ⓘ Familia

Familia

Familia ni kikundi cha watu wanaokaa pamoja kama baba, mama na watoto. Kikundi hicho mara yingi ni sehemu ya kundi kubwa zaidi la ukoo unaounganisha watu wenye asili katika uzazi wa pamoja.

Familia (biolojia)

Familia ni ngazi katika uainishaji wa kisayansi wa viumbehai. Familia ya wanyama au mimea hujumlisha spishi mbalimbali zilizo karibu. Kwa mfano paka-kaya ni spishi mojawapo pamoja na spishi 41 nyingine ndani ya familia ya Felidae inayojumlisha paka pamoja na chui, simba, tiger n.k. Ndani ya familia kuna jenasi mbalimbali zinazojumlisha spishi za karibu zaidi; kila familia ni sehemu ya ngazi ya juu zaidi inayoitwa oda. Familia ya Felidae wanyama wanaofanana na paka ni sehemu ya oda ya Carnivora yaani wanyama walanyama. Kwa kawaida majina ya kisayansi ya kila familia huishia kwa - "idae" kam ...

Familia takatifu

Familia takatifu katika Ukristo ni hasa ile iliyoundwa na Mtoto Yesu, Bikira Maria na mtakatifu Yosefu. Kwa imani ya Wakristo ni kwamba Mungu alipomtuma Mwanae pekee kujifanya mtu hakutaka azaliwe nje ya familia, kwa kuwa hiyo ndiyo mpango wake asili kwa ajili ya watu tangu alipoumba Adamu na Eva akawabariki wazaliane. Heshima kwa Familia takatifu katika Kanisa Katoliki ilianzishwa rasmi na Fransisko wa Laval, askofu wa kwanza wa New France Kanada katika karne ya 17.

Familia nyuklia

Familia nyuklia ni familia iliyoundwa na wazazi wawili na watoto wao. Ni tofauti na familia pana, inayohusisha ndugu wengi wa wazazi, na aina nyingine za familia.

Sheria ya Familia

Sheria za familia ni sehemu za sheria ambazo zinahusika na masuala ya familia na mahusiano ya ndani ikiwa ni pamoja na: Kikomo cha uhusiano pamoja na talaka, mali, wajibu wa mzazi kwa watoto). Masuala yanayojitokeza katika ndoa, ikiwa ni pamoja na dhuluma, uhalali, watoto, na dhuluma kwa mtoto. Asili ya ndoa, vyama vya muungano, na ushirikiano wa nyumbani; Sheria za familia zinaweza pia kuashiria mkataba wa ndoa katika imani ya Kiislamu, ambayo inaruhusu wanaume kuoa wake hadi wanne.

Detepwani (familia)

Detepwani ni ndege wa nusufamilia Cerylinae katika familia Alcedinidae. Spishi kubwa zinaitwa mkumburu au zumbulu. Wanafanana na midiria lakini spishi nyingi ni wakubwa zaidi na zote zina kishungi. Kwa kweli baina ya spishi hizi kuna zile kubwa kabisa za familia hii, lakini American pygmy kingfisher ni mdogo sana. Takriban spishi zote zina rangi ya majani ya metali mgongoni na nyekundu kidarini, lakini detepwani wa kawaida ni mweusi na mweupe tu. Detepwani hubobea katika kukamata samaki lakini hula gegereka, vyura na wadudu pia. Huchimba tundu katika ukingo wa mto ambalo ndani lake jike hu ...

