ⓘ Sayansi

UNESCO

UNESCO ni kifupisho cha United Nations Educational, Scientific and Cultural Organization yaani Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa. Ni kitengo cha Umoja wa Mataifa ambacho kinashughulika habari za elimu, sayansi na utamaduni duniani. Kisheria UNESCO ni shirika la kujitegemea lenye madola wanachama 191. Kati ya shughuli muhimu za UNESCO mojawapo ni Orodha la Urithi wa Dunia linalojumlisha mahali penye umuhimu wa pekee kihistoria, kisayansi au kiutamaduni. Nchi zote zina mahali angalau moja orodhani, nyingine zina pengi, hasa Italia na Hispania.

Kamusi Awali ya Sayansi na Tekinologia

KAST ni kifupi chake cha Kamusi Awali ya Sayansi na Tekinologia iliyoandaliwa na wataalamu wa TUKI na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1995. Kamusi hii inakusanya maneno ya kisayansi na ya kiteknolojia kwa utaratibu ufuatao: neno la Kiswahili maana yake kwa Kiingereza katika mabano maelezo yake kwa Kiswahili Mwishowe kuna faharasa ya Kiingereza inayoweza kutumiwa kama kamusi ndogo ya Kiingereza-Kiswahili ya maneno ya kisayansi. Kati ya kamusi za Kiswahili hii ni hatua kubwa mbele katika ukuzaji wa Kiswahili hata ikionyesha bado mapengo na kasoro mbalimbali. Hali halisi kuna kiasi kikubwa ...

Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia

Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia) ilikuwa wizara ya serikali nchini Tanzania iliyoanzishwa mwaka 2008. Ilitanguliwa na Ministry of Higher Education, Science and Technology, iliyoitwa Ministry of Science, Technology and Higher Education kabla ya mwaka 2005. Ofisi kuu ya wizara hii zilikuwa jijini Dar es Salaam. Mwaka 2015 wizara hiyo ilifutwa na idara zake kugawiwa kati ya Wiraza ya Elimu na Idara ya Kazi. Katika baraza ya mawaziri ya pili chini ya rais Magufuli wizara ilianzishwa upya mwaka 2020.

Upatanisho wa imani na sayansi

Upatanisho wa imani na sayansi ni juhudi zinazofanywa na watu wa dini mbalimbali kuondoa mzozo uliotokea kati ya imani na sayansi, hasa kuhusu suala la uumbaji kuhusiana na mageuko ya spishi. Juhudi hizo zinaitwa pengine kwa Kiingereza: theistic evolution, theistic evolutionism, evolutionary creationism, divine direction, au God-guided evolution. Ieleweke mapema kwamba juhudi hizo hazilengi kutunga au kupitisha nadharia yoyote katika sayansi, ila kuonyesha uwezekano wa kukubali kweli zilizothibitishwa na utafiti wa sayansi pamoja na kweli zilizosadikiwa kwa kupokea ufunuo wa Mwenyezi Mungu ...

Sayansi ya kilimo

Sayansi ya kilimo ni tawi la biolojia linalojumuisha sehemu za elimu mbalimbali zinazotumiwa katika kilimo. Mara nyingi hugawiwa katika elimu ya kilimo cha mimea, elimu ya mifugo na uchumi wa kilimo. Tiba ya mifugo mara nyingi haihesabiwi humo.

Fizikia

Fizikia ni fani ya sayansi inayohusu maumbile ya ulimwengu, hususan asili ya dunia na viumbe vyote. Ni taaluma yenye kushughulika na maada na uhusiano wake na nishati. Fizikia imetoa mchango mkubwa katika sayansi, teknolojia na falsafa.

                                     

ⓘ Sayansi

 • wa sayansi ya kisasa. Kuna sayansi mbalimbali ambazo huainishwa katika makundi yafuatayo: Sayansi Asili k.m. Biolojia Jiografia Zoolojia Sayansi Umbile
 • Sayansi ya jamii ni somo kuhusu jamii za binadamu. Ni sayansi ya kijamii ambayo hutumia mbinu mbalimbali za uchunguzi kwa kupima ili kutengeneza na kusafisha
 • Sayansi bandia kwa Kiingereza: Pseudoscience ni imani inayojidai kuwa sayansi lakini si sayansi kwa sababu haitumii njia za kisayansi. Kiputiputi, O
 • Sayansi ya tarakilishi ni sayansi kuhusu programu, data na maarifa. Mwanasayansi wa tarakilishi anasoma programu na nadharia ya tarakilishi.
 • Wizara ya Elimu, Sayansi Teknolojia na Ufundi Tanzania kwa Kiingereza: Ministry of Education, Science, Technology and Vocational Training kifupi ni
 • Sayansi za dunia nu jumla ya sayansi zinazochungulia maumbile na sifa za dunia yetu au sayari tunapoishi. Kuna matawi manne makuu yanayoshughulikia utafiti
 • Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa. Ni kitengo cha Umoja wa Mataifa ambacho kinashughulika habari za elimu, sayansi na utamaduni duniani
 • KAST ni kifupi chake cha Kamusi Awali ya Sayansi na Tekinologia iliyoandaliwa na wataalamu wa TUKI na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1995. Kamusi
 • Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania Kiingereza: Tanzania Commission for Science and Technology kifupi COSTECH ni shirika la umma ambalo linashirikiana
 • Upatanisho wa imani na sayansi ni juhudi zinazofanywa na watu wa dini mbalimbali kuondoa mzozo uliotokea kati ya imani na sayansi hasa kuhusu suala la
 • Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kwa Kiingereza: Ministry of Science, Information and Technology kifupi COSTECH ilikuwa wizara ya serikali
 • Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya ni chuo kikuu cha umma kinachopatikana katika jiji la Mbeya, Tanzania. Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia
                                     

