ⓘ Jinsia

Jinsia

Jinsia ni hali ya viumbe hai wengi kuwa wa kiume au wa kike, jambo muhimu katika mpango wa kuendeleza uhai kupitia uzazi. Hata hivyo, si viumbe vyote vinaendeleza uhai kwa njia ya uzaliano kijinsia: viumbehai vya mfuto kama bakteria vyenye mwili wa seli moja tu vinatumia uzaliano peke ambako seli hujigawa. mimea kadhaa huzaa kwa kutenga tu sehemu ya mizizi inayoanzisha mmea mpya; mbinu hiyohiyo hufuatwa kwa kutumia kipandikizi cha kupanda katika kilimo. Kuna pia njia ya kujizalisha ambayo ni namna ya pekee ya uzalioni kijinsia. Mimea kama karanga na pia wanyama kadhaa mfano vyawa na samaki ...

Ndoa za jinsia moja

Ndoa za jinsia moja ni makubaliano kati ya wanaume wawili au wanawake wawili ili kuishi pamoja kwa mfano wa mume na mke. Ndoa ya namna hiyo ni halali katika nchi zaidi ya ishirini duniani. Nchi hizo kwa mwaka wa 2019, na kwa mpangilio wa muda wa idhini ni: Uholanzi, Ubelgiji, Uhispania, Kanada, Afrika Kusini, Norwei, Uswidi, Ureno, Aisilandi, Ajentina, Denimaki, Brazil, Ufaransa, Uruguay, Nyuzilandi, Uingereza na Welisi, Uskoti, Luxemburg, Marekani, Eire, Grinilandi, Kolombia, Ufini, Visiwa vya Faroe, Malta, Ujerumani, Australia, Austria, Taiwan na Ekuador. Majimbo mengi huko Mexiko pia hu ...

Chembeuzi za jinsia

Chembeuzi za jinsia ni mbili kati ya chembeuzi za binadamu na za wanyama mbalimbali zinazoongoza utengenezaji wa seli zote za mwili kadiri ya urithi wa wazazi unaotunzwa katika DNA. Hizo chembeuzi za jinsia kwa binadamu ni chembeuzi X na chembeuzi Y. Ndizo zinazosababisha mtu kuwa mwanamume au mwanamke, na vilevile wanyama mbalimbali kuwa wa kiume au wa kike. Baba tu ana chembeuzi Y pamoja na ile ya X na hivyo anaweza kumrithisha mwanae, ambaye kwa njia hiyo atakuwa wa kiume. Kumbe mama ana jozi la chembeuzi X asiweze kurithisha chembeuzi Y. Ndiyo maana ni baba tu anayesababisha jinsia ya ...

Ndoa

Ndoa ni muungano kati ya watu wawili au zaidi unaokubaliwa na kuheshimiwa na jamii. Tukio la kuanzisha ndoa linaitwa harusi, na kabla ya ndoa kuni kipindi cha uchumba ambapo watu hao wawili walio kubaliana wanachunguzana tabia na kujifunza au kujuana zaidi baina yao. Kama watu wanaohusika wakikomesha ndoa yao kisheria, hali hii inaitwa talaka. Katika utamaduni wa nchi nyingi uhusiano huo ni kati ya mwanamume mmoja na mwanamke mmoja tu na unalenga ustawi wao na uzazi wa watoto katika familia. Katika nchi nyingine, hasa za Kiislamu na za Afrika, inakubalika ndoa kati ya watu wawili ambao mmo ...

Mwanamke

Mwanamke ni mwanadamu wa jinsia ya kike, kwa maana anafaa kuwa mke. Ndiyo sababu kwa kawaida anaitwa hivyo aliyefikia utu uzima au walau amebalehe. Kabla ya hapo huwa anaitwa mtoto wa kike, binti, mwanamwali au msichana. Baada ya kuzaa anaitwa kwa kawaida mama, jina lenye heshima kubwa katika utamaduni wa aina nyingi. Akianza kupata wajukuu, anajulikana pia kama bibi. Wanawake ni takriban nusu ya binadamu wote, wengine huwa wanaume. Ndizo jinsia mbili ambazo zinahesabiwa kwa kawaida kati ya binadamu. Mwanamke ana tabia zake za pekee upande wa mwili, nafsi na roho, na tofauti kati yao na wa ...

