ⓘ Jeshi

Jeshi

Jeshi ni jumla ya watu wanaopewa mamlaka ya kutumia nguvu ya silaha kutetea nchi kwa niaba ya dola au kutekeleza maagizo ya serikali dhidi ya maadui wa nje. Neno linatumika hasa kwa kutaja jeshi la ardhi, jeshi la wanamaji na jeshi la anga.

Jeshi la majini

Jeshi la majini au Jeshi la wanamaji ni kitengo cha pekee cha jeshi la mataifa mengi kilicho tayari kushindana na maadui kwenye maji hasa baharini. Linajumlisha askari, manowari, meli za kuasaidia manowari, mabandari ya pekee na vituo vingine na pia eropleni za vita ya bahari. Ni hasa nchi zenye pwani la bahari ambako kuna jeshi la pekee la wanamaji. Chanzo katika historia yalikuwa majeshi ya wanamaji ya Karthago, Ugiriki ya Kale na Dola la Roma. Tangu karne ya 19 Uingereza ilikuwa na jeshi la wanamaji kubwa duniani, na katika karne ya 20 nafasi yake ilichukuliwa na wanamaji wa Marekani ha ...

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ni jeshi lililoanzishwa mnamo mwezi Septemba katika mwaka wa 1964. Ilichukua nafasi ya jeshi la Tanganyika Rifles lililorithiwa na ukoloni wa Waingereza.

Jeshi Jekundu

Jeshi Jekundu lilikuwa jina la majeshi ya Umoja wa Kisovyeti tangu kuanzishwa kwake hadi mwaka 1946.

Jeshi la anga

Jeshi la anga ni jeshi linalotumia ndege n.k. Jeshi la anga hutumia ndege hizo kwa ajili ya kusafirisha wanajeshi na mabomu kama sehemu wanayokwenda kushambulia ni mbali sana na walipo.

Majeshi ya Ulinzi ya Kenya

Majeshi ya Ulinzi ya Kenya ni vikosi vya kijeshi vya Jamhuri ya Kenya: Jeshi la Ardhi la Kenya, Jeshi la Wanamaji la Kenya, na Jeshi la Anga la Kenya huunda vikosi vya ulinzi. Muundo wa sasa wa majeshi hayo ulifanywa mwaka 2010 na Katiba ya Kenya ya 2010. Aidha, KDF huongozwa na Sheria ya Majeshi ya ulinzi ya Kenya ya mwaka 2012. Rais wa Kenya ndiye Amirijeshi mkuu. Mara kwa mara, vikosi hivyo vimehusika katika ulinzi wa amani duniani. Tume ya Waki, ilipongeza utayari wake na kuvichukulia "kuwa walitimiza wajibu wake vizuri." katika vurugu ya mwaka 2008 Hata hivyo, kumekuwa na madai makubw ...

Kambi ya jeshi Lugalo

Kambi ya jeshi Lugalo ni kambi kubwa ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania iliyoko jijini Dar es Salaam kwenye barabara ya Bagamoyo. Ilianzishwa wakati wa ukoloni wa Uingereza kama kambi ya Kings African Rifles. Ilipewa jina la "Colito Barracks" baada ya ushindi wa kikosi kutoka Tanganyika juu ya Waitalia katika mapigano ya Alaba Kulito huko Ethiopia tarehe 19 Mei 1941, wakati wa Vita Kuu ya Pili. Uasi wa jeshi la Tanganyika Rifles wa mwaka 1964 ulianza hapo kwa njia ya mgomo wa wanajeshi. Baada ya uhuru jina la kambi lilibadilishwa ili kukumbuka ushindi wa Wahehe chini ya mtemi Mkwaw ...

Schutztruppe

Schutztruppe ilikuwa jina la jeshi la kikoloni la Ujerumani hadi Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Ilifanywa na askari Waafrika chini ya amri wa maafisa Wajerumani. Ilianzishwa katika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani hasa Tanganyika ya baadaye ikaendelea kupanuliwa pia katika makoloni ya Afrika ya Kusini-Magharibi ya Kijerumani Namibia ya leo na Kamerun. Katika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani jeshi hilo lilikuwa na vikosi 14 vyenye askari 2.500 kwa jumla. Chini ya mkuu Paul von Lettow-Vorbeck Schutztruppe ilipiga Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia ikaweza kuendelea hadi mwisho wa vita na kusalimu a ...

Kanali

Kanali ni cheo cha afisa wa jeshi chini ya safu ya afisa wa jumla. Hata hivyo, katika vikosi vingine vya kijeshi, kama vile vya Iceland au Vatikano, kanali ni cheo cha juu zaidi. Pia hutumiwa katika baadhi ya vikosi vya polisi na mashirika ya kiserikali. Kihistoria, katika karne ya 17, karne ya 18 na karne ya 19, kanali alikuwa kawaida katika jeshi. Matumizi ya kisasa ni tofauti sana. Cheo cha Kanali ni kawaida juu ya cheo cha luteni kanali. Cheo cha juu kinaitwa brigedia au mkuu wa brigedi. Nafasi sawa katika majeshi ya baharini zinaweza kuitwa nahodha au nahodha wa meli.

Mamluki

Mamluki ni askari aliyekodiwa ambaye hayuko katika kikosi cha jeshi la nchi. Mamluki hushiriki katika vita kwa ajili ya pesa au malipo mengine badala ya siasa au uzalendo.

