ⓘ Maumbile asilia na mazingira

Gesijoto

Gesijoto ni aina za gesi katika angahewa ya dunia zenye uwezo wa kuathiri mnururisho wa infraredi yaani wa joto. Ni sababu muhimu ya kupanda kwa halijoto duniani.

Mageuko ya spishi

Mageuko ya spishi ni nadharia ya kisayansi iliyobuniwa na kutumiwa na wataalamu wa biolojia, hasa tawi la jenetikia. Inasema ya kwamba spishi za viumbehai zilizopo duniani leo zimetokana na spishi zilizokuwa tofauti za zamani. Nadharia hii inategemea hoja ya kwamba awali uhai wote ulitokana na maumbo asilia. Katika wazo hili spishi zote jinsi zilivyo sasa zinaendelea kubadilika kutoka mifumo rahisi ya maisha kuelekea mifumo kamili zaidi. Mabadiliko hayo huonekana hasa pale ambapo viumbe vizalia huwa na sifa tofauti na zile za wazazi wao. Sifa hizi ni ishara za jeni ambazo hupitishwa kutoka ...

Biolojia

Biolojia ni sayansi asilia inayohusu utafiti wa uhai na viumbehai, kama vile mimea, wanyama, kuvu, bakteria na virusi, na jinsi vinavyohusiana kati yao na katika mazingira yao, pamoja na muundo wao, kazi, ukuaji, asili, mageuko, uenezi, na nadharia ya uainishaji. Biolojia ni somo kubwa mno lenye matawi, mada na masomo mengi. Miongoni mwa mada muhimu zaidi kuna kanuni unganishi tano ambazo zinasemekana kuwa misingi yenye hakika na dhahiri ya biolojia ya kisasa: Spishi mpya na sifa bainishi za kurithiwa hutokana na mageuko Jeni ni vitengo vya msingi vya urithi Viumbe hai hula na kugeuza nish ...

Mkoa wa Magharibi (Kenya)

Mkoa wa Magharibi ulikuwa mojawapo ya mikoa ya utawala ya Kenya nje ya Nairobi, ukiwa mkoa mdogo zaidi kati ya mikoa ya Kenya, lakini pia mkoa wenye msongamano mkubwa wa watu. Ulipakana na Uganda na mikoa ya Kenya ya Nyanza na Bonde la Ufa. Eneo lake lilikuwa km² 8.285 pekee na wakazi 3.569.400, hivyo ulikuwa na zaidi ya watu 400 kwa kila kilomita ya mraba. Wakazi wa Magharibi ni hasa Abaluhya Waluhya. Maadili ya Quakers ni maarufu sana hapa. Makao makuu yalikuwa Kakamega. Mkoa ulienea kutoka vilima vya Bungoma mpakani wa Uganda hadi tambarare karibu na Ziwa Viktoria. Mlima mkubwa wa pili ...

Bakteria

Bakteria au vijasumu ni viumbehai vidogo sana aina ya vidubini. Mwili wa bakteria huwa na seli moja tu. Huonekana kwa hadubini tu na kwa sababu hiyo hazikujulikana katika karne za kale. Kuna aina nyingi sana za bakteria na idadi yao ni kubwa kushinda viumbe vingine vyote duniani. Huishi kwenye ardhi na kwenye maji, ziko pia hewani zinaposukumwa na upepo. Aina nyingi huishi ndani ya viumbe vikubwa zaidi. Mwanadamu huwa na bakteria nyingi ndani ya utumbo wake ambazo ni za lazima kwa mmengenyo wa chakula. Hata katika ngozi kuna bakteria nyingi ambazo zinakinga mwili dhidi ya vidubini vilivyo ...

Utamaduni

Utamaduni ni jinsi binadamu anavyokabili maisha katika mazingira yake. Hiyo inajumlisha ujuzi, imani, sanaa, maadili, sheria, desturi n.k. ambavyo mtu anajipatia kama mwanajamii. Kama sifa maalumu ya binadamu, inayomtofautisha na wanyama, utamaduni ni suala la msingi katika anthropolojia, ukihusisha yale yote yanayopokezwa katika jamii fulani, kama vile lugha inayounganisha watu wanaohusika nao, fasihi, mafungamano, ndoa, michezo, ibada, sayansi na teknolojia. Utamaduni ulioendelea unaitwa pia "ustaarabu". Kila utamaduni unabadilikabadilika mfululizo: ndani ya watu husika, baadhi wanachang ...

Jenetikia

Jenetikia ni tawi la biolojia linalochunguza uritishano na mwachano wa viumbe hai. Kwa namna ya pekee imegundulika kwamba chembechembe zinazohifadhi taarifa za urithi wa viumbe hai zimo katika kiini cha kila seli yao kama nyuzinyuzi zinazoitwa kromosomu. Hizo zinabeba jeni kadhaa ambazo kila mojawapo inahusika na urithi wa tabia na umbile fulani kutoka kwa wazazi kwenda kwa kizazi kipya. Ukweli kwamba viumbe hai hurithi sifa kutoka kwa wazazi wao umetumika tangu zamani za kale kuboresha mazao ya mimea na wanyama kwa njia ya uzalishaji teuzi. Hata hivyo, sayansi ya kisasa ya jenetikia, amba ...