Baba

Baba ni mwanamume aliyemzaa mtoto au anamlea. Katika uzazi, baba ndiye anayesababisha jinsia ya mtoto kwa kumrithisha kromosomu Y mtoto wa kiume au kromosomu X tu mtoto wa kike. Saikolojia inaonyesha pia umuhimu wa kuwepo kwa baba mwenye pendo, akishirikiana na mama, katika kukua kwa mtoto.

                                     

ⓘ Jinsia

 • Jinsia ni hali ya viumbe hai wengi kuwa wa kiume au wa kike, jambo muhimu katika mpango wa kuendeleza uhai kupitia uzazi. Hata hivyo, si viumbe vyote vinaendeleza
 • Ndoa za jinsia moja ni makubaliano kati ya wanaume wawili au wanawake wawili ili kuishi pamoja kwa mfano wa mume na mke. Ndoa ya namna hiyo ni halali katika
 • Chembeuzi za jinsia pia: kromosomu za jinsia ing. sex chromosomes ni mbili kati ya chembeuzi za binadamu na za wanyama mbalimbali zinazoongoza utengenezaji
 • inayozidi kuongezeka ya nchi zimeanza kuruhusu ndoa kati ya watu wawili wa jinsia moja. Kumbe nchi nyingine zinapinga vikali jaribio hilo kama kinyume cha
 • Kaka ni jina ambalo linatumika kwa ndugu wa jinsia ya kiume, hasa akimzidi umri mwingine ambaye ni mdogo wake, lakini pengine hata kwa mdogo ikiwa msemaji
 • Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Kiingereza: Ministry of Community Development, Gender and Children kifupi MCDGC ni wizara ya serikali
 • Dada ni jina ambalo linatumika tu kwa ndugu wa jinsia ya kike tu. Jina hilo laweza kutumika kuanzia kwa mtoto mwenye umri mdogo hadi mkubwa, bali hutumika
 • Mke ni binadamu wa jinsia ya kike ambaye ameoana na mwanamume. Katika adhimisho la ndoa, mwanamke anaitwa pia bibi arusi. Mwanamke wa namna hiyo anaendelea
 • Mwanamke ni mwanadamu wa jinsia ya kike, kwa maana anafaa kuwa mke. Ndiyo sababu kwa kawaida anaitwa hivyo aliyefikia utu uzima au walau amebalehe. Kabla
 • Mume ni binadamu wa jinsia ya kiume ambaye ameoana na mwanamke. Katika adhimisho la ndoa, mwanamume anaitwa pia bwana arusi. Mwanamume wa namna hiyo anaendelea
 • mwanamume aliyemzaa mtoto au anamlea. Katika uzazi, baba ndiye anayesababisha jinsia ya mtoto kwa kumrithisha kromosomu Y mtoto wa kiume au kromosomu X tu
                                     

Kaka

Kaka ni jina ambalo linatumika kwa ndugu wa jinsia ya kiume, hasa akimzidi umri mwingine ambaye ni mdogo wake, lakini pengine hata kwa mdogo ikiwa msemaji ni ndugu wa kike anayetaka kuonyesha heshima kwa jinsia ambayo inapewa haki zaidi katika masuala mbalimbali kadiri ya utamaduni husika. Mara nyingi mtoto wa kiume wa kwanza ndiye mwenye nafasi ya pekee katika familia, k.mf. katika Biblia.

                                     

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto) ni wizara ya serikali nchini Tanzania. Ofisi kuu ya wizara hii zipo mjini Dar es Salaam.

                                     

Dada

Dada ni jina ambalo linatumika tu kwa ndugu wa jinsia ya kike tu. Jina hilo laweza kutumika kuanzia kwa mtoto mwenye umri mdogo hadi mkubwa, bali hutumika pia kuonyesha heshima kwa mwanamke mkubwa.

