lugha za Kivuka-Guinea Mpya

Lugha za Kivuka-Guinea Mpya ni familia kubwa ya lugha ambazo huzungumzwa katika kisiwa cha Guinea Mpya pande zote mbili nchini Indonesia na nchini Papua Guinea Mpya. Idadi ya lugha katika familia hiyo ni zaidi ya 300.

                                     

Lugha za Kisino-Tibeti

Lugha za Kisino-Tibeti ni familia kubwa ya lugha ambazo huzungumzwa katika bara ya Asia, hasa nchini Uchina. Idadi ya lugha katika familia hiyo ni zaidi ya 400.

                                     

Lugha za Kinilo-Sahara

Lugha za Kinilo-Sahara ni familia ya lugha za barani Afrika ambayo ni kati ya zile muhimu zaidi duniani. Hata hivyo, si wataalamu wote wanakubali familia hiyo. Katika familia hiyo kuna lugha takriban 200 zenye jumla ya wasemaji milioni 50-60 katika nchi 17, zikiwemo Algeria, Libya, Misri, Chad, Mali, Niger, Benin, Sudan, Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Afrika Mashariki, k.m. Kijaluo na Kimaasai.

                                     

Siku ya kimataifa ya lugha ya alama

Siku ya kimataifa ya lugha ya alama husherehekewa tarehe 23 Septemba kila mwaka ikiambatana na wiki ya viziwi duniani. Kuachaguliwa kwa tarehe 23 Septemba kunaendana moja kwa moja na tarehe ya kuanzishwa kwa shirikisho la wasiosikia duniani World Federation of the Deaf lililoanzishwa mwaka 1951.

                                     

Tarihi

Tarihi ni hadithi zinazosimulia kuhusiana na matukio ya kihistoria. Matukio hayo huweza kuwa ya kweli au ya kubuni, lakini huwakilishwa kisanaa ili kuwa ya kuvutia watu. Mara nyingi wahusika wake ni binadamu, lakini hupewa uwezo mkubwa au mdogo sana kutegemea na tukio linalosimulia. Mambo yanayosimulia katika tarihi ni kama vile: mafuriko n.k njaa, maafa,

                                     

Tashtiti

Tashtiti ni mbinu ya kuuliza swali kwa jambo ambalo unafahamu jibu lake, na hufanya hivyo kwa lengo la kusisitiza jambo, kuleta mshangao, n.k. Mfano Ikiwa mtu kapoteana na rafiki yake kwa muda mrefu, halafu ghafla wanakutana, huweza kumwuliza "Aisee! ni wewe?", hali anajua kuwa ni yeye.

                                     

Vipera vya semi

Vipera vya semi vimeundwa na vitu vifuatavyo: Nahau Misemo Vitendawili Mafumbo Methali maneno yenye sehemu mbili, ambapo upande wa kwanza unauliza na upande wa pili unajibu. Kwa mfano: Mwenda pole - hajikwai. Lakabu jina la kupanga analojipa au analopewa mtu kutokana na sifa fulani alizonazo kimaumbile ama kiutendaji. Mizungu