Ulevi

Ulevi, ujulikanao pia kama uraibu wa pombe, ni ulemavu tegemevu wa kudhuru. Dalili zake ni unywaji pombe kupindukia bila udhibiti pombe licha ya madhara yake hasi kwa afya ya mnywaji, mahusiano na hadhi yake machoni pa jamii. Kama matatizo mengine ya kiafya, ulevi ni mojawapo ya magonjwa yanayoweza kutibika. neno ulevi" limetumika kwa muda mrefu tangu kubuniwa mwaka wa 1849 na Magnus Huss, ila katika nyanja ya utabibu istilahi hii iligeuzwa kuwa "utumiaji pombe vibaya" na utegemezi pombe" katika miaka ya 1980 DSM III. Aidha mwaka wa 1979 kamati ya wataalamu ya Shirika la Afya Duniani haiku ...

Madhara ya ongezeko la joto duniani

Madhara ya ongezeko la joto duniani na mabadiliko ya hali ya hewa ni mada muhimu sana, hasa kwa mazingira na maisha ya binadamu. Ushahidi unaoonyesha mabadiliko ya hali ya hewa ni pamoja na rekodi muhimu ya kipimo joto, kupanda kwa maeneo ya bahari, na kupungua kwa kiwango kilichofunikwa na theluji katika ulimwengu. Kulingana na Ripoti ya Uchunguzi ya Nne ya IPCC, "nyingi" kati ya maongezeko ya vipimo vya joto vya wastani duniani tangu katikati ya karne ya 20 huenda ikawa ni kwa sababu ya ongezeko tunaloliona la wingi wa gesi ya hewaukaa inayotokana na binadamu". Inatibiriwa kuwa mabadilik ...

Anthropolojia ya Kimarekani

Anthropolojia ya Kimarekani ni aina ya anthropolojia inayozingatia hasa wazo la utamaduni ambao ulifafanuliwa kama uwezo wa kiubia wa binadamu wa kuainisha na kusimbika tajiriba zao kiishara na kuwasilisha kiishara tajiriba zilizosimbikwa kijamii. Anthropolojia ya Kimarekani imepangiliwa katika mawanda manne. Kila mojawapo huchangia sana utafiti wa utamaduni. Mawanda yenyewe ni: anthropolojia ya kibiolojia, isimu, anthropolojia ya kiutamaduni, na akiolojia. Utafiti katika mawanda haya umewaathiri kwa kiwango fulani wanaathropolojia wanaofanya kazi katika nchi zingine.

Dawa za mfadhaiko

Dawamfadhaiko ni dawa za ugonjwa wa akili zinazotumika kupunguza mivurugo ya halihisi ya moyo, kama vile mfadhaiko mkubwa na ukataji tamaa na hali ya wasiwasi kama vile woga wa kuingiliana na watu. Dawa kama vile vizuia oksidesi vya monoamini, dawa dhidi ya mfadhaiko aina ya trisaikliki, dawa dhidi ya mfadhaiko aina ya tetrasaikliki, vizuizi vya uchukuzi wa serotonini kinachochagua, na vizuizi vya uchukuzi wa serotonini-norepinefrini ndizo zinazohusishwa kwa kawaida na neno hilo. Dawa hizo ni kati ya zile ambazo kwa kawaida huagizwa na wataalamu wa magonjwa ya akili na madaktari wengine, n ...

                                     

ⓘ Maumbile asilia na mazingira

  • Kuna gesijoto asilia na pia gesijoto zilizoongezwa na binadamu. Kuwepo kwa gesijoto si jambo baya maana binadamu na maumbile asilia yote vilitokea katika
  • makundi ya viumbe kutokana na mabadiliko katika jeni za viumbe hao, mabadiliko ya maumbile na vyanzo vingine vya mabadiliko ya maumbile Mageuko hufanyika wakati
  • asilia inayohusu utafiti wa uhai na viumbehai, kama vile mimea, wanyama, kuvu kama uyoga bakteria na virusi, na jinsi vinavyohusiana kati yao na katika
  • maskini na wanaume wengi wamekwenda Nairobi au kwenye hoteli za pwani kwa kazi ya ajira. Mkoa wa Magharibi una maumbile mbalimbali ya mazingira kuanzia
  • kiasi kikubwa cha seli kwa bei nafuu na kwa haraka. Hata hivyo, katika mazingira ya asilia rutuba ni adimu na kwa hivyo ina maana kuwa bakteria haziwezi
  • hayakufungamana na maumbile Dhana ya utamaduni katika Anthropolojia ya Kimarekani ilikuwa na maana mbili: 1 Uwezo wa binadamu wa kuainisha na kuwasilisha