                                     

Mke

Mke ni binadamu wa jinsia ya kike ambaye ameoana na mwanamume. Katika adhimisho la ndoa, mwanamke anaitwa pia bibi arusi. Mwanamke wa namna hiyo anaendelea kuitwa mke hadi ndoa ivunjike kwa kifo cha mumewe hapo ataanza kuitwa "mjane" au kwa talaka hapo ataanza kuitwa "mtaliki". Utengano haumuondolei hadhi ya kuwa mke wala haki zinazoendana nayo kadiri ya sheria na desturi za jamii husika.

                                     

Mume

Mume ni binadamu wa jinsia ya kiume ambaye ameoana na mwanamke. Katika adhimisho la ndoa, mwanamume anaitwa pia bwana arusi. Mwanamume wa namna hiyo anaendelea kuitwa mume hadi ndoa ivunjike kwa kifo cha mkewe hapo ataanza kuitwa "mjane" au kwa talaka hapo ataanza kuitwa "mtaliki". Utengano haumuondolei hadhi ya kuwa mume wala haki zinazoendana nayo kadiri ya sheria na desturi za jamii husika.

                                     

Chuchu

Chuchu ni kichirizi kinachounganisha kwa viwele. Mamalia wa kike hutumia chuchu kwa ajili ya kunyonyesha watoto wadogo. Ziwa la mamalia wa kike na wa kiume limetengenezwa kwa muundo mmoja. Uzalishaji wa maziwa kwa ajili ya kunyonyesha unadhibitiwa na homoni. Hii ina manaa kwamba wanaume hawawezi kutumia matiti kuzalisha maziwa isipokuwa ikiwa wana matatizo na homoni zao.

                                     

Gameti

Gameti ni kiini cha kijinsia ambacho kinaungana na kiini cha jinsia nyingine ili kutunga mimba katika viumbehai wanaozaliana. Gameti hubeba nusu ya habari ya maumbile ya mzazi inayorithishwa kwa mtoto. Kwa binadamu na baadhi ya wanyama ukubwa wa gameti ni tofauti sana, ile ya kike ovum, yaani kijiyai ikiwa mara 100.000 kuliko ile ya kiume mbegu ya shahawa. Jina la gameti lilianzishwa na mwanabiolojia wa Austria Gregor Mendel.

                                     

Jike

Jike ni kiumbe yeyote yule ambaye ana jinsia ya kike. Jike laweza kuwa Simba, Nyani, Sungura, Mbwa, Nyati, Mbweha na kadhalika, ila kwa binadamu huitwa mwanamke. Hivyo basi kundi hili la viumbe huchangia kwa kiasi kikubwa sana kuzaliwa na kulea hasa viumbe vichanga kwa kuwanyonyesha na kuwahakikishia mahitaji mengine ya msingi kama vile kuwasafisha na kuwahakikishia ulinzi dhidi ya wanyama walanyama, kwa mfano jike la nyati hujitahidi kumlinda mwanaye wakati wote wawapo mbugani.

                                     

Kinembe (anatomia)

Kinembe ni kinyama kinachotokeza katika uchi wa mwanamke kinachomsaidia apate msisimko wakati wa kujamiana. Ndiyo sehemu ya kwanza kulengwa na ukeketaji, ambao unaendelea kufanyika hasa barani Afrika, ingawa unapingwa na wengi kwa misingi ya afya na haki za wanawake. Nchi kama Tanzania na Kenya zimefanikiwa kwa kiwango kikubwa kupinga suala hilo la ukeketaji sababu linakiuka haki za msingi za binadamu

                                     

Mfumo wa uzazi

Mfumo wa uzazi ni mfumo wa ogani za kijinsia ndani ya mwili zinazofanya kazi pamoja katika kulenga uzazi wa kijinsia. Mbali na ogani hizo, dutu mbalimbali zisizo hai, kama vile viowevu, homoni n.k., ni muhimu katika kukamilisha mfumo wa uzazi na kuuwezesha kufanikiwa. Tofauti na mifumo mingine mbalimbali ya viumbe hai, mara nyingi jinsia za spishi zenye tofauti za kijinsia zina tofauti muhimu ambazo zinawezesha urithi wa wazazi kuchanganyikana kwa faida ya afya ya watoto.