ⓘ Elimu

Elimu

Elimu kwa maana pana ni tendo au uzoefu wenye athari ya kujenga akili, tabia ama uwezo wa kimaumbile wa mtu binafsi. Katika dhana ya kiufundi, elimu ni njia ambayo hutumiwa makusudi na jamii kupitisha maarifa, ujuzi na maadili kutoka kwa kizazi kimoja hadi kingine. Walimu katika taasisi za elimu huratibisha elimu ya wanafunzi wao kupitia masomo kama vile ya kuandika, kusoma, kuhesabu hisabati, sayansi na historia. Mbinu hii wakati mwingine huitwa masomo haswa tunaporejelea somo la aina fulani, kwa kawaida mbinu hii hutumiwa na maprofesa katika taasisi za masomo ya juu. Kuna elimu maalumu k ...

Elimu nchini Kenya

Elimu nchini Kenya imekuwa ikizingatia mfumo wa 8-4-4 tangu mwishoni mwa miaka ya 1980, ikiwa ni miaka minane ya elimu ya msingi, ikifuatiwa na miaka minne ya shule ya upili, kisha miaka minne ya chuo au chuo kikuu. Mbali na haya, kuna sekta kubwa ya shule za binafsi ambazo hushughulikia watu wa viwango vya maisha ya kadri na ya juu, ambao kwa ujumla hufuata mfumo wa elimu ya Uingereza wa elimu ya sekondari na msingi. Kati ya watoto wote nchini Kenya, asilimia 85 huudhuria shule za msingi, asilimia 24 huudhuria shule za upili na asilimia 2 hujiunga na taasisi za elimu ya juu.

Elimu katika Afrika

Elimu katika Afrika ilianza kama chombo cha kuandaa vijana wake kuchukua nafasi yao katika jamii ya Afrika. Uzoefu wa elimu ya Kiafrika ilianzishwa hasa kuandaa vijana kwa jamii katika jamuiya ya Kiafrika na si kwa maisha nje ya Afrika. Mfumo wa shule ya awali ya ukoloni wa Ulaya ilijumuisha makundi ya watu wakubwa, wao wakifundisha vipengele na tamaduni ambazo zingeweza kuwasaidia wakiwa watu wazima. Elimu katika jamii ya awali ya Kiafrika ilijumuisha mambo kama sanaa, sherehe, michezo, matamasha, dansi, kuimba, na kuchora. Wavulana na wasichana walifunzwa kama wametenganishwa kusaidia ku ...

Elimu ya sekondari

Elimu ya sekondari, katika mifumo ya kisasa ya elimu ulimwenguni, huchukua kipindi cha pili cha elimu rasmi ambayo hutokea wakati wa ujana wa wanafunzi. Mfumo huu hutofautiana na masomo ya msingi ambayo ni ya lazima, ni ya jumla na yanayofanana. Yale ya shule za upili ni teule na ya hiari. Shule hizi hujulikana kama sekondari, shule za upili, shule za kati, vyuo au shule za ujuzi wa kitaalamu kulingana na kipindi au mfumo unaofuatwa. Maana ya dhana hizi hutofautiana kutoka mfumo mmoja hadi mwingine. Mpaka kamili kati ya elimu ya msingi na ya upili hutofautiana kutoka nchi moja hadi nyingin ...

Elimu ya juu

Elimu ya juu, yaani ile ya baada ya shule ya upili au elimu ya awamu ya tatu, si ya lazima. Elimu hii kwa kawaida hujumulisha viwango vya shahada pamoja na elimu ya ujuzi wa kitaalamu. Kwa jumla elimu ya juu hutolewa na vyuo na vyuo vikuu na huambatana na kutolewa kwa vyeti, stashahada za diploma na shahada za digrii kitaaluma. Masomo ya juu hujumuisha elimu, utafiti na huduma za jamii na katika uwanja wa elimu, hujumulisha viwango vya shahada ya kwanza na nyingine za juu. Elimu ya juu aghalabu huhusu kufuzu katika kiwango cha shahada ya kwanza, ya uzamili na ya uzamifu. Idadi kubwa ya wat ...

Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi

Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Tanzania kifupi ni wizara ya serikali inayoshughulikia masuala ya uanzishaji na uboresheji wa elimu, elimu ya juu katika sayansi na teknolojia nchini Tanzania pamoja na mafunzo ya ufundi. Ofisi kuu ya wizara hii ipo mjini Dodoma.

                                     

ⓘ Elimu

  • Elimu kwa maana pana ni tendo au uzoefu wenye athari ya kujenga akili, tabia ama uwezo wa kimaumbile wa mtu binafsi. Katika dhana ya kiufundi, elimu ni
  • Elimu nchini Kenya imekuwa ikizingatia mfumo wa 8 - 4 - 4 tangu mwishoni mwa miaka ya 1980, ikiwa ni miaka minane ya elimu ya msingi, ikifuatiwa na miaka minne
  • Elimu katika Afrika ilianza kama chombo cha kuandaa vijana wake kuchukua nafasi yao katika jamii ya Afrika. Uzoefu wa elimu ya Kiafrika ilianzishwa hasa
  • Elimu ya sekondari shule za upili katika mifumo ya kisasa ya elimu ulimwenguni, huchukua kipindi cha pili cha elimu rasmi ambayo hutokea wakati wa ujana
  • Elimu ya juu, yaani ile ya baada ya shule ya upili au elimu ya awamu ya tatu, si ya lazima. Elimu hii kwa kawaida hujumulisha viwango vya shahada pamoja
  • Wizara ya Elimu Sayansi, Teknolojia na Ufundi Tanzania kwa Kiingereza: Ministry of Education, Science, Technology and Vocational Training kifupi ni
  • Masomo ya msingi huchukua kati ya miaka 5 hadi 8 ya kwanza ya elimu rasmi. Kwa jumla elimu ya juu hujumulisha miaka 6 - 8 ya masomo kuanzia mwaka wa tano
  • Elimu nchini Tanzania hutolewa na sekta zote mbili, yaani, sekta za serikali na binafsi. Muundo wake kiujumla ni kama ifuatavyo: Miaka 2 elimu ya vidudu cheke - chea
  • serikali zinazoitwa Wizara ya Elimu au Wizara ya Elimu ya Umma Wizara ya kwanza kabisa inafikiriwa kuwa Tume ya Taifa ya Elimu pl. Komisja Edukacji Narodowej
                                     