Sayansi bandia

Kiputiputi, O. M. 2001. Kufundisha sayansi kwa Kiswahili. Mdee, JS and Mwansoko, HJM, Makala ya kongamano la kimataifa KISWAHILI 2000 Proceedings. Dar-es-Salaam: Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili

                                     

Sayansi za dunia

Sayansi za dunia nu jumla ya sayansi zinazochungulia maumbile na sifa za dunia yetu au sayari tunapoishi. Kuna matawi manne makuu yanayoshughulikia utafiti huu ni jiodesia jiofizikia jiolojia jiografia Yote hutumia matokeo na mbinu za masomo kama fizikia, kemia, biolojia na hisabati na kuyatumia kwa upimaji na utafiti wa dunia yetu.

                                     

Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania

Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania ni shirika la umma ambalo linashirikiana na serikali ya Tanzania. Ilianzishwa kwa agizo la Bunge la Tanzania mnamo mwaka wa 1986 ikiwa kama mpokezi wa Baraza la Sayansi na Utafiti Tanzania. Tume hii ni tawi la taasisi na Wizara ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia. Ofisi zake kuu zipo mjini Dar es Salaam.

                                     

Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya

Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya ni chuo kikuu cha umma kinachopatikana katika jiji la Mbeya, Tanzania. Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya zamani kilijulikana kama chuo cha ufundi Mbeya.

                                     

Audiolojia

Audiolojia ni kiwanja cha sayansi kinachohusika na masomo kuhusu sikio, kusikia na magonjwa ya masikio. Wanaaudiolojia hutumia ujuzi wao, kupeleleza kiwango cha kusikia cha mtu binafsi na kama kuna tatizo, huweza kujua tatizo liko wapi na pia hueleza matibabu yepi yanawezekana au yanapatikana.

                                     

Jaribio

Jaribio ni taratibu zinazofuatwa ili kuthibitisha, kukanusha au kuhalalisha makisio. Majaribio yanatofautiana sana katika malengo na vipimo, lakini kwa kawaida hutegemea na kurudiwa kwa taratibu husika na uchambuzi yakinifu wa matokeo yaliyopatikana. Mtoto anaweza kufanya majaribio ya msingi ili kuelewa uzito, lakini kundi la wanasayansi wanaweza kuchukua miaka mingi kufanya uchunguzi kuongeza uelewa wao kuhusu jambo fulani.

                                     

Jiofizikia

Jiofizikia ni fani ya sayansi ya miamba na dutu nyingine zinazounda dunia, pamoja na muundo wa kimaumbile uliomo duniani, ndani yake na juu ya uso wake.

                                     

Kiwango utatu

Kiwango utatu ni kiwango cha maji au dutu nyingine inapoweza kutokea mahali pamoja katika hali mango, kiowevu na gesi. Kiwango hiki kinategemea halijoto na shindikizo. Kiwango utatu cha maji ni kiwango cha kukadiria skeli ya selsiasi au sentigredi 273.16 K au 0.01 °C.

                                     

Mfululizo

Katika hisabati, mfululizo ni tendo la kihesabu la kujumlisha lisilo na mwisho toka idadi inayoanza. Mfululizo hutumika katika utarakilishi.

                                     

Mwanasayansi

Mwanasayansi ni mtu anayejihusisha na shughuli maalumu ili kupata maarifa. Kwa maana pana zaidi, mwanasayansi anaweza kutajwa kama mtu anayetumia mbinu za kisayansi. Mtu huyo anaweza kuwa mtaalamu katika eneo moja au zaidi ya sayansi. Wanasayansi hufanya utafiti kuelekea uelewa mkubwa zaidi wa uasilia, ikiwa ni pamoja na ulimwengu kimwili, kihisabati na kijamii. Kwa kawaida wanasukumwa na udadisi wao.

                                     

Nyuklia

Nyuklia ni neno ambalo linatumiwa katika lugha ya sayansi. Asili yake ni Kilatini "nucleus" inayomaanisha "kiini". Inatumiwa hasa kama tafsiri ya Kiingereza "nuclear". Kwa Kiswahili neno hili linatumiwa hasa katika fani za fizikia kwa kutaja mambo yanayohusu kiini cha atomu, na pia biolojia kwa mambo yanayohusu kiini cha seli. Nyuklia inaweza kutaja:

                                     

Stellarium (Programu)

Stellarium ni programu ya bure yenye leseni ya matumizi ya bure kwa umma. Ni programu nzuri na mahususi kwa kuona anganje kupitia kompyuta au simu ya mkononi. Programu hii inasaidia katika mambo ya astronomia na unajimu.