ⓘ Isimujamii

Isimujamii

Isimujamii ni tawi la isimu ambalo huchunguza uhusiano kati ya lugha na jamii. Aidha inajihusisha na athira yeyote ya jamii kama vile desturi za watu, matazamio, na muktadha, katika nyanja za lugha namna inavyotumika. Chini ya taaluma hiyo, kuna matawi mengi yanayoshughulikia uchanganuzi wa vipengele fulani vya uhusiano kati ya lugha na jamii, k.m. vipengele mbalimbali vya mawasiliano kupitia maoni ya msemaji tawi hilo pia huitwa isimu amali matumizi ya lugha baina ya jamii za watu tofauti, kama lugha mawasiliano, pijini na krioli matumizi ya lugha tofauti wakati mmoja, kama katika wingilu ...

Isimu

Isimu ni sayansi inayochunguza lugha. Imegawiwa katika matawi mbalimbali: semantiki kuhusu maana isimujamii kuhusu uhusiano kati ya lugha na jamii fonetiki kuhusu sauti zinazotolewa na binadamu mofolojia kuhusu mfumo wa maneno sintaksi kuhusu mfumo wa sentensi fonolojia kuhusu mfumo wa sauti katika lugha fulani

Lahaja

Lahaja ni vilugha vidogovidogo vya lugha moja ambavyo hubainishwa na jamii au jiografia. Lahaja za lugha moja zinakaribiana katika matamshi, miundo ya sarufi na msamiati. Kama lugha hutofautiana katika matamshi tu, tofauti hizo huitwa lafudhi upekee wa uzungumzaji, si lahaja. Uchambuzi na uchanganuzi wa lahaja ni tawi la isimujamii. Lahaja hutofautishwa kulingana na vipengele vifuatavyo: vipengele vya sera lahaja rasmi na lahaja sanifu vipengele vya maoni ya wasemaji wa lugha husika vipengele vya kijamii lahaja jamii na lahaja tabaka vipengele vya eneo Mfano wa lugha yenye lahaja mbalimbal ...

Lahaja sanifu

Lahaja sanifu ni lahaja ambayo imeteuliwa kutoka lahaja nyingine kutumika kwa upana zaidi kuliko lahaja za kawaida. Lahaja sanifu hutumika hasa kwa mawasiliano baina ya wasemaji wa lahaja tofauti za lugha moja; tena, hutumika katika shughuli zilizo rasmi. Ili kuwa sanifu, lahaja teule hufanyiwa marekebisho madogomadogo upande wa matamshi, sarufi na semantiki. Marekebisho hayo yanawezekana kutokea bila watu kujua.

Rejista

Rejista ni matumizi ya lugha kulingana na muktadha maalum. Miktadha tofauti husababisha aina mbalimbali za lugha. Baadhi ya vipengele vya miktadha hiyo ni: Umri Mada Wakati Mazingira Uhusiano baina ya wahusika Cheo Ujuzi wa lugha Tofauti ya kimatamshi Taaluma Kiwango cha elimu Jinsia Lugha anazozijua mtu Mifano ya rejista za lugha ni: lugha ya dini lugha ya biashara lugha ya sheria lugha ya mazungumzo lugha ya sayansi lugha ya Elimu

Ulumbi

Ulumbi, kwa asili ya neno, ni sifa ya matumizi bora ya lugha. Wataalamu mbalimbali wameutumia ulumbi kumaanisha "uhodari wa kutumia lugha ili kufaulisha mawasiliano" au "sifa ya kutumia maneno mengi". Wengine lakini wameutumia sawa na uwingilugha, yaani uwezo wa kutumia lugha mbili au zaidi. Chini ya kipengele cha kwanza cha ulumbi, yaani uhodari wa kutumia lugha, kuna umahiri na umilisi. Chini ya kipengele cha pili cha ulumbi, yaani uwezo wa kutumia lugha nyingi, kuna ujozilugha, ubadilishaji msimbo na diglosia.

Lugha ya taifa

Lugha ya taifa ni lugha au lahaja iliyoteuliwa miongoni mwa lahaja nyingi zilizopo katika jamiilugha fulani iliyopo katika eneo fulani ili itumike katika mawasiliano ya jamii hiyo. Mara nyingi lugha ya Taifa huteuliwa ili kukidhi haja ya mawasiliano miongoni mwa jamii. Lugha ya Taifa inakuwa kama nembo ya Taifa husika, hii inachangiwa na suala la lugha ya Taifa kuwa kama kitambulisho cha Taifa husika, kwa mfano, lugha ya Kiswahili nchini Tanzania inakuwa kama nembo ya Taifa, kwa sababu ni sehemu ya utamaduni yaani mila na desturi za Watanzania. Dhana ya lugha ya Taifa imetumika kiutofauti ...

Pijini na krioli

Pijini na Krioli ni aina za lugha mpya ambazo zinajitokeza katika mazingira ya pekee. Yafuatayo ni maelezo juu ya tofauti na mahusiano kati ya aina hizo mbili katika asili na matumizi. Lugha zote mbili, Pijini na Krioli, ni lingua franka.

                                     

ⓘ Isimujamii

  • Isimujamii pia isimu jamii ing. sociolinguistics ni tawi la isimu ambalo huchunguza uhusiano kati ya lugha na jamii. Aidha inajihusisha na athira yeyote
  • mfumo wa maneno sintaksi kuhusu mfumo wa sentensi semantiki kuhusu maana isimujamii kuhusu uhusiano kati ya lugha na jamii TUKI 1990, Kamusi Sanifu ya Isimu
  • uzungumzaji si lahaja. Uchambuzi na uchanganuzi wa lahaja ni tawi la isimujamii Lahaja hutofautishwa kulingana na vipengele vifuatavyo: vipengele vya
  • kijamii za matumizi ya lugha. Wengine hudai kuwa taaluma hiyo ni sehemu ya isimujamii TUKI 1990, Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
  • cha Dar es Salaam Buliba, Aswani, Kimani Njogu & Alice Mwihaki 2006, Isimujamii kwa Wanafunzi wa Kiswahili Nairobi: The Jomo Kenyatta Foundation Lango
  • cha Dar es Salaam Buliba, Aswani, Kimani Njogu & Alice Mwihaki 2006, Isimujamii kwa Wanafunzi wa Kiswahili Nairobi: The Jomo Kenyatta Foundation Lango
                                     

Isimu amali

Isimu amali ni tawi la isimu ambalo hushughulikia uchambuzi na uchanganuzi wa lugha kupitia kwa maoni ya mtumiaji wa lugha husika. Hasa taaluma hiyo inachunguza uchaguzi wa miundo wa maneno anaoufanya msemaji, vikwazo vya kijamii msemaji anavyokabiliana navyo katika matumizi yake ya lugha, na athari nyingine za kijamii za matumizi ya lugha. Wengine hudai kuwa taaluma hiyo ni sehemu ya isimujamii.

                                     

Ubadilishaji msimbo

Ubadilishaji msimbo ni kitendo cha mtu anayezungumza lugha fulani kumalizia tungo kwa lugha nyingine ambayo ni tofauti na aliyoanzia kuzungumza. Hali hii hutokana na uwililugha; yaani mtu kuwa na ujuzi wa lugha mbili sawasawa. Mfano wa ubadilishaji msimbo: I like my mama anayenipenda pia. Jabari anakwenda shule everyday.