Elimu (kipaji)

Elimu kama kipaji cha Roho Mtakatifu ni utayari wa Mkristo kuangaziwa na Roho Mtakatifu kuhusu mambo ya duniani ili kuelewa kasoro zake. Hivyo haitegemei akili wala elimu ya kawaida. Elimu ni kipaji cha Roho Mtakatifu kinachotutia maarifa ya mambo ya ulimwengu huu, kwa kutambua mapungufu yake pamoja na mitego, werevu na udanganyifu wa shetani akitujaribu mwenyewe au kwa kupitia vitu kama watu.

                                     

Chekechea

Chekechea, maana yake ni kitu kidogo, hivyo pia watoto wadogo. Neno hilohilo linatumika pia kwa vituo vya kuwalea kwa Kiingereza "kindergarten", yaani "bustani ya watoto". Ndiyo hatua ya kwanza kuelekea elimu rasmi. Watoto katika vituo hivyo wanajifunza kupitia michezo mbalimbali. Umri wao kwa kawaida ni kati ya miaka 3 na 7.

                                     

Cheti

Cheti ni hati anayopewa mtu kwa ajili ya kutambuliwa kuwa ana sifa fulani. Cheti huweza kutolewa kwa mtu aliyehitimu mafunzo fulani au aliyefanikiwa kwa jambo fulani. Vyeti vingi hutolewa kama tuzo kwa mtu aliyefanikiwa kuhusu jambo fulani. Vyeti vipo vya aina mbalimbali, kuna vyeti vya kitaaluma, vya kuzaliwa, vya ndoa au vya kimichezo.

                                     

Elimu ya watu wazima

Elimu ya watu wazima huchukua maumbo mengi, yakiwemo elimu rasmi darasani, elimu ya binafsi na masomo ya mtandao. Idadi fulani ya kozi za kazi maalumu, kama vile elimu ya mifugo, masuala ya madawa, uwekezaji, uhasibu na kozi nyinginezo kwa sasa hupatikana mtandaoni. Elimu hii imekuwa kawaida katika nchi nyingi. Kwa muda mrefu Tanzania ilikuwa kielelezo kwa Afrika nzima.

                                     

Madrasa

Madrasa katika Kiswahili ni mahali panapotolewa mafunzo ya Kurani kwa watoto wa Kiislamu. Mara nyingi yanapatikana karibu na mskiti.

                                     

Mahafali

Mahafali ni sherehe ya wanafunzi kupata diploma au shahada ya kitaaluma au sherehe ambayo wakati mwingine huhusishwa na kuhitimu masomo. Tarehe ya mahafali mara nyingi huitwa siku ya kuhitimu.

                                     

Mtaalamu

Mtaalamu mara nyingi humaanisha mtu ambaye ni bingwa katika taaluma fulani. Mtaalamu anaaminika katika fani yake kama chanzo cha ujuzi au maarifa. Utaalamu huo unaweza kutegemea elimu, lakini pengine pia malezi, ufundi, maandishi au mangamuzi yake. Kihistoria, mtaalamu aliweza kuitwa mzee wa hekima. Mtu huyo kwa kawaida alikuwa na uwezo mkubwa upande wa akili pamoja na busara katika maamuzi.

                                     

Muhula

Muhula ni kipindi cha mwaka wa masomo katika kalenda ya shule au taasisi ya elimu ambacho kinaonyesha muda ambao wanafunzi watakuwa shule na muda wa likizo. Katika mfumo wa elimu ya Tanzania kuna mihula mikuu miwili 2. Katika shule za msingi muhula wa kwanza unaanza mwezi Januari mpaka Juni. Na muhula wa pili unaanza mwezi Julai mpaka wa Desemba.

                                     

Nadharia

Nadharia ni mkusanyo wa taarifa mbalimbali zenye ukweli ndani yake bila kuegemea upande fulani. Katika lugha nyingi za Ulaya, neno hili asili yake ni katika Kigiriki cha kale lakini kwa matumizi ya kisasa imechukua maana kadhaa zenye kuhusiana nalo. Nadharia zinaongoza shughuli za kupata ukweli badala ya kufikia malengo, na huwa haiegemei upande wowote. Nadharia inaweza kuwa jumla ya ujuzi ambao unaweza au usiweze kuambatana na mafunzo ya kimatendo. Kuunda nadharia ni kutengeneza ujuzi.

                                     

Siku ya Elimu Duniani

Siku ya Elimu Duniani ni siku ya kimataifa ya maadhimisho ya elimu duniani inayofanyika 24 Januari kila mwaka kwa ajili ya kuhamasisha elimu. Tarehe 3 Desemba 2018 Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa ulipitisha na kuitangaza 24 Januari kuwa siku ya elimu kimataifa na husherehekewa katika kuidumisha misingi ya elimu na kuleta amani ya dunia pamoja na kusimamia maendeleo endelevu.