Wojtek (Dubu)

Wojtek alikuwa dubu wa kahawia wa Syria alinunuliwa, kama mtoto mchanga, katika kituo cha reli huko Hamadan, Iran, na askari wa Polandi ambao waliokolewa kutoka Umoja wa Kisovieti. Ili kupata riziki yake na usafiri, aliandikishwa rasmi kama askari wa kawaida, na baadaye akapandishwa cheo na kuwa koplo. Aliandamana na askari wenzake kwenda Italia, akihudumu katika kikundi cha 22nd Artillery Supply Company. Wakati wa mapigano ya Monte Cassino, nchini Italia mnamo 1944, Wojtek alisaidia kubeba makreti ya risasi na kuwa mashuhuri na kutembelea majemadari na wakuu wa nchi. Baada ya vita, kuacha ...

                                     

ⓘ Jeshi

  • maadui wa nje. Neno linatumika hasa kwa kutaja jeshi la ardhi, jeshi la wanamaji na jeshi la anga. Kazi ya jeshi ni kulinda nchi dhidi ya maadui wa nje kutetea
  • Jeshi la majini au Jeshi la wanamaji ni kitengo cha pekee cha jeshi la mataifa mengi kilicho tayari kushindana na maadui kwenye maji hasa baharini. Linajumlisha
  • Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ kwa Kiingereza Tanzania People s Defense Force TPDF ni jeshi lililoanzishwa mnamo mwezi Septemba katika
  • Jeshi Jekundu kwa Kirusi Красная армия krasnaya armiya, kwa Kiingereza Red Army lilikuwa jina la majeshi ya Umoja wa Kisovyeti tangu kuanzishwa kwake
  • Jeshi la Misri ni vikosi vya kijeshi vya nchi ya Misri. Jeshi hilo ndilo kubwa katika Afrika na Mashariki ya Kati, likiwa na wanajeshi wa nchi kavu, wa
  • Jeshi la anga ni jeshi linalotumia ndege n.k. Jeshi la anga hutumia ndege hizo kwa ajili ya kusafirisha wanajeshi na mabomu kama sehemu wanayokwenda kushambulia
  • Jeshi la ardhi ni mkono wa jeshi la nchi unaojumlisha vikosi vyote vilivyo tayari kupigania maadui kwenye nchi kavu, tofauti na mikono mingine inayoshughulika
  • Jeshi la Kujenga Taifa kifupi JKT ni tawi la jeshi la Tanzania. Liliasisiwa tarehe 10 Julai 1963 kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa vijana wa Kitanzania
  • ni vikosi vya kijeshi vya Jamhuri ya Kenya: Jeshi la Ardhi la Kenya, Jeshi la Wanamaji la Kenya, na Jeshi la Anga la Kenya huunda vikosi vya ulinzi. Muundo
                                     

Jeshi la Misri

Jeshi la Misri ni vikosi vya kijeshi vya nchi ya Misri. Jeshi hilo ndilo kubwa katika Afrika na Mashariki ya Kati, likiwa na wanajeshi wa nchi kavu, wa baharini, wa angani na Jeshi la Wananchi. Lilianzishwa mwaka 1922.

                                     

Jeshi la ardhi

Jeshi la ardhi ni mkono wa jeshi la nchi unaojumlisha vikosi vyote vilivyo tayari kupigania maadui kwenye nchi kavu, tofauti na mikono mingine inayoshughulika kazi ya ulinzi wa taifa baharini au hewani. Watu kwenye jeshi la ardhi huitwa askari au wanajeshi. Hupangwa kwa vikosi mbalimbali wakitumia silaha na vifaa kama vile bunduki, mizinga, vifaru, helikopta na mengine.

                                     

Jeshi la Kujenga Taifa

Jeshi la Kujenga Taifa ni tawi la jeshi la Tanzania. Liliasisiwa tarehe 10 Julai 1963 kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa vijana wa Kitanzania juu ya uzalendo, maadili pamoja na nidhamu.

                                     

Amirijeshi mkuu

Amirijeshi mkuu (kwa Kiingereza: "commander-in-chief" ni kiongozi wa majeshi yote katika nchi fulani. Kwa mfano nchini Tanzania amirijeshi mkuu ni rais: ndiye anayetoa amri kwa majeshi yake. Kwa sasa amirijeshi wa sasa Tanzania ni John Pombe Magufuli.

                                     

Askari

Askari ni mtu ambaye anahusika na mambo ya ulinzi na usalama katika nchi, pia hufanya kazi hiyo kama sehemu ya jeshi. Askari anaweza kuwa mtu aliyechaguliwa, afisa asiyeagizwa, au afisa wa jeshi.

                                     

Brigedia

Brigedia ni cheo cha jeshi, ukamilifu ambao unategemea nchi. Katika nchi nyingine, ni cheo cha juu kuliko koloneli, sawa na mkuu wa brigedi, kwa kawaida amri ya brigedi ya askari elfu kadhaa. Katika nchi nyingine, ni cheo ambacho hakijatumiwa.

                                     

Manuva

Manuva, ni mbinu na mikakati makini kama vile ya kivita. Wanajeshi wanafanya mazoezi mengi makali ya namna hiyo yakihusisha mwili na akili ili kujihakikishia ushindi katika mapigano.