                                     

ⓘ Familia

 • Familia kutoka Kilatini familia ni kikundi cha watu wanaokaa pamoja kama baba, mama na watoto. Kikundi hicho mara yingi ni sehemu ya kundi kubwa zaidi
 • Familia ni ngazi katika uainishaji wa kisayansi wa viumbehai. Familia ya wanyama au mimea hujumlisha spishi mbalimbali zilizo karibu. Kwa mfano paka - kaya
 • Familia takatifu katika Ukristo ni hasa ile iliyoundwa na Mtoto Yesu, Bikira Maria na mtakatifu Yosefu. Kwa imani ya Wakristo ni kwamba Mungu alipomtuma
 • Familia pana kwa Kiingereza extended family ni jamii iliyoundwa na ndugu wa vizazi kadhaa, kwa mfano babu, bibi, wazazi na watoto wao, au pia shangazi
 • Familia nyuklia kwa Kiingereza nuclear family, elementary family au conjugal family ni familia iliyoundwa na wazazi wawili na watoto wao. Ni tofauti
 • Sheria za familia ni sehemu za sheria ambazo zinahusika na masuala ya familia na mahusiano ya ndani ikiwa ni pamoja na: Asili ya ndoa, vyama vya muungano
 • Familia inaweza kumaanisha Familia - kama kundi la baba, mama na watoto wanaoishi pamoja Familia biolojia - vikundi vya viumbehai kama wanyama wanaopangwa
 • Detepwani ni ndege wa nusufamilia Cerylinae katika familia Alcedinidae. Spishi kubwa zinaitwa mkumburu au zumbulu. Wanafanana na midiria lakini spishi
 • Lugha za Kiniger - Kongo ni familia ya lugha barani Afrika. Katika familia hiyo kuna lugha takriban 1400 zenye wasemaji milioni 370 katika Afrika Magharibi
 • Familia Lamprophiidae Afrika Familia Prosymnidae Afrika Familia Psammophiidae Afrika, Asia na Ulaya Familia Pseudaspididae Afrika Familia
 • Familia ya Jomo Kenyatta ni jina la kutaja familia ya Rais wa awamu ya 1 wa Kenya. Uhuru Kenyatta
                                     

Familia pana

Familia pana ni jamii iliyoundwa na ndugu wa vizazi kadhaa, kwa mfano babu, bibi, wazazi na watoto wao, au pia shangazi, mjomba, binamu n.k., si wazazi na watoto peke yao kama familia nyuklia. Katika nchi ambazo zinakubali mitara, familia zinaweza kuwa pana zaidi.

                                     

Familia (maana)

Familia inaweza kumaanisha Familia biolojia - vikundi vya viumbehai kama wanyama wanaopangwa pamoja katika uainishaji wa kisayansi Familia - kama kundi la baba, mama na watoto wanaoishi pamoja Kundi mbalimbali za vitu, magimba na kadhalika zinazopangwa pamoja kwa sababu zina tabia za pamoja; wanafalaki wanaweza kujadili "familia za nyota"; wanahisabati hupanga "familia za namba" n.k.

                                     

Lugha za Kiniger-Kongo

Lugha za Kiniger-Kongo ni familia ya lugha barani Afrika. Katika familia hiyo kuna lugha takriban 1400 zenye wasemaji milioni 370 katika Afrika Magharibi, mashariki na kusini. Kundi kubwa hasa ndani ya familia hiyo ni lugha za Kibantu kama Kiswahili.

                                     

Babu

Babu kwa mjukuu wake ni hasa baba wa mzazi wake mmojawapo. Katika DNA anachangia 25%. Inakadiriwa kwamba miaka 30.000 iliyopita idadi ya watu waliofikia umri wa kuona wajukuu wao iliongezeka sana na kuwezesha ushirikishaji wa ujuzi na mangamuzi mbalimbali kuliko awali. Pia babu anaweza kushika nafasi ya baba ikiwa huyo hayupo k.mf. amekufa na kumfaidisha mtoto kimalezi. Hata kama baba yupo, babu anaweza kutoa mchango mzuri katika makuzi ya mtoto.

                                     

Binamu

Binamu ni ndugu wa ukoo tofauti, kwa sababu ni mtoto wa mjomba au wa shangazi, si mtoto wa baba mkubwa, baba mdogo, mama mkubwa wala mama mdogo. Kuhusu mahusiano na uwezekano wa kuoana kuna desturi na sheria tofauti duniani.